Monday, September 17, 2012

BIAFRA YAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI KWA MAFANIKIO

Jumapili ya tarehe 16 Septemba 2012 ilikuwa ni siku ya uchaguzi wa viongozi wa klabu. Uchaguzi huo ulifanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa michezo wilaya ya Kinondoni. Kufanikiwa kwa uchaguzi huo ambao ulifanyika katika makao makuu ya klabu, 90 Degrees Pub Kinondoni kulitokana na hamasa ya wanachama kujitolea katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama zilivyobainishwa katika katiba ya klabu. 
BAADHI YA WANABIAFRA WAKIWA KLABUNI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU SEPTEMBA 16, 2012          

Wagombea wa nafasi mbalimbali wakisubiri kuanza kwa zoezi la uchaguzi kutoka kushoto ni Ibrahim Kilasa, Freddy Mwesigwa (wagombea nafasi ya Kamati ya Uchumi na Mipango), na Abdul Mollel (mgombea nafasi ya Mwenyekiti)



Bi. Jacqueline Barozi (mgombea nafasi ya Makamu M/Kiti) akiwa na Mustafa Muro (mgombea Kamati ya Nidhamu na Rufaa




Nancy Raphael (mgombea kamati ya Ufundi) katikati akiwa na wagombea wenza Mossi Saidi (kushoto) na Boniface Banga (kulia)
 UCHAGUZI huo pia ulihudhuriwa na klabu rafiki za Namanga na Kunduchi kwanza ambapo wanachama toka klabu hizo walijumuika kwa pamoja na Wanabiafra katika kuhakikisha zoezi hilo la uchaguzi linafanikiwa. Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Asia Mohamed, Wanakunduchi Kwanza waliwasili katika makao maku ya klabu ya Biafra majira ya saa nne asubuhi na muda mfupi baadae wanachama wa Namanga Sports Club nao waliwasili eneo hilo.
Mwenyekiti wa Kunchi Kwanza Jogging (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na baadhi ya Wanakunduchi Kwanza


John Gako kutoka Namanga akiomba utaratibu toka kwa 'floor manager' wa shughuli Bi. Magreth Warisanga (aliyesimama)
VIONGOZI kutoka idara ya Michezo Manispaa ya Kinondoni waliwasili ukumbini hapo majira ya saa sita mchana na mara baada ya kupokelewa na kutoa salam zao za uchaguzi, moja kwa moja walitoa mwongozo wa namna zoezi zima la uchaguzi litakavyofanyika baada ya kuridhika na maandalizi ya uchaguzi wenyewe. 
Mr. Mrimi kutoka idara ya Michezo Manispaa ya Kinondoni (Katikati) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Balozi Msolomi, Isere, Mwinyimadi Tambaza (kushoto) msimamizi wa soka kwa watoto wadogo KIDYOSA

Wasimamizi wa uchaguzi wakifuatalia kwa makini maelezo ya mgombea (haonekani pichani)
MARA baada ya kukamilika kwa zoezi la kujieleza, wanachama walianza moja kwa moja zoezi la upigaji kura ambapo baada ya kukamilika kwa zoezi hilo wagombea wa nafasi za juu za klabu walipendekeza mawakala wao katika zoezi la kuhesabu kura.
Mawakala wa wagombea pamoja na wasimamizi wa uchaguzi wakiwa katika zoezi la kuhesabu kura

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea

zoezi la kuhesabu kura likiendelea

Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu wake pamoja na wagombea wengine wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi

Wagombea wa nafasi ya Kamati ya Ufundi wakisikiliza matokeo ya uchaguzi kwa hamu
ZOEZI la kuhesabu kura ambalo lilidumu kwa takriban masaa mawili lilikamilika na hatimaye msimamizi mkuu wa uchaguzi pamoja na jopo lake walirejea katika ukumbi wa mkutano na moja kwa moja kuanza kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa kuanzia na wateule wa kamati za Ufundi, Uchumi na Mipango, Nidhamu na Rufaa na kisha Kamati ya utendaji, Mweka Hazina, Katibu Msaidizi, Katibu Mkuu, Makamau Mwenyekiti pamoja na Mwenyekiti. 
WASHINDI - KAMATI YA UCHUMI NA MIPANGO

AKIPONGEZWA KWA USHINDI WA NAFASI YA MWENYEKITI NDUGU ABDUL MOLLEL (KATIKATI)

WASHINDI WA NAFASI MBALIMBALI WAKIONGOZWA NA VIONGOZI WAKUU

MWENYEKITI MTEULE WA BIAFRA SPORTS CLUB, ABDUL MOLLEL AKITOA SHUKRANI KWA NIABA YA VIONGOZI WATEULE KWA WANACHAMA, WADAU NA MASHABIKI KWA KUFANIKISHA ZOEZI LA UCHAGUZI

MAKAMU MWENYEKITI MTEULE AKITETA JAMBO NA KATIBU MKUU MTEULE

MWINYIMADI TAMBAZA AKSISITIZA UMUHIMU WA KUIENZI TIMU YA WATOTO WA BIFRA KIDS

SHUGHULI ya uchaguzi ilikamilika majira ya saa moja jioni ambapo washindi pamoja na wanachama na wadau wengine wote walijumuika kwa burudani mbalimbali zilizotolewa ili kukamilisha siku hiyo maalum.

TUNAWAPONGEZA SANA VIONGOZI WOTE WALIOSHINDA PAMOJA NA WANACHAMA WOTE WA BIAFRA SPORTS CLUB, USHINDI WENU UWE CHACHU YA KULETA MAENDELEO YA KLABU NA MICHEZO KWA UJUMLA!

 
 

No comments:

Post a Comment