Monday, December 24, 2012

SALAAM ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA TOKA BIAFRA!

Wakati wakristo wakiwa katika maandalizi ya sikukuu ya kuzaliwa mwokozi, Yesu kristo mnamo tarehe 25 Disemba pamoja na maandalizi ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013, klabu ya michezo ya Biafra inapenda kuwatakia wanachama, wapenzi, mashabiki pamoja na wadau wote wa michezo krismasi njema pamoja na heri ya mwaka mpya 2013.

Katika kipindi hiki cha mapumziko ya sikukuu, mazoezi yataendelea kila jumapili kama kawaida! Karibuni wote.

Wednesday, December 05, 2012

HABARI MCHANGANYIKO ZINAZOHUSU VILABU MBALIMBALI VYA JOGGING MKOA DAR ES SALAAM

Mwezi disemba ndio umeingia. Katika mfumo wa kupeana taarifa mbalimbali zinazohusu klabu zetu zinazojihusisha na mchezo wa mbio za pole pole (jogging), katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi disemba kuna matukio kadhaa yaliloyofanyika na yatakayofanyika. Kama ilivyo ada, klabu ya michezo ya Biafra ilijumuika pamoja na klabu ya Namanga katika na kufanya mazoezi ya pamoja jumapili ya tarehe 2 Disemba. 

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ally Selemeani (mwenye bukta nyeusi) akiiwakilisha vyema Biafra
Mazoezi hayo yaliyofanyika kuzunguka barabara na mitaa mbali ya Namanga na Msasani yalianzia na kumalizikia Leecars Pub ambapo ni makao makuu ya klabu ya Namanga. Mara baada ya mazoezi ya pamoja, wanamichezo wote walijumuika na kujadiliana machache kwa ajili ya maendeleo ya klabu zote ikiwemo pea kupashana taarifa mbalimbali.

Kule Magomeni nako, klabu za Mzimuni na Taifa Jogging zilikutana na kufanya mazoezi ya pamoja ya mbio za pole pole na kisha kucheza mechi za mpira wa miguu (wanaume) na mpira wa pete (wanawake). Picha zote za michezo kati ya Taifa na mzimuni Jogging ni kwa hisani ya Taifa Jogging.
Wana Taifa na Mzimuni Jogging kwenye mchakamchaka

Kipindi cha mapumziko kwa mechi ya mpira wa miguu wanaume

Wachezaji wa mpira wa pete kutoka Taifa Jogger katika picha ya pamoja

Klabu ya michezo ya Namanga imejiandaa kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wake mnamo tarehe 9 Disemba, 2012. Akitoa taarifa ya kufanyika kwa mkutano huo mbele ya makatibu wa vilabu vya Biafra, Msasani na Kunduchi Kwanza, Katibu Mkuu wa Namanga ndugu Mangole alieleza kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Maandalizi ya mkutano huo yanaendelea. Alieleza kuwa vilabu rafiki vyote vitaalikwa kuhudhuria mkutano. 
Mwenyekiti wa namanga Sports Club ndugu David Mwaka (aliyesimama) akichangia mada kwenye kikao cha maandalizi ya mkutano mkuu: Picha kwa hisani ya John Badi)
 Kwa habari zaidi kuhusu mkutano huo bofya hapa.

TUNAWATAKIA WANA NAMANGA MKUTANO MKUU WENYE MAFANIKIO

Saturday, December 01, 2012

1.12. 2012: SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Tangu Disemba 1, 1988 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya UKIMWI duniani. Wazo la kuadhimisha siku hiyo lilitolewa na James W. Bunn naThomas Netter ambao walikuwa ni maofisa habari (Global Programme on AIDS) kwenye Shirika la Afya Duniani. Dhumuni la kuadhimisha siku hiyo ni kutoa fursa kwa watu duniani kote kuungana katika mapambano dhidi ya VVU
Utepe Mwekundu
Huu ni wakati muafaka kwa jamii nzima wakiwemo wanamichezo pia kutafakari juu ya janga la UKIMWI. 

UKIMWI UNAUA! CHUKUA HATUA SASA, JILINDE NA MLINDE MWENZAKO PIA.

