Tuesday, March 26, 2013

MCHAKATO WA MASHINDANO YA FIFA COPA COCA COLA (U15) 2013 WAANZA RASMI

Mchakato wa mashindano ya Fifa Copa Coca Cola kwa mwaka 2013 umeanza rasmi leo ambapo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodgar Chilla Tenga alifungua semina elekezi iliyoshirikisha makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na waratibu wa mikoa wa michezo ya UMISSETA ambao katika ngazi ya wilaya na mkoa wao ndio waendeshaji na wasimamizi wa mashindano hayo. 


Kikosi cha Timu ya Vijana ya Bifra (BYFT) kilichoshiriki michuano ya Copa Coca Cola (17) mwaka 2012 mkoa wa Kinondoni


BYFT wakisalimiana na wachezaji wa African Talent - Copa Coca Cola (U17) 2012
Rais Tenga alitanabaisha kwamba kuanzia mwaka huu, michuano ya FIFA Copa Coca-Cola itakuwa ikishirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15. Hivyo, amewataka viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha wanaingiza wachezaji wenye umri sahihi katika michuano hiyo. 
Nahodha wa BYFT (kulia) pamoja na mwamuzi na nahodha ya African Talent
Rais Tenga alionya kuwa hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao wamezidi umri unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo ni kubaini vipaji na kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu. Pia alisisitiza washiriki wa semina hiyo kuwepo wakati michuano hiyo ikiendelea “Kwanza nawashukuru kwa kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni vizuri pia mkahakikisha mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya ambayo tutakubaliana katika semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza kutuanzishia mambo mengine badala ya yale tutakayokubaliana,” amesema Tenga.
Baadhi ya wachezaji wa BYFT wakiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Klabu ya Biafra - Michael Silili (mweye fulana ya nyeupe)
 
Michuano hiyo kwa mwaka huu 2013 inatarajiwa kuanzia katika ngazi ya wilaya mwezi Aprili na fainali zake katika ngazi ya taifa zitafanyika mwezi Septemba.  
 
Viongozi, wachezaji na mashabiki wa BYFT katika picha ya pamoja
Klabu ya michezo ya Biafra inatarajia kuingiza timu yake ya vijana katika michuano mara baada ya Kamati ya Utendaji kukutana na kocha, mameneja wa timu pamoja na wachezaji ili kupanga mikakati ya ushiriki wao.

Thursday, March 21, 2013

JOGGING; HISTORIA, UMUHIMU NA USALAMA WAKATI WA MAZOEZI (SEHEMU YA PILI))

Katika sehemu ya kwanza ya makala hii tuliangalia zaidi maana ya jogging pamoja na utaratibu wake. Fuatilia makala haya kwa sehemu ya pili juu ya historia ya jogging Tanzania

Hatuwezi kuizungumzia jogging bila ya kutaja au kuihusisha wilaya ya Temeke katika mkoa wa Dar es Salaam. Tangu miaka ya 80, Wakaazi wengi wa wilaya ya Temeke wamekuwa ni watu ambao wanajihusisha na michezo mbalimbali moja kwa moja. Hivyo basi, hata jogging ilianza kushika kasi wilaya ya Temeke kabla ya kusambaa katika wilaya nyingine za Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. 
Wana jogging wakikatiza barabara ya uwanja wa taifa
  
Wana jogging wakikatia barabara ya Kilwa
Temeke Jogging ni moja kati ya klabu kongwe za jogging Tanzania na ni miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wa mchezo huo. Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu za mwanzo kabisa kujikusanya na kuanzisha klabu ambayo inajihusisha na mchezo wa jogging zaidi. 
Wana jogging Temeke
Viongozi wa Tameke Jogging
Baada ya Temeke Jogging kuanzisha klabu yao, makundi mengine mengi nayo yakajiunda na kuanzisha vilabu vyao. Kama ukipata fursa ya kutembelea Temeke siku za mwisho wa wiki hasa majira ya asubuhi utashuhudia makundi kwa makundi ya watu wakifanya jogging. Kutoka Temeke jogging ikasambaa hadi wilaya nyingine Dar es Salaam ambapo kwa wilaya ya Kinondoni Klabu ya kwanza kuanzishwa ilikuwa  ni Namanga Jogging.
Namanga Jogging wakikatiza barabara ya Ali Hassan Mwinyi
 Baada ya kustawi kwa klabu ya Namanga, vilabu vingine kadhaa vya jogging katika Wilaya ya Kinondoni hasa baada ya Kanali Fabian Massawe ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni (wakati huo) kuhimiza wenyeviti wa serikali za mitaa katika wilaya ya Kinondoni kuanzisha vilabu vya jogging kwenye mitaa yao ili kulinda afya za wakaazi wa Kinondoni. 

