Heri ya mwaka mpya wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wote wa Biafra. Januari ndio hivyo imekwisha nasi klabuni tumeanza kutekeleza mpango kazi wa mwaka 2013. Kwa mwaka huu klabu imepanga kufanya matukio makubwa manne.
Viongozi wa juu wa klabu wakiwa katika kikao cha kujadili Mpango Kazi wa mwaka 2013 |
Kutembelea na kutoa misaada ya kibinadamu katika vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu Manispaa ya Kinondoni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambapo vituo vilivyopendekezwa vitatembelewa kuanzia tarehe 2, 9 na 16 Juni ambayo ndio kilele cha siku ya mtoto wa Afrika.
Binti kutoka kituo cha Hanasif akiwa na zawadi mwaka 2011 |
Mwezi Juni na Julai pia klabu itaendesha mashindano ya Soka kwa timu za vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakayojulikana kama Biafra Cup U17. Kombe hilo linatarajiwa kufanyika kila mwaka na litatumika katika kukuza vipaji vya mchezo wa soka kwa vijana na pia klabu itatumia kombe hilo katika kusaka wachezaji nyota na kuwasajili kwenye timu. Katika kuhakikisha wanafanya vyema kwenye michuano hiyo, timu ya soka ya vijana (U17) ya Biafra ipo katika mazoezi ya kina chini ya kiongozi wao William Masika.
Kikosi cha #BYFTU17 wakiwa wamevaa jezi mpya zilizonunuliwa kwa ufadhili mchezaji mwenzao aliyehamia Norway - Hamada aka Elnino |
Matukio Mengine ni Biafra Day iliyopangwa kufanyika tarehe 7 Julai, 2013, kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani tarehe 1 Disemba, 2013 pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani na wa michezo kwa kutembelea katika mbuga ya wanayama ya mikumi pamoja na kufanya mazoezi ya mbio za pole pole na wakaazi wa vitongoji vya Mikumi mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi Disemba.
Karibu sana mdau katika kufanikisha mpango kazi huu.
Michezo ni Afya, Michezo ni Furaha!!!!
KWA MASWALI/MAONI/USHAURI WASILIANA NA: -
KATIBU MKUU,
BIAFRA SPORTS CLUB
+255 715 253 653
biafra.jsclub@gmail.com
www.facebook.com/biafrasportsclub
ISELE STREET, BALOZI MSOLOMI,
KINONDONI
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment