Thursday, March 14, 2013

TAARIFA KUTOKA KWA MSAJILI WA VYAMA NA VILABU VYA MICHEZO WILAYA A KINONDONI

JE KUNA MAOMBI YA USAJILI WA CHAMA AU KLABU YA MICHEZO YAPO KWA MSAJILI UKISUBIRI CHETI? BASII HI NI HABARI NJEMA KWAKO!

Msajili wa vyama na vilabu vya michezo manispaa ya Kinondoni ndugu Jumanne Mrimi (pichani) ametoa wito kwa vyama na vilbu vyote ambavyo viliwasilisha maombi ya usajili wa vyama au vilabu kuwa wanaweza kuanza kufuatilia vyeti vyao kwa msajili wa vyama na vilabu vya michezo Tanzania. 
Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo Manispaa ya Kinondoni ndugu Jumanne Mrimi
Akizungumza na blogu hii ofisini kwake, ndugu Mrimi alitanabaisha kwamba, zoezi la utoaji wa vyeti kwa vyama na vilabu vilivyokamilisha taratibu zote za usajili lilisimama kutokana na kutokuwepo kwa msajili wa vyama na vilabu vya michezo nchini kwa takriban mwaka mmoja. Hivyo, zoezi hilo limeanza rasmi baada ya kupatikana kwa msajili. Pia alikumbusha kuwa mara baada ya kupata vyeti, ni muhimu vyama na vilabu hivyo vikawasilisha ofisini kwake nakala ya vyeti hivyo kwa ajili ya kumbukumbu. Msajili pia alitumia fursa hiyo kuipongeza klabu ya michezo ya Biafra kwa kupata cheti cha usajili na kuwakumbusha kuwa ni vyema sasa kwao kutimiza malengo waliyojiwekea katika kuhamasisha na kuinua michezo katika manispaa ya Kinondoni.
Cheti cha Klabu ya Biafra
Moja kati ya vilabu vilivyopata usajili wake mnamo mwezi februari, 2013 ni klabu ya michezo ya Biafra ambayo imesajiliwa tarehe 20 Februari, 2013 na kupewa namba ya NSC 9848.

Ofisi ya msajili wa vyama na vilabu vya michezo ipo katika jengo la Jubilee, ghorofa ya 9, mtaa wa ohio.  

No comments:

Post a Comment