Tuesday, July 24, 2012

WANACHAMA WATOTO WA BIAFRA WANG'ARA NDANI YA UZI MPYA

Katika hatua za kwapendezesha wanachama wa Biafra wenye umri mdogo, uongozi wa klabu, kwa kushirikiana na wanachama wake wote umegawa sare za mazoezi kwa wanachama wake wenye umri mdogo ambao hushiriki mazoezi ya kila Jumapili. 
Watoto wa Biafra ndani ya sare mpya

Shukrani zimwendee mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu mheshimiwa Henry Maseko kwa kuweza kufanikisha upatikanaji wa sare hizo.

Thursday, July 19, 2012

BIAFRA SPORTS CLUB YAWATAKIA WAISLAM WOTE HERI YA MFUNGO WA RAMADHANI

Kwa niaba ya wanachama, wadau na mashabiki wa Biafra, mwenyekiti wa klabu hiyo ndugu Abdul Ahmad Mollel amewatakia waisalamu nchini na duniani kwa ujumla heri ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao unatarajiwa kuanza Ijumaa tarehe 20 Julai, 2012. Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa watu wote wanaoshiriki mfungo wa Ramadhan na wasioshiriki pia kutumia kipindi hiki katika kutenda yale yote mema ambayo yatupasa kutenda ikiwemo kufanya ibada, kutoa sadaka, kuwajali wasio na uwezo hasa yatima na wajane.
Baadhi ya watoto kutoka katika kituo cha Hananasif

Kwa wanabiafra, mwenyekiti aliwakumbusha kuwa wakati wa Ramadhan wanachama wataendelea na mazoezi kwa wale wenye kupenda kwa kuwa kufanya mazoezi ni jambo muhimu katika kujenga afya za watu. Hivyo basi, alitoa rai kwa wanachama wote ambao wangependa kufanya mazoezi wanakaribishwa.
Baadhi ya wachezaji wa Biafra Kids wakijipatia mlo wa Idd pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu 2011


Tuesday, July 17, 2012

KATIBU WA KAMATI YA UFUNDI YA BIAFRA AFUNGA NDOA!!!

Siku jumamosi tarehe 14 Julai, 2012 ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa mwanabiafra Ally Juma ambaye ni katibu wa Kamati ya Ufundi ya klabu hiyo baada ya kufunga ndoa na Bi Zahra Iddi. Ndoa hiyo ilifungwa nyumbani kwa familia ya bi harusi Tegeta Msikitini na sherehe iliyofana kufanyika katika ukumbi wa 90 Degrees Pub ambako ni makao makuu ya klabu ya michezo ya Biafra.

Bwana na Bi harusi baada ya kuingia ukumbini wakiwa pamoja na wapambe wao

Baadhi ya wanabiafra wakiongozwa na makamu mwenyekiti Jackline Barozi (mwenye gauni jeusi)

Katibu wa Biafra Kaka Poli akiwakaribisha wageni ukumbini pembeni ni MC wa sherehe hiyo

Bwana harusi ambaye ni katibu wa kamati ya ufundi ya klabu akimtambulisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo ndugu Michael Silili 

Maharusi wakilishana keki 


Mwenyekiti wa Biafra Abdul A. Mollel akila keki kwa niaba ya klabu 

Wanabiafra wakijadiliana
Wanabiafra waliohudhuria sherehe hiyo wakiongozwa na Katibu Kaka Poli

Baadhi ya wageni waalikwa

Kwa niaba ya wanachama, viongozi, mashabiki na wadau wote, klabu inatoa pongezi za dhati kwa maharusi na kuwaoombea mwenyezimungu aibariki ndoa yao.



Thursday, July 12, 2012

BIAFRA DAY 2012 YASOGEZWA HADI SEPTEMBA KUPISHA ZOEZI LA SENSA YA WATU

Katibu Mkuu wa klabu ya michezo ya Biafra ndugu Yahya Poli ameutangazia umma kwamba BIAFRA DAY 2012 ambayo awali ilipangwa kufanyika tarehe 26 Agosti, 2012 sasa imesogezwa mbele hadi tarehe 2 Septemba, 2012. Kusogezwa huko mbele kwa juma moja kumetokana na siku ya awali tarehe 26 Agosti, 2012 itakuwa ni siku maalum ya Sensa ya watu na makazi nchini Tanzania.
Wanabiafra wakikatiza eneo la daraja la salender wakiwa kwenye mazoezi ya mbio za polepole