Wednesday, November 28, 2012

BONANZA LA MICHEZO NA BURUDANI LAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI TAR 17 NOVEMBA, 2012

Jumamosi tarehe 17 Novemba, 2012 wanamichezo kutoka katika klabu mbalimbali za jogging pamoja na wadau wengine walikutana katika Bonanza lilioandaliwa na klabu ya michezo ya Biafra. Bonanza hilo lililopambwa na Serengeti Breweries kupitia bia ya Serengeti lilihusisha michezo pamoja na Burudani mbalimbali.

Add caption


Wanamichezo walikutana makao makuu ya Biafra, 90 Degrees pub kuanzia saa 12 asubuhi. Mazoezi ya mbio za pole pole kuzunguka maeneo mbalimbali ya manispaa ya Kinondoni, kata ya Mwananyamala zilifanyika punde baada ya vilabu vyote alikwa kufika klabuni.

Wanamichezo toka Mzimuni jogging

Mara baada ya kumaliza mbio za pole pole, wanamichezo walijongea katika viwanja vya Biafra kwa michezo mbalimbali ikiwemo mechi ya soka la veterani kati ya Care Veterani na kombaini ya vilabu vya jogging.

Care Veterani
Mchezaji wa Care Veterani Said Babaa akijiandaa kupatiwa huduma ya kwanza

Ayoub Layson wa Biafra akiongoza katika mashindano ya kutembea na yai kwenye kijiko
Michezo ni furaha
 Baada ya michezo mbalimbali wanamichezo pamoja na wadau wengine walirejea klabuni ambapo burudani mbalimbali zilikuwa zikiendelea. Hatimaye ukafika wakati ambapo baadhi ya vilabu vilitoa zawadi kwa timu ya soka ya vijana ya Biafra ambapo klabu ya Seamens ya Kigamboni walitoa mpira halisi kwa timu hiyo.

Katibu Mkuu wa Seamen Club Kaka Elly akimkabidhi zawadi ya mpira Katibu Mkuu wa Biafra Yahya Poli

Katibu Mkuu wa Biafra akiuonesha mpira kwa washiriki wa Bonanza

Katibu Mkuu wa Biafra akishangilia zawadi ya mpira pamoja na Wana-Seamen

Baada ya kuguswa na zawadi ya mpira iliyotolewa na Seamen Club kwa timu ya vijana ya Biafra, Magogoni Veterani nao walichangia pesa taslimu Sh. 5000/= kwa ajili ya mfuko wa timu hiyo. 
Magogoni Vetrani wakijinadi

Kwa mbwembwe na adabu wakiwakilisha mchango kwa mweka hazina wa Biafra Bi. Asha M. W.

Baada ya matukio hayo mahususi wanamichezo waliendelea kupata burudani mbalimbali zilizoandaliwa kwenye bonanza hilo ikiwemo promosheni ya bia ya serengeti. 
Kilinge cha wana Seamen club

Kilinge cha Kunduchi Kwanza

Kilinge cha wanabiafra

Kilinge cha Namanga Sports Club

Kaka Mudi toka Temeke Jogging akiwaimbisha wanamichezo

Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Biafra Mustafa Muro (kulia)
Ummy wa Kunduchi Jogging (aliyesimama) akifuatilia jambo na Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed (mwenye shati la draft)




Wednesday, October 24, 2012

PONGEZI KWA MWANABIAFRA ROSE MWAKIBUGI KWA BIRTHDAY ILIYOPENDEZA

Wanabiafra pamoja na marafiki mbalimbali walijumuika pamoja katika sherehe ya kustukiza "suprise" ya kuzaliwa kwa mwnabiafra mwenzao Mrs. Rose Mwakibugi ambayo iliandaliwa na mwanabiafra mwingine ambaye pia ni mume wa bi Rose, kaka Robert Mwakibugi.
Keki ya Birthday
Katika kufungua sherehe hiyo Robert Mwakibugi alitumia fursa kwa kumpongeza mke wake kwa kutimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake na pia kwa upendo alionao kwake yeye mwenyewe pamoja na familia yao kwa ujumla. 
Mr.s Rose Mwakibugi - birthday girl akiwa ofisini kwake Chimbinga Unique Pub akishangaa yanayojiri                  
Wanabiafra kutoka kushoto Robert Mwakibugi, Yahya Poli, Rose Mwakibugi, na Jaqueline Barozi

