Jumapili tarehe 17 Machi, 2013 wanamichezo toka vilabu vya Namanga, Mwananyamala, Kunduchi Kwanza na wenyeji wao Biafra walifanya mazoezi ya pamoja ya mbio za pole pole ambazo zilianzia makao ya klabu hiyo hadi barabara ya Kawawa, kisha barabara ya mwananyama, hadi mwananyamala hospitali, studio mpaka barabara ya Kinondoni na hatimaye Kawawa hadi klabuni. Bbaadae walimpongeza mwanachama wa Biafra Bi. Miriam Joseph kwa kujifungua mtoto wa kiume takriban miezi miwili iliyopita. Fuatilia matukio kwa picha.
Katibu wa mwananyamala Jogging akiwasalimia wanamichezo |
Baadhi wa wana-Mwananyamala Jogging |
Makamu M/kiti wa Biafra Jaqueline Barozi (kulia) akiwa na mjumbe mteule wa kamati ya Uchumi na Mipango ya klabu ya Biafra Ayoub Layson wakifuatilia matukio |
Mwenyekiti wa Biafra Abdul mollel (aliyesimama) akiwasalimia wadau |
Katibu wa Biafra Yahya Poli akimpongea Bi. Miriam Jospeh kwa kupata mtoto wa kiume |
Miriam Joseph akiwasalimu na kuwashukuru wanamichezo waliojitokeza na kumpongeza |
Viongozi wa Kunduchi Kwanza Kaka Jffari na Shekhan Khamis |
Siku hiyo pia, klabu ya Mwananyamala Jogging ilimtuma mwakilishi wake Bertha (pichani chini) kushiriki mbio za nusu marathoni zilizofanyika wilaya ya Ilala ambapo mwanachama huyo alijinyakulia nafasi ya pili na kupata medali ya fedha. Baada ya kutoka huko alijumuika pamoja na wanamichezo wengine klabuni Biafra.
Bertha aliyeshinda mbi za nusu Marathoni akiiwakilisha Mwananyamala Jogging |
Taarifa kutoka maeneo mengine ni kuwa klabu ya Kunduchi Jogging ambayo makao makuu yake yapo Ngalawa kunduchi Mtongani iliandaa bonanza la michezo ambalo liliwakuta pamoja wanamichezo kutoka katika vilabu mbalimbali kama vile Kawe Social and Sports Club, Msasani, n.k.
Bonanza hilo lilihusisha mbio za pole pole na hatimaye mchezo wa mpira wa miguu kwa timu za veterani kutoka vilabu vilivyoalikwa.
No comments:
Post a Comment