Akielezea zaidi, ndugu Poli alitanabaisha kwamba mipango ya kufanikisha BIAFRA DAY 2012 bado inaendelea na kuwakaribisha wadau wote ambao wangependa kushiriki siku hiyo kwa ufadhili na udhamini wasisite kuwasiliana na viongozi wa klabu kwa kuwa fursa bado ipo. Pia alitoa msisitizo kwa kamati zote za klabu kukutana kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya BIAFRA DAY, 2012. 
BIAFRA DAY 2011 - Wanabiafra wakishindana kuvuta kamba



  

Thursday, July 05, 2012

BIAFRA DAY 2012 YAPANGWA KUFANYIKA MWEZI WA NANE

Kama ilivyo ada, kila mwaka tangu kuanzishwa kwake, klabu ya michezo ya Biafra hutenga siku maalum ambayo hujulikana kama BIAFRA DAY kwa ajili ya kujumuika pamoja na wadau wake wote kwa ajili ya michezo na shughuli nyingine mbalimbali. Mwaka huu 2012,  BIAFRA DAY imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam.
Wanabiafra katika picha ya pamoja ndani ya DarLive Mbagala

BIAFRA DAY 2012 itaanza rasmi saa kumi na mbili asubuhi na kumalizika saa moja usiku ambapo wanamichezo na wadau wengine wote watajumuika pamoja kwa mbio za pole pole jogging ambaazo zitaanzia katika viwanja vya Biafra na kuzunguka maeneo mbalimbali ya Kinondoni na hatimaye kumalizikia katika viwanja vya biafra. Akizungumzia matukio yatayofanyika siku hiyo, Katibu wa klabu ya Biafra alitanabaisha kwamba, mwaka huu Biafra Day inatarajiwa kuwa tofauti kwa kuongeza masuala mbalimbali kama vile huduma za upimaji wa virusi vya UKIMWI, kisukari, kansa, n.k. Michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, kukimbia na guni, kurusha mshale nayo pia itachezwa.
Wanabiafra wakishusha kilima cha Mbagala kuelekea Zakheem

Mwenyekiti wa klabu ya Biafra, Abdul Mollel akizungumzia maandalizi ya siku hiyo alitanabaisha kwamba, maandalizi yanaendelea, wanachama wamekuwa wakikutana mara mara katika kuhakikisha siku hiyo inafanyika kwa kadri ilivyopangwa.

Pia alitanabaisha kwamba, fursa ya kudhamini BIAFRA DAY 2012 ipo kwa  kampuni, mashirika au mtu binafsi hivyo aliwaomba wadau wote kujitokeza kwa wingi katika kuidhamini siku hiyo.
Baadhi ya washiriki wakielekea katika viwanja vya Biafra - BIAFRA DAY 2011

BIAFRA DAY 2011 - washiriki wakijiandaa kuanza mashindano ya mbio mita 100


KWA UDHAMINI:
WASILIANA NA:
0717 375375 (MWENYEKITI)
0719 947700 (MWEKA HAZINA)
0715 253 653 (KATIBU MKUU)

AU TUANDIKIE BARUA PEPE:



TANZIA: MWANABIAFRA ASHA YUSUF AFIWA NA BABA YAKE MZAZI LEO TAREHE 5 JULAI, 2012

Klabu ya michezo ya Biafra, kwa masikitiko makubwa inapenda kuwatangazia wanachama, wadau, mashabiki na wapenda michezo kwa ujumla kwamba mwanachama mwenzao ASHA YUSUPH (pichani chini) amefiwa na BABA YAKE MZAZI asubuhi ya leo tarehe 5 Julai, 2012 katika hospitali ya Mwananyamala.
ASHA YUSUPH (WA KWANZA KUSHOTO) AKIWA NA EDITHA TUNGARAZA NA NANCY RUPIA

Akizungumza na Katibu wa Biafra, Asha aliwaarifu wadau wote kwamba, msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu Kinondoni Shamba na mazishi yatafanyika kesho jioni huko shambani kwa marehemu Kongowe (mbagala) Dar es Salaam.
Asha Yusuf (wa tano toka kushoto waliosimama mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wanabiafra

Kwa niaba ya wanachama na wadau wote wa Biafra, mwenyekiti anatoa pole kwa mwanachama mwenzetu pamoja na ndugu, jamaa na rafiki zake kwa msiba huo na pia kuwaomba Wanabiafra wote kumfariji mwanachama mwenzao. Kwa mawasiliano, namba ya Asha Yusuph ni 0659327117.

Inna Lillahi - Wa Inna Ilaihi Raaji'un, Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa; Jina lake Lihimidiwe.