Robert Mwakibugi akimlisha mkewe Rose Mwakibugi keki ya upendo

Bw. na Bi. Mwakibugi wakimlisha keki mtoto wa Habil ambaye pia ni mwanachama wa Biafra



Kwa upendeleo maalum, kwa niaba ya wanabiafra Makamu M/Kiti Bi. Jacqueline Barozi allilishwa keki na Rose mwakibugi akisaidiana na M/Kiti Abdul Mollel

Birthday girl akipongezwa
 
Mwamabiafra Henry Maseko akitoa mkono wa pongezi

Wanabiafra Henry Maseko kushoto na King A.Y. Mpore 
KWA NIABA YA WANACHAMA WOTE KLABU INATOA PONGEZI KWA BI ROSE MWAKIBUGI KWA SHEREHE YAKE YA BIRTHDAY, TUNAMTAKIA MAISHA MAREFU YENYE FURAHA, AMANI NA MAFANIKIO. KATIBU MKUU, BIAFRA SPORTS CLUB

Monday, October 22, 2012

MAZOEZI YA MBIO ZA POLE POLE JANA JUMAPILI YAWAKUTANISHA TENA WANABIAFRA

Kama ilivyo ada, Wanabiafra kila jumapili hujikusanya na kufanya mazoezi ya mbip za pole pole (jogging) kuzunguka maeneo mbalimbali ya Kinondoni. Mazoezi ya jana yaliwakutanisha zaidi ya wanachama 30 wa Biafra ambao wakubwa kwa wadogo. 
Mwenyekiti wa Kamatu ya Uchumi Ibrahim kilasa (mwenye miwani) akikimbia pamoja na watoto

Hujachelewa kujiunga na klabu yetu, karibu sana!

Monday, October 15, 2012

BIRTHDAY YA KAWE JOGGING YAFANA

Klabu ya mchezo wa mbio za pole pole ya Kawe jana tarehe 14 Oktoba, 2012 ilitimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Anjela Kairuki (Mb.). 
WanaKawe Jogging

Wanamichezo kutoka vilabu mbalimbali walishiriki katika hafla hiyo ambayo ilianza kwa mazoezi ya mbio za pole pole yaliyoanzia na kuishia katika vwanja vya Tanganyika Packers na hatimaye michezo mingine ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku na soka la vijana ambapo Biafra Youth Football Team ilitoka sare ya bila kufungana na timu ya vijana ya Kawe.

Mara baada ya michezo kumalizika wanamichezo wote walijumuika pamoja katika ukumbi wa Massae Pub ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Kawe jogging kwa shguli nyinginezo zilizoenda sambamba na hafla hiyo.
 


Thursday, October 11, 2012

BIAFRA JOGGING YAALIKWA KUSHIRIKI SHEREHE KUTIMIZA MWAKA MMOJA TANGU KUANZISHWA KWA KAWE JOGGING



Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa klabu ya Kawe Jogging, wanachama wa klabu hiyo wamealika klabu mbalimbali zinazojihusisha na uhamasisjaji wa mchezo wa mbio za pole pole mkoa wa Dar es Salaam katika kusherehekea maadhimisho hayo. Biafra Jogging, Mzimuni Jogging, Kunduchi Kwanza Jogging na klabu ni nyinginezo kwa pamoja zitafanya mazoezi ya mbio za pole pole na kisha kushiriki katika michezo mingine kama vile kuvuta kamba na  mpira wa miguu kwa wanawake na wanaume.

Wana-Kawe Jogging wakiwa katika Magofu ya Kaole mwanzoni mwaka 2012


Biafra Jogging wakiwa pamoja na Namanga Jogging mazoezini
Klabu ya michezo ya Biafra inatoa pongezi za dhati kwa Kawe Jogging na wanachama wake wote katika sherehe hizo za kutimiza mwaka mmoja. 

