Saturday, March 24, 2012

Friday, March 23, 2012

JE UNAPENDA KUJIFUNZA, KUFAHAMU NA KUPIMA SARATANI YA KIBOFU????

KAMA JIBU NI NDIO!!!

Siku ya jumapili tarehe 25 Machi, 2012 pale Leecars ambapo ni makao makuu ya klabu ya Michezo ya Namanga kuanzia saa 3 kamili asubuhi kutatolewa elimu na tiba bure ya ugonjwa wa kansa ya kibofu.

Picha ya kibofu kilichoathiriwa na saratani ya kibofu


Ila kukuarifu tu kidogo kuhusu saratani hiyo ni: -
  1. Saratani ya kibofu  (Prostate Cancer) ni saratani inayoshambulia kibofu cha mkojo na mfumo mzima wa kukojoa
  2. Madhara yatokanayo na saratani hii ni; Upungufu wa damu mwilini, Kushindwa kuzuia mkojo na hivyo kujikojolea, Kupungua kwa tundu kwenye mrija wa kutolea mkojo (urethral stricture), Kuvimba kwa ureters kutokana na mkojo kushindwa kwenda kwenye kibofu cha mkojo.
  3. Kuna aina mbalimbali za saratani ya kibofu cha mkojo kama vile: transitional cell carcinoma, Squamous cell carcinoma na Adenocarcinoma,
  4. Dalili za saratani ya kibofu ni; Kukojoa damu (gross haematuria), Maumivu au kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation), Kuhisi bado hujamaliza mkojo baada ya kukojoa, kuhisi kukojoa lakini mkojo hautoki unapokojoa, maumivu ya tumbo,
  5. Watu walio kwenye hatari ya kupata saratani ya kibofu ni; Wale wanaofanyakazi kwenye saluni za nywele, Wanaofanya kazi ya kupaka rangi, Wafanyakazi wa viwanda vya nguo, Wanaofanya kazi kwenye viwanda vya ngozi, Wafanyakazi wa viwanda vya mipira (rubber), watu wanaofanya kazi zinazohusiana na kemikali moja kwa moja, watu wanaovuta sigara, madereva wa malori, n.k.
  6. Tiba ya saratani ya kibofu imegawanyika katika makundi manne; tiba ya mionzi, dawa, upasuaji na  immunotherapy ama biological therapy.
Tembelea blogu ya TANZAMED ili upate kujifunza mengi yanayohusiana na saratani ya kibofu na magonjwa mengine. 

Sunday, March 11, 2012

TAREHE YA UCHAGUZI MKUU WA VIONGOZI YASOGEZWA MBELE HADI TAREHE 25 MACHI, 2012

Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Biafra anauwatangazia wanachama wote pamoja na umma kwa ujumla kwamba uchaguzi mkuu wa kwanza wa viongozi wa klabu hiyo ambao ulipangwa kufanyika mnamo tarehe 11 Machi, 2012 umehairishwa hadi tarehe 25 Machi, 2012. Kusogezwa mbele kwa uchaguzi kutaiwezesha klabu  kufanya semina ya uongozi kwa wagombea pamoja na wanachama wote kwa ujumla. Seimna hiyo imepangwa kufanyika tarehe 18 Machi, 2012. Mwezeshaji katika semina hiyo atakuwa ni mkurugenzi wa klabu ya Biafra pamoja na wawezeshaji wengine.

Kutoka kushoto Abdul Mollel (Mwenyekiti), Bethwelly Kyando (Katibu Mkuu Msaidizi), Yahya Poli (Katibu Mkuu)