Thursday, March 21, 2013

JOGGING; HISTORIA, UMUHIMU NA USALAMA WAKATI WA MAZOEZI (SEHEMU YA PILI))

Katika sehemu ya kwanza ya makala hii tuliangalia zaidi maana ya jogging pamoja na utaratibu wake. Fuatilia makala haya kwa sehemu ya pili juu ya historia ya jogging Tanzania

Hatuwezi kuizungumzia jogging bila ya kutaja au kuihusisha wilaya ya Temeke katika mkoa wa Dar es Salaam. Tangu miaka ya 80, Wakaazi wengi wa wilaya ya Temeke wamekuwa ni watu ambao wanajihusisha na michezo mbalimbali moja kwa moja. Hivyo basi, hata jogging ilianza kushika kasi wilaya ya Temeke kabla ya kusambaa katika wilaya nyingine za Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. 
Wana jogging wakikatiza barabara ya uwanja wa taifa
  
Wana jogging wakikatia barabara ya Kilwa
Temeke Jogging ni moja kati ya klabu kongwe za jogging Tanzania na ni miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wa mchezo huo. Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu za mwanzo kabisa kujikusanya na kuanzisha klabu ambayo inajihusisha na mchezo wa jogging zaidi. 
Wana jogging Temeke
Viongozi wa Tameke Jogging
Baada ya Temeke Jogging kuanzisha klabu yao, makundi mengine mengi nayo yakajiunda na kuanzisha vilabu vyao. Kama ukipata fursa ya kutembelea Temeke siku za mwisho wa wiki hasa majira ya asubuhi utashuhudia makundi kwa makundi ya watu wakifanya jogging. Kutoka Temeke jogging ikasambaa hadi wilaya nyingine Dar es Salaam ambapo kwa wilaya ya Kinondoni Klabu ya kwanza kuanzishwa ilikuwa  ni Namanga Jogging.
Namanga Jogging wakikatiza barabara ya Ali Hassan Mwinyi
 Baada ya kustawi kwa klabu ya Namanga, vilabu vingine kadhaa vya jogging katika Wilaya ya Kinondoni hasa baada ya Kanali Fabian Massawe ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni (wakati huo) kuhimiza wenyeviti wa serikali za mitaa katika wilaya ya Kinondoni kuanzisha vilabu vya jogging kwenye mitaa yao ili kulinda afya za wakaazi wa Kinondoni. 

Miongoni mwa klabu zilizoanzishwa baada ya kupata hamasa ya Namanga ni klabu ya michezo ya Biafra ambayo pamoja na michezo mingine inajihusisha moja kwa moja na jogging ambapo wanachama pamoja na wadau wengine hujumuika pamoja siku za jumapili alfajiri na kufanya jogging.

Wanabiafra wakiwa kwenye jogging
Kwa sasa wilaya ya Kinondoni kama ilivyo Temeke, siku za mwisho wa juma watu wengi hujitokeza na kufanya jogging katika barabara mbalimbali.

Itaendelea ...........

No comments:

Post a Comment