Thursday, February 28, 2013

JOGGING YAVIKUTANISHA TENA VILABU KUNDUCHI JUMAPILI TAREHE 3 MACHI, 2013

Katika kuhamasisha mchezo wa mbio za pole pole (jogging) maeneo ya Kunduchi na kuimarisha uhusuiano wa vilabu vya jogging, Jumapili ya tarehe 3 Machi, 2013 wanamichezo kutoka katika vilabu vya Namanga, Kawe, Biafra na Kunduchi Kwanza pamoja na wadau wengine wa michezo watajumuika na kufanya mazoezi ya pamoja ya jogging ambayo yataratibiwa na klabu ya Kunduchi Kwanza ambao ndio wenyeji na waratibu wa mazoezi hayo. 
Jogging
 

Jogging ikiendelea

Baada ya mazoezi hayo, wanamichezo wote waliohudhuria watajumuika pamoja makao makuu ya klabuya Kunduchi yaliyopo Malanja Pub ambapo kutafanyika na kikao cha pamoja cha viongozi vilabu shiriki juu ya mustakbali wa mchezo wa mbio za pole pole wilaya ya Kinondoni ikifuatiwa na burudani mbalimbali.

Wadau wote mnakaribishwa!


Monday, February 25, 2013

VIONGOZI WA VILABU VYA JOGGING KINONDONI WAKUTANA NA MSAJILI WA VYAMA NA VILABU VYA MICHEZO WILAYA YA KINONDONI

Jioni ya tarehe 25 Februari, 2013, viongozi kutoka katika vilabu vya michezo vinavyojihusisha na mchezo wa mbio za pole pole walikutana na Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo wilaya ya Kinondoni ndugu Jumanne Mrimi (pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
Ndugu Jumanne Mrimi - Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo wilaya ya Kinondoni
 Viongozi waliomtembelea ni kutoka katika vilabu vya Namanga (David Mwaka na Andrew Mangole), Kawe (Mohammed Risasi, Alhaj Seif Mukhere na Khadija Mabrouk) Biafra ( Abdul Mollel na Yahya Poli) na Kunduchi Kwanza (Alphonsina Joseph).

David Mwaka (mwenye shati jekundu) - Mwenyekiti Namanga Sports Club


Alhaj Seif Mukhere  - Kaimu Katibu Mkuu Kawe Sports & Social Club

Mohammed Risasi - Mwenyekiti Kawe Sports & Social Club

Andrew Mangole - Katibu Mkuu Namanga Sports Club na Bi. Khadija Mabrouk - Makamu Mwenyekiti Kawe Sports and Social Club
Lengo la kumtembelea msajili ofisini kwake lilikuwa ni katika harakati za kufufua uhai na hamasa ya mchezo wa mbio za pole pole katika manispaa ya Kinondoni ambapo viongozi wa klabu hizo wamedhamiria kuhuisha Chama cha Mchezo wa Jogging wilaya ya Kinondoni kilichoasisiwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni wakati huo Kanali Fabian Massawe na kisha baadaye kuunda shirikisho la mchezo huo.

Yahya Poli - Katibu Mkuu Biafra Sports Club na Alphonsina Joseph - Katibu Mkuu Kunduchi Kwanza Jogging and Sports Club

Maazimio ya kikao hicho yalikuwa ni pamoja na kuwasiliana na vilabu vyote vinavyojihusisha na jogging wilaya ya Kinondoni na kuunda umoja na uongozi wa chama cha jogging.
Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni (mwenye shati jeusi) akisalimiana na viongozi
Mwishoni kabisa katika majumuisho yake, msajili aliahidi kushirikiana na uongozi utakaoundwa na kutoa mwongozo wa namna ya kuunda chama hicho wakati wowote atakapohitajika kufanya hivyo, vile vile aliwaasa viongozi waliomtembelea kusambaza taarifa kwa vilabu vingine ili navyo viweze kushiriki kikamilifu.
Baadhi ya viongozi wa vilabu vya jogging katika picha ya pamoja - kutoka kushoto Jumanne Mrimi (Msajili), Abdul Mollel, David Mwaka, Mohamed Risasi, Andrew Mangole, Khadija Mabrouk, Alhaj Seif Mukhere
 

Wednesday, February 20, 2013

BIAFRA SPORTS CLUB YAPATA USAJILI RASMI

Leo tarehe 20 Februari, 2013 klabu ya michezo ya Biafra imepata usajili rasmi toka Baraza la Michezo Tanzania (BMT). Usajili huo umetokana na kutimiza masharti na kanuni zote ziliyowekwa na baraza hilo katika usajili wa vilabu vya michezo nchini Tanzania. 
Cheti cha Usajili wa Biafra Sports Club
Akizungumza wakati akikabidhi cheti hicho kwa Katibu Mkuu wa Biafra ndugu Yahya Poli, Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo Tanzania Mama Rwezaula aliwapongeza wanachama wote kwa kuanzisha klabu hiyo na pia aliwasihi viongozi na wanachama kuhakikisha wanasimamia na kuilinda katiba ya klabu hiyo na kujiepusha na migogoro ili kuendeleza michezo nchini.
Barua ya Usajili wa Biafra Sports Club

 Mwenyekiti wa klabu hiyo ndugu Abdul Mollel akizungumza tokea safarini Songea, aliwapongeza wanachama wote kwa kujitolea kwao katika kuiendeleza klabu na uvumilivu pale palipotokea na vikwazo vya hapa na pale. 

