Kipute cha kuanza kwa mikikimikiki ya hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya (UCL) 2012/13 kinaanza leo usiku majira ya saa 3:45 (kwa saa za afrika mashariki) wakati mwamuzi Wolfgang Stark kutoka nchini Ujerumani atakapopuliza kipyenga katika mechi inayowakutanisha wababe ambao ni vinara katika ligi za nchi zao Paris Saint German (PSG) watakapowakaribisha Barcelona (Barca) katika uwanja wa Parc des Princes ndani ya jiji la Paris na pia kutazamwa na mamilioni ya mashabiki wa soka duniani kote.
PSG ambao ndio wenyeji katika mpambano huo watakuwa wakiongozwa na kocha wao Carlo Ancelotti ambaye anatarajiwa kuchezesha kikosi chake mahiri kuanzia kwa mlinda mlango Sirigu; Jallet, Thiago Silva, Alex, Maxwell; Matuidi, Verratti; Moura, Lavezzi, Pastore; Ibrahimovic.
Silaha za maangamizi za PSG kutoka kushoto David Beckham, Jeremy Menez na Zlatan Ibrahimovic |
Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa saratani, kocha wa Barcelona, Tito Vilanova leo ataongoza benchi la ufundi la timu hiyo ambapo kikosi chake kinatarajiwa kuwajumuisha mlinda mlango Valdes; Alves, Mascherano, Pique, Alba; Xavi, Busquets, Iniesta; Sanchez, Messi na Villa. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, mshambuliaji wa timu hiyo David Villa (pichani chini) alisisitiza kutorudia kosa walilofanya Milan.
Wakati huo huo katika uwanja wa Allianz-Arena uliopo mjini Munich, Ujerumani, Bayern Munich wataikaribisha Juventus ya Italia katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa robo fainali ya michuano ya ligi ya klabu bingwa ulaya. Mtanange huo unatarajiwa kuchezeshwa na mwamuzi kutoka nchini Uingereza Mark Clattenburg. Kocha wa Bayern Munich - Jupp Heynckes (pichani chini) akizungumza na wandishi wa habari alitanabaisha kwamba wachezaji wote wako tayari kwa mechi hiyo na wana ari kubwa ya ushindi.
Kocha wa Bayern Munich - Jupp Heynckes |
Heynckes anatarajiwa kuwachezesha Manuel Neuer, Dante, Jerome Boateng, Daniel Van Buyten, Philip Lamn,
Holger Badstuber, Franck Ribery, Arjen Robben, Thomas Muller, Bastian
Schweinsteiger na Mario Mandzukic katika kikosi cha kwanza.
Antonio Conte (pichani chini) kocha wa Juventus akiizungumzia mechi hiyo aliwaonya wenyeji wao kwa kuwaarifu kuwa wanakwenda Munich wakiwa tayari wanahisi ni majeruhi na wanachofuata ni ushindi wakiwa ugenini.
Antonio Conte |
Conte anatarajiwa kuchezesha kikosi chake hatari cha maangamizi ambacho kinaongozwa na Gianluigi Buffon, Giorgio Chiellini, Martin Caceres, Leonardo Bonucci,
Andrea Barzagli, Andrea Pirlo, Sebastian Giovinco, Kwadwo Asamoah,
Arturo Vidal, Claudio Marchisco and Mirko Vucinic.
Picha zote zimepakuliwa toka vyanzo mbalimbali mtandaoni.
No comments:
Post a Comment