WE! WE! MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA

Monday, October 01, 2012

FRANCIS CHEKA AMTWANGA TENA KARAMA NYILAWILA

Jumamosi iliyopita tarehe 29 Oktoba, 2012 mtoto wa Kinondoni Msisiri ambaye kwa sasa anauwakilisha vyema mkoa wa Morogoro Francis Cheka alizidi kuonesha ubabe kwa mabondia wenzake hasa wa Tanzania baada ya kumtandika kwa TKO katika raundi ya sita mwanamasumbwi mwenye makeke na maneno mengi Kalama Nyilawila. Mpambano huo uliopigwa katika ukumbi wa PTA Sabasaba ulishuhudiwa na mamia ya mashabiki wa mchezo wa ngumi huku mgeni rasmi akiwa ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Afande Suleiman Kova. 

Bondia Francis Cheka akipima uzito

Bondia Kalama Nyilawila akipima uzito
Mpambano huo ulikuwa ni wa kuwania ubingwa wa mabara wa UBO mkanda ambao ulikuwa wazi ulizidi kumweka katika nafasi nzuri ya mchezo wa ngumi duniani Francis Cheka ambaye ni bingwa wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC na sasa UBO.
Bondia Karama Nyilawila  kulia akijitahidi kukwepa makonde ya Francis Cheka

Bondia Francis Cheka (kulia) akimsukumia konde Kalama Nyilawila


Katika raundi tano za kwanza Nyilawila alionyesha kumdhibiti kiasi Cheka kwa kumchezea 'kibabebabe' huku akitumia nguvu nyingi kujihami hali iliyopelekea baadhi ya mashabiki wa Nyilawila kushangilia kwa nguvu huku wa kuwa mwisho wa tambo za Cheka ulikuwa umewadia.
Hata hivyo raundi ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha wake Abdallah Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani wake ambapo mwamuzi wa pambano hilo, Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka, lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo.  
Baada ya kuonyesha ishara hiyo, mashabiki wa Cheka walilipuka kwa shangwe kkushangilia ushindi huo wa TKO. Itakumbukwa kuwa hii ni mara ya ili kwa Cheka kumpiga Nyilawila

Mgeni rasmi Kamanda Kova (kulia) akimnyanyua mkono Francis Cheka kuashiria ushindi
Klabu ya Michezo ya Biafra inampa pongezi nyingi Bondia Francis Cheka (mtoto wa nyumbani) kwa ushindi huo. 

(Picha na habari kwa hisani ya  Super D Boxing Blog na Shaffih Dauda Blog)

Friday, September 28, 2012

KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA YAJIPANGA KUWAKABIDHI RASMI BARUA ZA UTEUZI VIONGOZI WAKE JUMAPILI TAREHE 30 SEPTEMBA, 2012

Mwenyekiti mteule wa Klabu ya Michezo ya Biafra Bw. Abdul Mollel anawakaribisha wanachama, mashabiki pamoja na wadau wote kwa ujumla katika hafla ya kukabidhi barua za uteuzi kwa viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 16 Septemba, 2012. Hafla hiyo itafuatiwa na mazoezi ya pamoja ya mbio za polepole zitakazofanyika kuanzia majira ya saa 12:15 asubuhi makao makuu ya klabu 90 Degrees Pub Kinondoni na kuishia hapo hapo klabuni. 
Mwenyekiti mteule wa Biafra Abdul A. Mollel akitoa shukrani kwa wasimamizi wa uchaguzi, wanachama na wadau wote kwa kuweza kufanikisha uchaguzi huo.
Akielezea mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) siku hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Klabu Mr. Michael Silili alibainisha kwamba mazoezi yataanzia klabuni saa 12:15 asubuhi na kupitia barabara ya Kawawa na kuvuka Moroko kisha barabara ya migombani mpaka hospitali ya Mikocheni hadi viktoria na kukatisha baraba ya kuelekea mwananyamala kisha kupitia barabara ya kwakopa hadi kanisani na kumalizia klabuni kupitia barabara ya Isere.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Michael Silili (Kulia) akiwa na mjumbe wa kamati hiyo Nancy Rafael wakifuatilia jambo kwa makini.

Akimalizia, Katibu Mkuu Mteule Bw. Yahya Poli aliwakaribisha wadau wote hata wale ambao si wanachama kwa mazoezi ya pamoja na baadaue hafla hiyo ya kukabidhi rasmi barua za uteuzi kwa viongozi wa klabu. Kwa wale ambao wanapenda kushiriki basi wanaweza kuwasiliana na katibu huyo kwa namba ya 0715253653.

 WE! WE! MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!