Friday, March 08, 2013

JUMAPILI HII JOGGING NI KUNDUCHI KWANZA

Katika kuhamasisha uimarishaji wa afya kwa kutumia michezo pamoja na kuimarisha ujirani mwema klabu ya michezo ya Kunduchi Kwanza kwa kushirikiana na vilabu vya Namanga, Kawe na Biafra pamoja na wadau wengine iimeandaa na kuwaaliaka wadau wote katika mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili tarehe 10 Machi, 2013 kuanzia saa 12:20 asubuhi. Ruti ya mbio hizo itaanzia katika makao makuu ya klabu ya Kunduchi Kwanza - Malanja Pub na kisha kuzunguka maeneo mbalimbali ya kata ya Kunduchi na hatimaye kumalizika hapo hapo Malanja Pub ambapo wanamichezo watapata fursa ya kujumuika pamoja na kujadiliana maswala mbalimbali yanayohusu mchezo wa mbio za pole pole.

MWALIKO WA KUSHIRIKI MAZOEZI JUMAPILI
Akizungumzia mazoezi hayo, Katibu Mkuu wa Kunduchi Kwanza Jogging alisema kuwa siku hiyo itakuwa ni maalum kwa wanamichezo kumpa pole mwanachama wa klabu ihoy ambaye pia ni mmiliki wa Malanja ambaye alipata ajali ya kuunguliwa na eneo lake la biashara. Hivyo hakutakuwa na michezo mingine zaidi ya jogging tu.Alieleza zaidi kuwa mbio hizo zinatarajiwa kuwa na urefu wa takriban kilomita 7.



No comments:

Post a Comment