Monday, December 08, 2014

KILELE CHA UHURU MARATHON 2014 CHATOQ CHANGAMOTO KWA WANABIAFRA KUJIANDAA VYEMA

Tarehe 7 Disemba, 2014 Tanzania ilishuhudia wanariadha toka mataifa mbalimbali duniani wakishiriki katika mashindano ya riadha yajulikanayo kama Uhuru Marathon ambayo ambayo kilele chake kilifanyika katika viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam. Fabian Joseph aliibuka kinara wa mashindano hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa waziri wa michezo mheshimiwa Dr. Fenella Mukangara. 
Waziri wa Michezo, Habari na Utamaduni Dr. Fenella Mukangara (picha kwa hisani ya Issa Michuzi)
Zaidi ya kushiriki kama timu katika mashindano hayo, klabu ya michezo ya Biafra ilishiriki katika maandalizi ya mbio hizo kwa kushirikiana kwa karibu na wandaaji katika kupata washiriki toka katika vilabu vya jogging nchini Tanzania ambapo vilabu kadhaa vya jogging vilijitokeza. 
Wanabiafra katika picha ya pamoja na wanajogging


Klabu ya michezo ya Biafra ilitoa washiriki zaidi ya 10 katika mashindano hayo kwa ngazi mbalimbali kama vile 3, 5 na 21km. Ambapo baadhi yao Juma Ramadhani, Aziza Mwaimu, Zein Ahmed, Noha Machaka na Boniface Mangasala walishiriki katika mbio za 21km. 
Wanabiafra waliokimbia 21km katika picha ya pamoja huku wakionesha vyeti vyao kutoka kushoto Zein Ahmed, Aziza Mwaimu, Noha Machaka na Juma Ramadhani



Noha Machaka alishindana 21km akionesha cheti chake cha ushiriki.


Zeinin Ahmed (aliyelala) akichuliwa msuli

Wanabiafra katika picha ya pamoja baada ya mashindano wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao Ms. Jaqueline Barozi (watatu toka kushoto)

Asha Yusuph na Zein Ahmed wakionesha cheti cha ushiriki cha Zein

Wanabiafra Emima George Madumba na Zein Ahmed 

Mwanabiafra Aziza Mwaimu akimaliza mbio
Katika kilele hicho pamoja na washiriki toka katika klabu ya michezo ya Biafra kutoa ushindani kwa wanariadha wengine kulikuwa na changamoto mbalimbali zilizojitokeza kama vile kutopima afya kabla ya mashindano na kukosa uzoefu wa mashindano hayo.

Baada ya kujifunza changamoto hizo Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Michezo ya Biafra imeweka mkakati mahususi wa kuwawezesha wanachama wake kushiriki kikamilifu katika mashindano yajayo.

Akiongea na blogu hii baada ya mashindano hayo, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Biafra ndugu Abdul Mollel aliwashukuru waandaaji kwa kuwawezesha wanajogging kushiriki mbio hizo na vile vile kwa klabu yake kupata nafasi ya kuratibu ushiriki wa vilabu hivyo katika mashindano hayo.
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Biafra Henry Maseko (kushoto) na Ayoub Layson

Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Biafra (mwenye kofia) akiwapanga vijana wake




Wednesday, December 03, 2014

BIAFRA YASHIRIKI KATIKA SHEREHE ZA KUKABIDHI VYETI GYA USAJILI KWA VILABU VYA JOGGING TEMEKE TARE 30 NOVEMBA, 2014

Katika kuhakikisha tasnia ya mchezo wa mbio za pole pole inakuwa rasmi na kutambulika, Chama cha Mchezo wa Mbio za Pole wilaya ya Temeke (TEJA) kiliandaa hafla fupi ya kukabidhi rasmi vyeti vya usajili kwa vilabu 8 vinavyojihusisha na mchezo wa mbio za polepole wilayani Temeke.

Baadhi ya wanajogging katika sherehe hizo

Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Biafra ndugu Abdul Mollel akiwasalimia wanamichezo
 
Makamu Mwenyekiti wa TEJA ndugu Jimmy Mkande
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mheshimiwa Abdullah Ally Hassan Mwinyi ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki akiiwakilisha Tanzania.
Mgeni rasmi katika ubora wake sambamba na wanamichezo
Mgeni rasmi alipata wasaa wa kusikiliza risala iliyosomwa kwake na waandaaji wa sherehe hizo kabla ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa vyeti ambapo katika majibu yake aliwashauri waandaaji kuandaa sherehe nyingine ambapo yale ambayo yameombwa na vikundi kupitia risala yao yatatolewa taarifa ya utekelezaji.
Risala ikisomwa kwa mgeni rasmi



Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la ugawaji vyeti burudani mbalimbali ziliendelea katika kuisherehesha siku yenyewe. 
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanachama wa vilabu vya jogging 

Jimmy Mkande akiwa pamoja na baadhi ya wanabiafra

Baadhi ya Wanabiafra katika picha ya pamoja

Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Michezo ya Michezo ya Biafra, tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana viongozi wa Chama cha Jogging aTemeke (TEJA) kwa jitahada zao za kuuimarisha na kuurasimisha mchezo wa mbio za polepole Tanzania. 

WANABIAFRA WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA KUHAMASISHA MICHEZO KWA VIJANA NA WATOTO

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) chini ya udhamini wa taasisi ya UK Sports - Internationa Inspiration iliandaa mafunzo uhamasishaji wa michezo kwa vijana na watoto. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika uwanja wa taifa yaliwakutanisha pamoja makatibu tawala pamoja na maafisa michezo toka katika wilaya zote nchini. Mafunzo hayo pia yalifanyika ikiwa ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wa baraza la Michezo Tanzania uliofanyika katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Mkinga, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Makatibu Wakuu na Wenyeviti wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. (picha kwa hisani ya Hivi Sasa Blog).
Baada ya mafunzo hayo, sherehe  rasmi ya uzinduzi wa kampeni ya Inspire Tanzania ilifanyika tarehe 20 September, 2014 katika uwanja wa taifa. Sherehe hiyo ilitanguliwa na mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambayo yaliratibiwa na klabu ya michezo ya Biafra pamoja na vilabu vingine vya jogging katika mkoa wa Dar es Salaam ambavyo Temeke Jogging, Faita, Jogging, Kopa Jogging, n.k.