Friday, September 28, 2012

KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA YAJIPANGA KUWAKABIDHI RASMI BARUA ZA UTEUZI VIONGOZI WAKE JUMAPILI TAREHE 30 SEPTEMBA, 2012

Mwenyekiti mteule wa Klabu ya Michezo ya Biafra Bw. Abdul Mollel anawakaribisha wanachama, mashabiki pamoja na wadau wote kwa ujumla katika hafla ya kukabidhi barua za uteuzi kwa viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 16 Septemba, 2012. Hafla hiyo itafuatiwa na mazoezi ya pamoja ya mbio za polepole zitakazofanyika kuanzia majira ya saa 12:15 asubuhi makao makuu ya klabu 90 Degrees Pub Kinondoni na kuishia hapo hapo klabuni. 
Mwenyekiti mteule wa Biafra Abdul A. Mollel akitoa shukrani kwa wasimamizi wa uchaguzi, wanachama na wadau wote kwa kuweza kufanikisha uchaguzi huo.
Akielezea mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) siku hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Klabu Mr. Michael Silili alibainisha kwamba mazoezi yataanzia klabuni saa 12:15 asubuhi na kupitia barabara ya Kawawa na kuvuka Moroko kisha barabara ya migombani mpaka hospitali ya Mikocheni hadi viktoria na kukatisha baraba ya kuelekea mwananyamala kisha kupitia barabara ya kwakopa hadi kanisani na kumalizia klabuni kupitia barabara ya Isere.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Michael Silili (Kulia) akiwa na mjumbe wa kamati hiyo Nancy Rafael wakifuatilia jambo kwa makini.

Akimalizia, Katibu Mkuu Mteule Bw. Yahya Poli aliwakaribisha wadau wote hata wale ambao si wanachama kwa mazoezi ya pamoja na baadaue hafla hiyo ya kukabidhi rasmi barua za uteuzi kwa viongozi wa klabu. Kwa wale ambao wanapenda kushiriki basi wanaweza kuwasiliana na katibu huyo kwa namba ya 0715253653.

 WE! WE! MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!

No comments:

Post a Comment