Miongoni mwa klabu zilizoanzishwa baada ya kupata hamasa ya Namanga ni klabu ya michezo ya Biafra ambayo pamoja na michezo mingine inajihusisha moja kwa moja na jogging ambapo wanachama pamoja na wadau wengine hujumuika pamoja siku za jumapili alfajiri na kufanya jogging.

Wanabiafra wakiwa kwenye jogging
Kwa sasa wilaya ya Kinondoni kama ilivyo Temeke, siku za mwisho wa juma watu wengi hujitokeza na kufanya jogging katika barabara mbalimbali.

Itaendelea ...........

Wednesday, March 20, 2013

JOGGING; HISTORIA, UMUHIMU NA USALAMA WAKATI WA MAZOEZI (SEHEMU YA KWANZA)

"Jogging" ni hali ya kukimbia pole pole kwa ajili ya kufanya mazoezi, hivyo mchezo huu unajulikana kama mchezo wa mbio za pole pole. Jogging inaweza kufanywa na mtu mmoja au kikundi cha watu ambao hukimbia pole pole kwa umbali fulani ili kujiweka sawa kiafya. Watu wengi hufanya mazoezi ya mbio za pole pole siku za mapumziko ya mwisho wa wiki yaani jumamosi na jumapili hasa majira ya asubuhi na jioni.
Watu wakiwa kwenye mazoezi ya mbio za pole pole (jogging)
Ili kuleta hamasa na ari ya mazoezi kwa wanamichezo, mara nyingi wakimbiaji huimba nyimbo na vibwagizo mbalimbali na wakati mwingine hukimbia huku wakiweka na vionjo vya kucheza kulingana na mirindimo ya nyimbo za hamasa zinazoimbwa. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Biafra Michael Silili (mwenye vuvuzela) akiwaimbisha wakimbiaji


Kutokana na ufinyu wa miundo mbinu hasa ya barabara za waenda kwa miguu, washiriki wa mchezo huu hutumia barabara za jumuia (public roads) kama sehemu ya kukimbilia hali ambayo wakati mwingine huhatarisha usalama wa wakimbiaji kutokana na kukimbia katika barabara ambazo zinatumika pia na vyombo vya moto kama vile magari na pikipiki. 

Wana-jogging wakipishana na vyombo vya moto barabarani (pichani chini na juu)

Ili kuweza kukabiliana na changamoto za usalama barabarani wakati wa mazoezi wanamichezo hujipanga katika mistari isiyozidi mitatu huku waongozaji wakiwa wawili ambapo mmoja huwa mbele na mwingine huwa nyuma ili kuweza ukongoza wanamichezo na magari. Waongozaji hao hutumia bendera nyekundu na kijani wakati wa kuongoza. Wanamichezo hutumia upande wa kushoto wa barabara ili kuruhusu vyombo vya moto navyo kutumia barabara hizo. 

Mpangilio wa mistari mitatu unavyoonekana
Waongozaji wa mbele wakiwa na bendera

Mara nyingi katika mazoezi ya jogging wakimbiaji wenye umri mdogo hutangulia mbele ili kuhakikisha usalama wao na pia kwa ajili ya urahisi wa kuwapatia huduma ya kwanza iwapo itahitajika.
Watoto wakiwa kwenye jogging
 Itaendelea ................

Tuesday, March 19, 2013

YALIYOJIRI KWENYE JOGGING JUMAPILI TAREHE 17 MACHI 2013

Jumapili tarehe 17 Machi, 2013 wanamichezo toka vilabu vya Namanga, Mwananyamala, Kunduchi Kwanza na wenyeji wao Biafra walifanya mazoezi ya pamoja  ya mbio za pole pole ambazo zilianzia makao ya klabu hiyo hadi barabara ya Kawawa, kisha barabara ya mwananyama, hadi mwananyamala hospitali, studio mpaka barabara ya Kinondoni na hatimaye Kawawa hadi klabuni. Bbaadae walimpongeza mwanachama wa Biafra Bi. Miriam Joseph kwa kujifungua mtoto wa kiume takriban miezi miwili iliyopita. Fuatilia matukio kwa picha. 
Katibu wa mwananyamala Jogging akiwasalimia wanamichezo

