Siku ya jumapili tarehe 25 Machi, 2012 pale Leecars ambapo ni makao makuu ya klabu ya Michezo ya Namanga kuanzia saa 3 kamili asubuhi kutatolewa elimu na tiba bure ya ugonjwa wa kansa ya kibofu.
Picha ya kibofu kilichoathiriwa na saratani ya kibofu
Ila kukuarifu tu kidogo kuhusu saratani hiyo ni: -
- Saratani ya kibofu (Prostate Cancer) ni saratani inayoshambulia kibofu cha mkojo na mfumo mzima wa kukojoa
- Madhara yatokanayo na saratani hii ni; Upungufu wa damu mwilini, Kushindwa kuzuia mkojo na hivyo kujikojolea, Kupungua kwa tundu kwenye mrija wa kutolea mkojo (urethral stricture), Kuvimba kwa ureters kutokana na mkojo kushindwa kwenda kwenye kibofu cha mkojo.
- Kuna aina mbalimbali za saratani ya kibofu cha mkojo kama vile: transitional cell carcinoma, Squamous cell carcinoma na Adenocarcinoma,
- Dalili za saratani ya kibofu ni; Kukojoa damu (gross haematuria), Maumivu au kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation), Kuhisi bado hujamaliza mkojo baada ya kukojoa, kuhisi kukojoa lakini mkojo hautoki unapokojoa, maumivu ya tumbo,
- Watu walio kwenye hatari ya kupata saratani ya kibofu ni; Wale wanaofanyakazi kwenye saluni za nywele, Wanaofanya kazi ya kupaka rangi, Wafanyakazi wa viwanda vya nguo, Wanaofanya kazi kwenye viwanda vya ngozi, Wafanyakazi wa viwanda vya mipira (rubber), watu wanaofanya kazi zinazohusiana na kemikali moja kwa moja, watu wanaovuta sigara, madereva wa malori, n.k.
- Tiba ya saratani ya kibofu imegawanyika katika makundi manne; tiba ya mionzi, dawa, upasuaji na immunotherapy ama biological therapy.
No comments:
Post a Comment