Mwezi disemba ndio umeingia. Katika mfumo wa kupeana taarifa mbalimbali
zinazohusu klabu zetu zinazojihusisha na mchezo wa mbio za pole pole (jogging),
katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi disemba kuna matukio kadhaa
yaliloyofanyika na yatakayofanyika. Kama ilivyo ada, klabu ya michezo ya
Biafra ilijumuika pamoja na klabu ya Namanga katika na kufanya mazoezi
ya pamoja jumapili ya tarehe 2 Disemba.
|
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ally Selemeani (mwenye bukta nyeusi) akiiwakilisha vyema Biafra |
Mazoezi hayo yaliyofanyika kuzunguka barabara na mitaa mbali ya Namanga na Msasani yalianzia na kumalizikia Leecars Pub ambapo ni makao makuu ya klabu ya Namanga. Mara baada ya mazoezi ya pamoja, wanamichezo wote walijumuika na kujadiliana machache kwa ajili ya maendeleo ya klabu zote ikiwemo pea kupashana taarifa mbalimbali.
Kule Magomeni nako, klabu za Mzimuni na Taifa Jogging zilikutana na kufanya mazoezi ya pamoja ya mbio za pole pole na kisha kucheza mechi za mpira wa miguu (wanaume) na mpira wa pete (wanawake). Picha zote za michezo kati ya Taifa na mzimuni Jogging ni kwa hisani ya Taifa Jogging.
|
Wana Taifa na Mzimuni Jogging kwenye mchakamchaka |
|
Kipindi cha mapumziko kwa mechi ya mpira wa miguu wanaume |
|
|
Wachezaji wa mpira wa pete kutoka Taifa Jogger katika picha ya pamoja |
Klabu ya michezo ya Namanga imejiandaa kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wake mnamo tarehe 9 Disemba, 2012. Akitoa taarifa ya kufanyika kwa mkutano huo mbele ya makatibu wa vilabu vya Biafra, Msasani na Kunduchi Kwanza, Katibu Mkuu wa Namanga ndugu Mangole alieleza kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Maandalizi ya mkutano huo yanaendelea. Alieleza kuwa vilabu rafiki vyote vitaalikwa kuhudhuria mkutano.
|
Mwenyekiti wa namanga Sports Club ndugu David Mwaka (aliyesimama) akichangia mada kwenye kikao cha maandalizi ya mkutano mkuu: Picha kwa hisani ya John Badi) |
Kwa habari zaidi kuhusu mkutano huo bofya hapa.
TUNAWATAKIA WANA NAMANGA MKUTANO MKUU WENYE MAFANIKIO
i like it this blog information
ReplyDelete