HONGERA WANABIAFRA WOTE - SASA TUJENGE KLABU YETU KWA KUINUA NA KUHAMASISHA MICHEZO, UPENDO, UMOJA NA USHIRIKIANO!!!!

Monday, February 11, 2013

MATUKIO YA WANABIAFRA KATIKA WIKINDI ILIYOPITA

Wanamichezo takriban wote wana msemo wao kuwa "michezo ni afya, michezo ni furaha, michezo huwaunganisha watu". Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa juma lililopita kwa Wanabiafra. Siku ya ijumaa tarehe 8 Februari, 2013 ambapo Wanabiafra pamoja na marafiki kadhaa walikutana na kuianza wikiendi kwa burudani ya muziki, vinywaji na nyama choma pale Chiminga Unique Pub. 
Ally Masharubu na Ayub Layson wakitafuna nyama ya mbuzi

Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel alisimama kuwasalimia wanabiafra na marafiki

Kutoka kushoto; Ally Masharubu, Ayub Layson na Editha Tungaraza

Mwanabiafra Dustan Barozi (kulia) pamoja na marafiki zake

Editha Tungaraza akifaidi msosi

Makamu Mwenyekiti wa Biafra Jacqueline Barozi (aliyesimama) akichukua oda ya vinywaji


Rose Mwakibugi Almaarufu mama Chimbinga alihakikisha vinywaji vipo na vya kutosha

Robert Mwakibugi akiiwakilisha vyema Chimbinga Unique Pub
Kama unapenda kushiriki kwenye mijumuiko ya aina hii, usisite, wasiliana na Katibu Mkuu, Biafra Sports Club kwa barua pepe; biafra.jsclub@gmail.com

Friday, February 01, 2013

WANABIAFRA KUTEMBELEA VITUO VYA WATOTO YATIMA MWAKA 2013

Heri ya mwaka mpya wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wote wa Biafra. Januari ndio hivyo imekwisha nasi klabuni tumeanza kutekeleza mpango kazi wa mwaka 2013. Kwa mwaka huu klabu imepanga kufanya matukio makubwa manne

Viongozi wa juu wa klabu wakiwa katika kikao cha kujadili Mpango Kazi wa mwaka 2013

Kutembelea na kutoa misaada ya kibinadamu katika vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu Manispaa ya Kinondoni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambapo vituo vilivyopendekezwa vitatembelewa kuanzia tarehe 2, 9 na 16 Juni ambayo ndio kilele cha siku ya mtoto wa Afrika.
Binti kutoka kituo cha Hanasif akiwa na zawadi mwaka 2011
 Mwezi Juni na Julai pia klabu itaendesha mashindano ya Soka kwa timu za vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakayojulikana kama Biafra Cup U17. Kombe hilo linatarajiwa kufanyika kila mwaka na litatumika katika kukuza vipaji vya mchezo wa soka kwa vijana na pia klabu itatumia kombe hilo katika kusaka wachezaji nyota na kuwasajili kwenye timu. Katika kuhakikisha wanafanya vyema kwenye michuano hiyo, timu ya soka ya vijana (U17) ya Biafra ipo katika mazoezi ya kina chini ya kiongozi wao William Masika
Kikosi cha #BYFTU17 wakiwa wamevaa jezi mpya zilizonunuliwa kwa ufadhili mchezaji mwenzao aliyehamia Norway - Hamada aka Elnino

Matukio Mengine ni Biafra Day iliyopangwa kufanyika tarehe 7 Julai, 2013, kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani tarehe 1 Disemba, 2013 pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani na wa michezo kwa kutembelea katika mbuga ya wanayama ya mikumi pamoja na kufanya mazoezi ya mbio za pole pole na wakaazi wa vitongoji vya Mikumi mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi Disemba.

Karibu sana mdau katika kufanikisha mpango kazi huu. 

Michezo ni Afya, Michezo ni Furaha!!!! 

KWA MASWALI/MAONI/USHAURI WASILIANA NA: - 
KATIBU MKUU,
BIAFRA SPORTS CLUB
+255 715 253 653 
biafra.jsclub@gmail.com
www.facebook.com/biafrasportsclub
ISELE STREET, BALOZI MSOLOMI,
KINONDONI 
DAR ES SALAAM.