Wednesday, March 20, 2013

JOGGING; HISTORIA, UMUHIMU NA USALAMA WAKATI WA MAZOEZI (SEHEMU YA KWANZA)

"Jogging" ni hali ya kukimbia pole pole kwa ajili ya kufanya mazoezi, hivyo mchezo huu unajulikana kama mchezo wa mbio za pole pole. Jogging inaweza kufanywa na mtu mmoja au kikundi cha watu ambao hukimbia pole pole kwa umbali fulani ili kujiweka sawa kiafya. Watu wengi hufanya mazoezi ya mbio za pole pole siku za mapumziko ya mwisho wa wiki yaani jumamosi na jumapili hasa majira ya asubuhi na jioni.
Watu wakiwa kwenye mazoezi ya mbio za pole pole (jogging)
Ili kuleta hamasa na ari ya mazoezi kwa wanamichezo, mara nyingi wakimbiaji huimba nyimbo na vibwagizo mbalimbali na wakati mwingine hukimbia huku wakiweka na vionjo vya kucheza kulingana na mirindimo ya nyimbo za hamasa zinazoimbwa. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Biafra Michael Silili (mwenye vuvuzela) akiwaimbisha wakimbiaji


Kutokana na ufinyu wa miundo mbinu hasa ya barabara za waenda kwa miguu, washiriki wa mchezo huu hutumia barabara za jumuia (public roads) kama sehemu ya kukimbilia hali ambayo wakati mwingine huhatarisha usalama wa wakimbiaji kutokana na kukimbia katika barabara ambazo zinatumika pia na vyombo vya moto kama vile magari na pikipiki. 

Wana-jogging wakipishana na vyombo vya moto barabarani (pichani chini na juu)

Ili kuweza kukabiliana na changamoto za usalama barabarani wakati wa mazoezi wanamichezo hujipanga katika mistari isiyozidi mitatu huku waongozaji wakiwa wawili ambapo mmoja huwa mbele na mwingine huwa nyuma ili kuweza ukongoza wanamichezo na magari. Waongozaji hao hutumia bendera nyekundu na kijani wakati wa kuongoza. Wanamichezo hutumia upande wa kushoto wa barabara ili kuruhusu vyombo vya moto navyo kutumia barabara hizo. 

Mpangilio wa mistari mitatu unavyoonekana
Waongozaji wa mbele wakiwa na bendera

Mara nyingi katika mazoezi ya jogging wakimbiaji wenye umri mdogo hutangulia mbele ili kuhakikisha usalama wao na pia kwa ajili ya urahisi wa kuwapatia huduma ya kwanza iwapo itahitajika.
Watoto wakiwa kwenye jogging
 Itaendelea ................

No comments:

Post a Comment