Monday, March 11, 2013

KUNDUCHI KWANZA YAFANIKISHA MAZOEZI PAMOJA NA HARAMBEE TAREHE 10 MACHI, 2013

Jana tarehe 10 Machi, 2013 wanamichezo kutoka Kawe Beach, Kawe Social & Sports Club, Msasani Jogging & Sports Club, Naamanga Sports Club, Biafra Sports Club pamoja na wenyeji Kunduchi Kwanza walikusanyika pamoja na kufanya mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambazo ziliwakutanisha zaidi ya wanamichezo 100 pamoja na wadau wengine. Mbio hizo zilianzia Makao Makuu ya klabu ya Kunduchi Kwanza Malanja kupitia mbuyuni, Afrikana, kipita shoto (round about) cha Kawe na kisha kurudia njia hiyo hiyo hadi Malanja. 
Kundi la Msasani  

Kundi la mwisho

Michael Juma aka Mopao (mwenye bukta nyeusi mbele) akiongoza Earobics 


Mara baada ya mazoezi ya mbio pamoja na aerobics, wanamichezo waliendelea kupata mapumziko mafupi na burudani mbalimbali zilizoandaliwa.
Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (mwenye bukta ya bluu) akijadiliana jambo na wadau

Wadau wakipata supu

Wenyeji Kunduchi Kwanza wakifuatilia matukio
Mwenyekiti wa Kawe Social and Sports Club almaarufu Mzee Risasi (menye fulana nyeupe akiwa na wadau
Baada ya mapumziko na burudani mbalimbali, wanamichezo walijumuika tena pamoja kwa ajili ya tukio mahususi kwa ajili ya siku hiyo ambapo wana Kunduchi Kwanza pamoja na wanamichezo na wadau wengine wote waliohudhuria walipata fursa ya kumpa pole Mmiliki wa Malanja Executive Inn ambaye pia ni mlezi na mdhamini wa klabu ya Kunduchi Kwanza baada ya kuunguliwa na ukumbi wa Malanja sehemu ambayo pamoja na kutumika kwa ajili ya matukio mbalimbali ya kijamii wana Kunduchi kwanza walikuwa wakiutumia kwa ajili ya mikutano yao. 
Wana Kunduchi Kwanza wakiwa kwenye mkutano ndani ya Malanja Hall kabla ya kuungua
Zoezi la kutoa pole lilifanyika pamoja na harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi huo ambapo wanamichezo wote waliokuwepo walichangia kwa kadri ya uwezo na vilabu vyote vilivyoshiriki navyo vilichangia.  
MC akiwakaribisha Kunduchi Kwanza (pichani) kusalimiana na wadau

Wana Kunduchi Kwanza

Wana Kawe Social & Sports Club wakisalimia wadau 

wana Msasani Jogging wakiongozwa na Katibu Mkuu wao ndugu Mangula

Wana Namanga Sports Club 

Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel akitoa pole za klabu yake

Sehemu ya pesa taslimu zilizochangwa mara tu baada ya kuanza harambee

Mweka Hazina wa Kunduchi Kwanza (kulia) akiwa na Malanja 

Kamati ya kusimamia zoezi la harambee wakijiandaa kumkabidhi rambi rambi mhanga bwana Massawe almaarufu Malanja
Katika harambee hiyo wanamichezo pamoja na wadau wote walionyesha kuguswa sana ajali hiyo ambapo kwa muda mfupi tu zilipatikana pesa taslimu zaidi ya shilingi laki nne na ahadi zaidi ya shilingi pia toka katika vilabu vilivyoshiriki harambee hiyo.
Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed akimkabidhi Malanja mchango wa harambee
Bwana Malanja akiwaonesha wadau mchango alioupokea
 Pia wadau walichangia vifaa ambapo klabu ya Kawe wao waliahidi kuchangia zaidi ya viunga mia moja vya makuti mara tu ujenzi utakapoanza pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu.  Mwakilishi wa Kunduchi Veterani pamoja na wanachama wao wote waliahidi kuchangia viti 10 katika harambee hiyo pia. 
Kunduchi Veterani
Jumla ya michango yote ilikuwa takriban shilingi milioni moja na laki mbili na nusu. Akizungumza baada ya kukabidhiwa mchango huo, bwana Malanja alitoa shukrani kwa wanamichezo wote walioshiriki katika harambee hiyo na pia alieleza namna alivyoguswa na upendo walioonyesha wana Kunduchi Kwanza tangu ilipotokea ajali hiyo ya moto mpaka sasa ambapo wamekuwa wakimpa moyo na kuahidi kutoa ushirikiano wao pindi ujenzi utakapoanza. 
Mzee risasi akiwa na Malanja

Mopao na mzee Ole
Akipokea shukrani hizo kwa niaba ya wanamichezo na wadau mweka hazina wa Namanga bwana Michael J Juma almaarufu Mopao alimhakikishia bwa Malanja kuwa kwa mchango huo wanamichezo wameonyesha ni jinsi gani wana upendo kwakwe na kumuomba aupokee kwa moyo mmoja kwa hicho ndicho wadau walichojaaliwa kukipata kwa wakati ule. 

Mdau akichagiza kwa dansi kuashiria kukamilika kwa harambee

Wadau wakiserebuka

Baada ya kumalizika kwa harambee, wanamichezo na wadau wengine waliendelea kupata burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa. 
Baadhi ya wana Kunduchi Kwanza wakiongozwa na Katibu Msaidizi Bi Sizya Risasi (wa kwanza kulia)

No comments:

Post a Comment