Mchakato wa mashindano ya Fifa Copa Coca Cola kwa mwaka 2013 umeanza rasmi leo ambapo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodgar Chilla Tenga alifungua semina elekezi iliyoshirikisha
makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na waratibu wa mikoa wa
michezo ya UMISSETA ambao katika ngazi ya wilaya na mkoa wao ndio waendeshaji na wasimamizi wa mashindano hayo.
Kikosi cha Timu ya Vijana ya Bifra (BYFT) kilichoshiriki michuano ya Copa Coca Cola (17) mwaka 2012 mkoa wa Kinondoni |
BYFT wakisalimiana na wachezaji wa African Talent - Copa Coca Cola (U17) 2012 |
Rais Tenga
alitanabaisha kwamba kuanzia mwaka huu, michuano ya FIFA Copa
Coca-Cola itakuwa
ikishirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15. Hivyo, amewataka viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha
wanaingiza wachezaji wenye umri sahihi katika michuano hiyo.
Nahodha wa BYFT (kulia) pamoja na mwamuzi na nahodha ya African Talent |
Rais
Tenga alionya kuwa hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao
wamezidi umri unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo ni
kubaini vipaji na kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu. Pia alisisitiza washiriki wa semina hiyo kuwepo wakati michuano hiyo ikiendelea “Kwanza
nawashukuru kwa kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni
vizuri pia mkahakikisha mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya
ambayo tutakubaliana katika semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza
kutuanzishia mambo mengine badala ya yale tutakayokubaliana,” amesema
Tenga.
Baadhi ya wachezaji wa BYFT wakiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Klabu ya Biafra - Michael Silili (mweye fulana ya nyeupe) |
Michuano hiyo kwa mwaka huu 2013 inatarajiwa kuanzia katika ngazi ya wilaya mwezi Aprili na fainali zake katika ngazi ya taifa zitafanyika mwezi Septemba.
Viongozi, wachezaji na mashabiki wa BYFT katika picha ya pamoja |
Klabu ya michezo ya Biafra inatarajia kuingiza timu yake ya vijana katika michuano mara baada ya Kamati ya Utendaji kukutana na kocha, mameneja wa timu pamoja na wachezaji ili kupanga mikakati ya ushiriki wao.
No comments:
Post a Comment