Monday, February 25, 2013

VIONGOZI WA VILABU VYA JOGGING KINONDONI WAKUTANA NA MSAJILI WA VYAMA NA VILABU VYA MICHEZO WILAYA YA KINONDONI

Jioni ya tarehe 25 Februari, 2013, viongozi kutoka katika vilabu vya michezo vinavyojihusisha na mchezo wa mbio za pole pole walikutana na Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo wilaya ya Kinondoni ndugu Jumanne Mrimi (pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
Ndugu Jumanne Mrimi - Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo wilaya ya Kinondoni
 Viongozi waliomtembelea ni kutoka katika vilabu vya Namanga (David Mwaka na Andrew Mangole), Kawe (Mohammed Risasi, Alhaj Seif Mukhere na Khadija Mabrouk) Biafra ( Abdul Mollel na Yahya Poli) na Kunduchi Kwanza (Alphonsina Joseph).

David Mwaka (mwenye shati jekundu) - Mwenyekiti Namanga Sports Club


Alhaj Seif Mukhere  - Kaimu Katibu Mkuu Kawe Sports & Social Club

Mohammed Risasi - Mwenyekiti Kawe Sports & Social Club

Andrew Mangole - Katibu Mkuu Namanga Sports Club na Bi. Khadija Mabrouk - Makamu Mwenyekiti Kawe Sports and Social Club
Lengo la kumtembelea msajili ofisini kwake lilikuwa ni katika harakati za kufufua uhai na hamasa ya mchezo wa mbio za pole pole katika manispaa ya Kinondoni ambapo viongozi wa klabu hizo wamedhamiria kuhuisha Chama cha Mchezo wa Jogging wilaya ya Kinondoni kilichoasisiwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni wakati huo Kanali Fabian Massawe na kisha baadaye kuunda shirikisho la mchezo huo.

Yahya Poli - Katibu Mkuu Biafra Sports Club na Alphonsina Joseph - Katibu Mkuu Kunduchi Kwanza Jogging and Sports Club

Maazimio ya kikao hicho yalikuwa ni pamoja na kuwasiliana na vilabu vyote vinavyojihusisha na jogging wilaya ya Kinondoni na kuunda umoja na uongozi wa chama cha jogging.
Afisa Ushirika Manispaa ya Kinondoni (mwenye shati jeusi) akisalimiana na viongozi
Mwishoni kabisa katika majumuisho yake, msajili aliahidi kushirikiana na uongozi utakaoundwa na kutoa mwongozo wa namna ya kuunda chama hicho wakati wowote atakapohitajika kufanya hivyo, vile vile aliwaasa viongozi waliomtembelea kusambaza taarifa kwa vilabu vingine ili navyo viweze kushiriki kikamilifu.
Baadhi ya viongozi wa vilabu vya jogging katika picha ya pamoja - kutoka kushoto Jumanne Mrimi (Msajili), Abdul Mollel, David Mwaka, Mohamed Risasi, Andrew Mangole, Khadija Mabrouk, Alhaj Seif Mukhere
 

No comments:

Post a Comment