Baadhi wa wana-Mwananyamala Jogging
Makamu M/kiti wa Biafra Jaqueline Barozi (kulia) akiwa na mjumbe mteule wa kamati ya Uchumi na Mipango ya klabu ya Biafra Ayoub Layson wakifuatilia matukio
Mwenyekiti wa Biafra Abdul mollel (aliyesimama) akiwasalimia wadau



Katibu wa Biafra Yahya Poli akimpongea Bi. Miriam Jospeh kwa kupata mtoto wa kiume
Miriam Joseph akiwasalimu na kuwashukuru wanamichezo waliojitokeza na kumpongeza
Viongozi wa Kunduchi Kwanza Kaka Jffari na Shekhan Khamis
Siku hiyo pia, klabu ya Mwananyamala Jogging ilimtuma mwakilishi wake Bertha (pichani chini) kushiriki mbio za nusu marathoni zilizofanyika wilaya ya Ilala ambapo mwanachama huyo alijinyakulia nafasi ya pili na kupata medali ya fedha. Baada ya kutoka huko alijumuika pamoja na wanamichezo wengine klabuni Biafra.
Bertha aliyeshinda mbi za nusu Marathoni akiiwakilisha Mwananyamala Jogging
KUTOKA MAENEO MENGINE: -
Taarifa kutoka maeneo mengine ni kuwa klabu ya Kunduchi Jogging ambayo makao makuu yake yapo Ngalawa kunduchi Mtongani iliandaa bonanza la michezo ambalo liliwakuta pamoja wanamichezo kutoka katika vilabu mbalimbali kama vile Kawe Social and Sports Club, Msasani, n.k. 


Bonanza hilo lilihusisha mbio za pole pole na hatimaye mchezo wa mpira wa miguu kwa timu za veterani kutoka vilabu vilivyoalikwa.

YALIYOJIRI KWENYE BBQ NA MARAFIKI WA UKWELI IJUMAA YA TAREHE 15 MACHI 2013

Katika kuendeleza mahusiano mazuri na kuwa na wakati mzuri kwa marafiki wa ukweli, ijumaa juma lililopita ilikuwa ni siku ni sik nzuri kwa marafiki waliojumuika pamoja katika kuianza wikiendi. Ili kuweza kuifanya jioni hiyo kuwa nzuri zaidi, wadau walioshiriki walijipatia fursa ya kupata mbuzi choma (BBQ) pamoja na vinywaji pale Chimbinga Unique Pub huku wakiburudishwa na muziki maridhawa kwa ajili ya jioni hiyo toka kwa dj.
Baadhi ya wadau waliofika mapema Chimbinga


Wadau waki-show love

Dj akipanga mambo yake

Mbuzi nayo ikiendelea kuiva


tayari imeiva

Mama Chimbinga - Rose Mwakibugi (mwenye rasta) akishuhudia maandalizi ya BBQ

Wadau wakipata supu ya utumbo wa mbuzi!

Muda wa mlo ukawadia

Chit-Chat and Networking ikiendelea
Wadau wakionesha upendo
Wadau walipendekeza tukio liwe linafanyika kila ijumaa ya mwisho ya wa mwezi na taarifa ziwafikie mapema ili waweze kujiandaa vya kutosha ikiwemo kuwakilisha uchakavu wao kwa wahusika!

Thursday, March 14, 2013

TAARIFA KUTOKA KWA MSAJILI WA VYAMA NA VILABU VYA MICHEZO WILAYA A KINONDONI

JE KUNA MAOMBI YA USAJILI WA CHAMA AU KLABU YA MICHEZO YAPO KWA MSAJILI UKISUBIRI CHETI? BASII HI NI HABARI NJEMA KWAKO!

