Katika kuhakikisha tasnia ya mchezo wa mbio za pole pole inakuwa rasmi na kutambulika, Chama cha Mchezo wa Mbio za Pole wilaya ya Temeke (TEJA) kiliandaa hafla fupi ya kukabidhi rasmi vyeti vya usajili kwa vilabu 8 vinavyojihusisha na mchezo wa mbio za polepole wilayani Temeke.
|
Baadhi ya wanajogging katika sherehe hizo |
|
Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Biafra ndugu Abdul Mollel akiwasalimia wanamichezo |
|
Makamu Mwenyekiti wa TEJA ndugu Jimmy Mkande |
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mheshimiwa Abdullah Ally Hassan Mwinyi ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki akiiwakilisha Tanzania.
|
Mgeni rasmi katika ubora wake sambamba na wanamichezo |
Mgeni rasmi alipata wasaa wa kusikiliza risala iliyosomwa kwake na waandaaji wa sherehe hizo kabla ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa vyeti ambapo katika majibu yake aliwashauri waandaaji kuandaa sherehe nyingine ambapo yale ambayo yameombwa na vikundi kupitia risala yao yatatolewa taarifa ya utekelezaji.
|
Risala ikisomwa kwa mgeni rasmi
|
Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la ugawaji vyeti burudani mbalimbali ziliendelea katika kuisherehesha siku yenyewe.
|
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanachama wa vilabu vya jogging |
|
Jimmy Mkande akiwa pamoja na baadhi ya wanabiafra |
|
Baadhi ya Wanabiafra katika picha ya pamoja
Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Michezo ya Michezo ya Biafra, tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana viongozi wa Chama cha Jogging aTemeke (TEJA) kwa jitahada zao za kuuimarisha na kuurasimisha mchezo wa mbio za polepole Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment