Sunday, March 11, 2012

TAREHE YA UCHAGUZI MKUU WA VIONGOZI YASOGEZWA MBELE HADI TAREHE 25 MACHI, 2012

Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Biafra anauwatangazia wanachama wote pamoja na umma kwa ujumla kwamba uchaguzi mkuu wa kwanza wa viongozi wa klabu hiyo ambao ulipangwa kufanyika mnamo tarehe 11 Machi, 2012 umehairishwa hadi tarehe 25 Machi, 2012. Kusogezwa mbele kwa uchaguzi kutaiwezesha klabu  kufanya semina ya uongozi kwa wagombea pamoja na wanachama wote kwa ujumla. Seimna hiyo imepangwa kufanyika tarehe 18 Machi, 2012. Mwezeshaji katika semina hiyo atakuwa ni mkurugenzi wa klabu ya Biafra pamoja na wawezeshaji wengine.

Kutoka kushoto Abdul Mollel (Mwenyekiti), Bethwelly Kyando (Katibu Mkuu Msaidizi), Yahya Poli (Katibu Mkuu)

2 comments:

  1. sawa ila naamini kwa kusogeza mbele siku ni katika kujiandaa kuchagua viongozi bora zaidi si bora viongozi

    ReplyDelete
  2. Kweli, nakubaliana na Anonymous hapo juu kwamba kusogezwa mbele kwa uchaguzi huo ni katika kuweka maandalizi sawa hasa napongeza uamuzi wa kutoa semina ya uongozi kwa wagombea na wanachama wote wa klabu. Mapendekezo, kwa teknolojia imekuwa kubwa, wekeni fomu za uanachama 'online' ili akina sisi pia tuzi-download.

    ReplyDelete