Msajili wa vyama na vilabu vya michezo manispaa ya Kinondoni ndugu Jumanne Mrimi (pichani) ametoa wito kwa vyama na vilbu vyote ambavyo viliwasilisha maombi ya usajili wa vyama au vilabu kuwa wanaweza kuanza kufuatilia vyeti vyao kwa msajili wa vyama na vilabu vya michezo Tanzania. 
Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo Manispaa ya Kinondoni ndugu Jumanne Mrimi
Akizungumza na blogu hii ofisini kwake, ndugu Mrimi alitanabaisha kwamba, zoezi la utoaji wa vyeti kwa vyama na vilabu vilivyokamilisha taratibu zote za usajili lilisimama kutokana na kutokuwepo kwa msajili wa vyama na vilabu vya michezo nchini kwa takriban mwaka mmoja. Hivyo, zoezi hilo limeanza rasmi baada ya kupatikana kwa msajili. Pia alikumbusha kuwa mara baada ya kupata vyeti, ni muhimu vyama na vilabu hivyo vikawasilisha ofisini kwake nakala ya vyeti hivyo kwa ajili ya kumbukumbu. Msajili pia alitumia fursa hiyo kuipongeza klabu ya michezo ya Biafra kwa kupata cheti cha usajili na kuwakumbusha kuwa ni vyema sasa kwao kutimiza malengo waliyojiwekea katika kuhamasisha na kuinua michezo katika manispaa ya Kinondoni.
Cheti cha Klabu ya Biafra
Moja kati ya vilabu vilivyopata usajili wake mnamo mwezi februari, 2013 ni klabu ya michezo ya Biafra ambayo imesajiliwa tarehe 20 Februari, 2013 na kupewa namba ya NSC 9848.

Ofisi ya msajili wa vyama na vilabu vya michezo ipo katika jengo la Jubilee, ghorofa ya 9, mtaa wa ohio.  

Tuesday, March 12, 2013

UNAALIKWA KUJUMUIKA NA MARAFIKI SIKU YA IJUMAA TAREHE 15 MACHI, 2013

Kama ilivyo ada, kwa mara ya pili tena CHIMBINGA UNIQUE PUB kwa kushirikiana na BIAFRA SPORTS CLUB wanakualika wewe mdau, kujumuika pamoja na marafiki mbalimbali katika shamra shamra za kuianza wikiendi yako. Akizungumza maandalizi ya siku hiyo mdau wa Biafra na Mkurugenzi wa Chimbinga Unique Pub ndugu Robert Mwakibugi (pichani) almaarufu CHIMBINGA alithibitisha kwamba tarehe 15 Machi, 2013 kuanzia saa 1:00 jioni wadau wote watakuwa Chimbinga Unique Pub tayari kwa kuianza wikiendi pamoja na marafiki. 
Robert Mwakibugi akiiwakilisha Chimbinga Unique Pub
 Katika kuipendezesha siku hiyo, Chimbinga alifafanua kuwa kutakuwa na burudani mbalimbali hasa muziki wa bolingo, funk, sweet reggae, n.k. na katika kuinogesha zaidi siku hiyo patakuwa na mbuzi choma (BBQ) kwa ajili ya wadau watakaohudhuria.


Mwanabiafra na mdau maarufu wa Chimbinga Unique Pub - Dastun Barozi (kulia) akiwa na marafiki zake Chimbinga
Ili kuweza kuifanya siku hiyo iwe ya kipekee na ipendeze zaidi, Chimbinga aliwakumbusha wadau kuchangia uchakavu wa Tshs. 10, 000/= kwa kila mtu anayependa kushiriki siku hiyo.

USISAHAU, NI IJUMAA HII TAREHE 15 MACHI, 2013. NJOO WEWE, NA YULE TUKUTANE NA MARAFIKI ZETU WA UKWELI, TUPATE BURUDANI ZA UKWELI NA TUIANZE WIKIENDI YETU KIUKWELI.

Monday, March 11, 2013

KUNDUCHI KWANZA YAFANIKISHA MAZOEZI PAMOJA NA HARAMBEE TAREHE 10 MACHI, 2013

Jana tarehe 10 Machi, 2013 wanamichezo kutoka Kawe Beach, Kawe Social & Sports Club, Msasani Jogging & Sports Club, Naamanga Sports Club, Biafra Sports Club pamoja na wenyeji Kunduchi Kwanza walikusanyika pamoja na kufanya mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambazo ziliwakutanisha zaidi ya wanamichezo 100 pamoja na wadau wengine. Mbio hizo zilianzia Makao Makuu ya klabu ya Kunduchi Kwanza Malanja kupitia mbuyuni, Afrikana, kipita shoto (round about) cha Kawe na kisha kurudia njia hiyo hiyo hadi Malanja. 
Kundi la Msasani  

Kundi la mwisho

Michael Juma aka Mopao (mwenye bukta nyeusi mbele) akiongoza Earobics 


Mara baada ya mazoezi ya mbio pamoja na aerobics, wanamichezo waliendelea kupata mapumziko mafupi na burudani mbalimbali zilizoandaliwa.
Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (mwenye bukta ya bluu) akijadiliana jambo na wadau

