Wanamichezo takriban wote wana msemo wao kuwa "michezo ni afya, michezo ni furaha, michezo huwaunganisha watu". Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa juma lililopita kwa Wanabiafra. Siku ya ijumaa tarehe 8 Februari, 2013 ambapo Wanabiafra pamoja na marafiki kadhaa walikutana na kuianza wikiendi kwa burudani ya muziki, vinywaji na nyama choma pale Chiminga Unique Pub.
| Ally Masharubu na Ayub Layson wakitafuna nyama ya mbuzi |
| Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel alisimama kuwasalimia wanabiafra na marafiki |
| Kutoka kushoto; Ally Masharubu, Ayub Layson na Editha Tungaraza |
| Mwanabiafra Dustan Barozi (kulia) pamoja na marafiki zake |
| Editha Tungaraza akifaidi msosi |
| Makamu Mwenyekiti wa Biafra Jacqueline Barozi (aliyesimama) akichukua oda ya vinywaji |
| Rose Mwakibugi Almaarufu mama Chimbinga alihakikisha vinywaji vipo na vya kutosha |
| Robert Mwakibugi akiiwakilisha vyema Chimbinga Unique Pub |
Kama unapenda kushiriki kwenye mijumuiko ya aina hii, usisite, wasiliana na Katibu Mkuu, Biafra Sports Club kwa barua pepe; biafra.jsclub@gmail.com
No comments:
Post a Comment