Sunday, March 03, 2013

MAZOEZI YA MBIO ZA POLE POLE JUMAPILI TAR 3 MACHI YANOGA

Kama ilivyo ada, baada ya kuhairishwa ka safari ya kwenda kunduchi wanamichezo toka vilabu vya Namanga na Biafra waliamua kufanya mazoezi pamoja kwa kuanzia Namanga na na kuishia Biafra. Mbio hizo zilipita katika bara ya Ubalozi (USA), Old bagamoyo, Migombani, Mission Mikocheni, Mwai Kibaki, Mwinjuma, Hospitali ya Mwananyamala, Dunga, Kawawa na kuishia 90 Degrees Pub ambapo ni Makao makuu ya klabu y Biafra. 
Jogging barabara ya ubalozi (USA)


Katibu Mkuu wa Biafra akiongoza jahazi







Mara baada ya kumaliza jogging wanamichezo waliendelea na mazoezi ya aerobics yaliyokuwa yakiongozwa na mwanabiafra Khamis Suleiman (mwenye fulana nyekundu pichani chini).
 


Wanamichezo wote baada ya kutula walikaribishwa na Katibu Mkuu wa Biafra na baada ya pongezi za kushiriki na kumaliza mbio kwa wanamichezo wotw, taarifa mbalimbali zilitolewa ikiwemo ya  maendeleo ya mchakato wa kuanzisha Shirikisho la Jogging Manispaa ya Kinondoni pamoja na hatua zilizochukuliwa katika kuhuisha Chama cha Mchezo wa Jogging Kinondoni.
Katibu wa Biafra akiwakaribisha wanamichezo





Kutoka kushoto; Mary, Kaka Poli, na Bebee

 Safari yetu ya Kunduchi itafanyika jumapili ya tarehe 10 Machi, 2013. Karibuni wadau wote!!!

MAZOEZI NI AFYA ACHA KUJIACHIA!!!

No comments:

Post a Comment