Wadau wakipata supu

Wenyeji Kunduchi Kwanza wakifuatilia matukio
Mwenyekiti wa Kawe Social and Sports Club almaarufu Mzee Risasi (menye fulana nyeupe akiwa na wadau
Baada ya mapumziko na burudani mbalimbali, wanamichezo walijumuika tena pamoja kwa ajili ya tukio mahususi kwa ajili ya siku hiyo ambapo wana Kunduchi Kwanza pamoja na wanamichezo na wadau wengine wote waliohudhuria walipata fursa ya kumpa pole Mmiliki wa Malanja Executive Inn ambaye pia ni mlezi na mdhamini wa klabu ya Kunduchi Kwanza baada ya kuunguliwa na ukumbi wa Malanja sehemu ambayo pamoja na kutumika kwa ajili ya matukio mbalimbali ya kijamii wana Kunduchi kwanza walikuwa wakiutumia kwa ajili ya mikutano yao. 
Wana Kunduchi Kwanza wakiwa kwenye mkutano ndani ya Malanja Hall kabla ya kuungua
Zoezi la kutoa pole lilifanyika pamoja na harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi huo ambapo wanamichezo wote waliokuwepo walichangia kwa kadri ya uwezo na vilabu vyote vilivyoshiriki navyo vilichangia.  
MC akiwakaribisha Kunduchi Kwanza (pichani) kusalimiana na wadau

Wana Kunduchi Kwanza

Wana Kawe Social & Sports Club wakisalimia wadau 

wana Msasani Jogging wakiongozwa na Katibu Mkuu wao ndugu Mangula

Wana Namanga Sports Club 

Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel akitoa pole za klabu yake

Sehemu ya pesa taslimu zilizochangwa mara tu baada ya kuanza harambee

Mweka Hazina wa Kunduchi Kwanza (kulia) akiwa na Malanja 

Kamati ya kusimamia zoezi la harambee wakijiandaa kumkabidhi rambi rambi mhanga bwana Massawe almaarufu Malanja
Katika harambee hiyo wanamichezo pamoja na wadau wote walionyesha kuguswa sana ajali hiyo ambapo kwa muda mfupi tu zilipatikana pesa taslimu zaidi ya shilingi laki nne na ahadi zaidi ya shilingi pia toka katika vilabu vilivyoshiriki harambee hiyo.
Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed akimkabidhi Malanja mchango wa harambee
Bwana Malanja akiwaonesha wadau mchango alioupokea
 Pia wadau walichangia vifaa ambapo klabu ya Kawe wao waliahidi kuchangia zaidi ya viunga mia moja vya makuti mara tu ujenzi utakapoanza pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu.  Mwakilishi wa Kunduchi Veterani pamoja na wanachama wao wote waliahidi kuchangia viti 10 katika harambee hiyo pia. 
Kunduchi Veterani
Jumla ya michango yote ilikuwa takriban shilingi milioni moja na laki mbili na nusu. Akizungumza baada ya kukabidhiwa mchango huo, bwana Malanja alitoa shukrani kwa wanamichezo wote walioshiriki katika harambee hiyo na pia alieleza namna alivyoguswa na upendo walioonyesha wana Kunduchi Kwanza tangu ilipotokea ajali hiyo ya moto mpaka sasa ambapo wamekuwa wakimpa moyo na kuahidi kutoa ushirikiano wao pindi ujenzi utakapoanza. 
Mzee risasi akiwa na Malanja

Mopao na mzee Ole
Akipokea shukrani hizo kwa niaba ya wanamichezo na wadau mweka hazina wa Namanga bwana Michael J Juma almaarufu Mopao alimhakikishia bwa Malanja kuwa kwa mchango huo wanamichezo wameonyesha ni jinsi gani wana upendo kwakwe na kumuomba aupokee kwa moyo mmoja kwa hicho ndicho wadau walichojaaliwa kukipata kwa wakati ule. 

Mdau akichagiza kwa dansi kuashiria kukamilika kwa harambee

Wadau wakiserebuka

Baada ya kumalizika kwa harambee, wanamichezo na wadau wengine waliendelea kupata burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa. 
Baadhi ya wana Kunduchi Kwanza wakiongozwa na Katibu Msaidizi Bi Sizya Risasi (wa kwanza kulia)