Wednesday, October 24, 2012

PONGEZI KWA MWANABIAFRA ROSE MWAKIBUGI KWA BIRTHDAY ILIYOPENDEZA

Wanabiafra pamoja na marafiki mbalimbali walijumuika pamoja katika sherehe ya kustukiza "suprise" ya kuzaliwa kwa mwnabiafra mwenzao Mrs. Rose Mwakibugi ambayo iliandaliwa na mwanabiafra mwingine ambaye pia ni mume wa bi Rose, kaka Robert Mwakibugi.
Keki ya Birthday
Katika kufungua sherehe hiyo Robert Mwakibugi alitumia fursa kwa kumpongeza mke wake kwa kutimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake na pia kwa upendo alionao kwake yeye mwenyewe pamoja na familia yao kwa ujumla. 
Mr.s Rose Mwakibugi - birthday girl akiwa ofisini kwake Chimbinga Unique Pub akishangaa yanayojiri                  
Wanabiafra kutoka kushoto Robert Mwakibugi, Yahya Poli, Rose Mwakibugi, na Jaqueline Barozi

Robert Mwakibugi akimlisha mkewe Rose Mwakibugi keki ya upendo

Bw. na Bi. Mwakibugi wakimlisha keki mtoto wa Habil ambaye pia ni mwanachama wa Biafra



Kwa upendeleo maalum, kwa niaba ya wanabiafra Makamu M/Kiti Bi. Jacqueline Barozi allilishwa keki na Rose mwakibugi akisaidiana na M/Kiti Abdul Mollel

Birthday girl akipongezwa
 
Mwamabiafra Henry Maseko akitoa mkono wa pongezi

Wanabiafra Henry Maseko kushoto na King A.Y. Mpore 
KWA NIABA YA WANACHAMA WOTE KLABU INATOA PONGEZI KWA BI ROSE MWAKIBUGI KWA SHEREHE YAKE YA BIRTHDAY, TUNAMTAKIA MAISHA MAREFU YENYE FURAHA, AMANI NA MAFANIKIO. KATIBU MKUU, BIAFRA SPORTS CLUB

Monday, October 22, 2012

MAZOEZI YA MBIO ZA POLE POLE JANA JUMAPILI YAWAKUTANISHA TENA WANABIAFRA

Kama ilivyo ada, Wanabiafra kila jumapili hujikusanya na kufanya mazoezi ya mbip za pole pole (jogging) kuzunguka maeneo mbalimbali ya Kinondoni. Mazoezi ya jana yaliwakutanisha zaidi ya wanachama 30 wa Biafra ambao wakubwa kwa wadogo. 
Mwenyekiti wa Kamatu ya Uchumi Ibrahim kilasa (mwenye miwani) akikimbia pamoja na watoto

Hujachelewa kujiunga na klabu yetu, karibu sana!

Monday, October 15, 2012

BIRTHDAY YA KAWE JOGGING YAFANA

Klabu ya mchezo wa mbio za pole pole ya Kawe jana tarehe 14 Oktoba, 2012 ilitimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Anjela Kairuki (Mb.). 
WanaKawe Jogging

Wanamichezo kutoka vilabu mbalimbali walishiriki katika hafla hiyo ambayo ilianza kwa mazoezi ya mbio za pole pole yaliyoanzia na kuishia katika vwanja vya Tanganyika Packers na hatimaye michezo mingine ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku na soka la vijana ambapo Biafra Youth Football Team ilitoka sare ya bila kufungana na timu ya vijana ya Kawe.

Mara baada ya michezo kumalizika wanamichezo wote walijumuika pamoja katika ukumbi wa Massae Pub ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Kawe jogging kwa shguli nyinginezo zilizoenda sambamba na hafla hiyo.
 


Thursday, October 11, 2012

BIAFRA JOGGING YAALIKWA KUSHIRIKI SHEREHE KUTIMIZA MWAKA MMOJA TANGU KUANZISHWA KWA KAWE JOGGING



Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa klabu ya Kawe Jogging, wanachama wa klabu hiyo wamealika klabu mbalimbali zinazojihusisha na uhamasisjaji wa mchezo wa mbio za pole pole mkoa wa Dar es Salaam katika kusherehekea maadhimisho hayo. Biafra Jogging, Mzimuni Jogging, Kunduchi Kwanza Jogging na klabu ni nyinginezo kwa pamoja zitafanya mazoezi ya mbio za pole pole na kisha kushiriki katika michezo mingine kama vile kuvuta kamba na  mpira wa miguu kwa wanawake na wanaume.

Wana-Kawe Jogging wakiwa katika Magofu ya Kaole mwanzoni mwaka 2012


Biafra Jogging wakiwa pamoja na Namanga Jogging mazoezini
Klabu ya michezo ya Biafra inatoa pongezi za dhati kwa Kawe Jogging na wanachama wake wote katika sherehe hizo za kutimiza mwaka mmoja. 

WE! WE! MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA

Monday, October 01, 2012

FRANCIS CHEKA AMTWANGA TENA KARAMA NYILAWILA

Jumamosi iliyopita tarehe 29 Oktoba, 2012 mtoto wa Kinondoni Msisiri ambaye kwa sasa anauwakilisha vyema mkoa wa Morogoro Francis Cheka alizidi kuonesha ubabe kwa mabondia wenzake hasa wa Tanzania baada ya kumtandika kwa TKO katika raundi ya sita mwanamasumbwi mwenye makeke na maneno mengi Kalama Nyilawila. Mpambano huo uliopigwa katika ukumbi wa PTA Sabasaba ulishuhudiwa na mamia ya mashabiki wa mchezo wa ngumi huku mgeni rasmi akiwa ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Afande Suleiman Kova. 

Bondia Francis Cheka akipima uzito

Bondia Kalama Nyilawila akipima uzito
Mpambano huo ulikuwa ni wa kuwania ubingwa wa mabara wa UBO mkanda ambao ulikuwa wazi ulizidi kumweka katika nafasi nzuri ya mchezo wa ngumi duniani Francis Cheka ambaye ni bingwa wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC na sasa UBO.
Bondia Karama Nyilawila  kulia akijitahidi kukwepa makonde ya Francis Cheka

Bondia Francis Cheka (kulia) akimsukumia konde Kalama Nyilawila


Katika raundi tano za kwanza Nyilawila alionyesha kumdhibiti kiasi Cheka kwa kumchezea 'kibabebabe' huku akitumia nguvu nyingi kujihami hali iliyopelekea baadhi ya mashabiki wa Nyilawila kushangilia kwa nguvu huku wa kuwa mwisho wa tambo za Cheka ulikuwa umewadia.
Hata hivyo raundi ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha wake Abdallah Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani wake ambapo mwamuzi wa pambano hilo, Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka, lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo.  
Baada ya kuonyesha ishara hiyo, mashabiki wa Cheka walilipuka kwa shangwe kkushangilia ushindi huo wa TKO. Itakumbukwa kuwa hii ni mara ya ili kwa Cheka kumpiga Nyilawila

Mgeni rasmi Kamanda Kova (kulia) akimnyanyua mkono Francis Cheka kuashiria ushindi
Klabu ya Michezo ya Biafra inampa pongezi nyingi Bondia Francis Cheka (mtoto wa nyumbani) kwa ushindi huo. 

(Picha na habari kwa hisani ya  Super D Boxing Blog na Shaffih Dauda Blog)