Ile mechi iliyohairishwa kwa zaidi ya mara tatu kati ya Biafra Kids aka The Juniors dhidi ya Mchangani FC hatimaye imechezwa jana jumapili tarehe 04 Mei, 2012 saa 4:30 asubuhi katika uwanja wa Mwl. Nyerere, magomeni Makurumla.
The Juniorz wakipasha misuli kabla ya kuingia uwanjani
The Juniorz wakisalimiana na wachezaji wa Mchangani FC kabla ya kuanza kwa mechi
Mechi ilichelewa kuanza kwa takribani nusu mara baada ya kukosekana kwa mpira. Si waandaaji, Mchangani FC wala BIafra Kids waliokuwa na mpira hali iliyosababisha uazimwe mpira ambao haukuwa na bora kwa ajili ya kuchezewa mechi.
Kikosi kilichoanza cha The Juniorz
Kikosi kilichoanza cha Mchangani FC
Baada ya kupulizwa kipenga hca kuashiria kuanza kwa mechi hiyo, The Juniorz walilishambulia lango la Mchangani na kukosa magoli mawili mapema tu dakika ya 8 na ya 17. Kosa kosa hizo zilitokana na ubovu wa mpira. Pamoja na ubovu wa mpira huo, vijana walijitahidi kucheza kandanda safi hadi dakika ya 27 walipopachika bao la kwanza kupitia kwa Babulu Nusura baada ya kupokea krosi safi ya Abu Selemani. Bao hilo liliwaamsha vijana wa Mchangani ambao waliokuwa wakisaidiwa na upepo na hatimaye mnamo dakika ya 42 wakajipatia bao la kusawazisha. Hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1 -1.
The Juniorz wakiwa katika mapumziko
Wakati wa mapumziko ulikuwa ni wakati muafaka kwa vijana kupata ushauri na kurekebisha makosa mawili yaliyojitokeza kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kusomana mchezo na pia kujaribu kuona namna wanavyoweza kukutumia mpira mbovu. hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa timu hizo ziligawana pointi kwa kutoka sare ya 1 - 1. Matokeo hayo yamewaweka The Juniorz katika nafasi ya pili ya msimao huo wakiwa na pointi 4 na magoli 6.
The Juniorz wakitoka uwanjani
Wakizungumza baada ya mechi hiyo, wachezaji wote walisikitishwa sana na matokeo ya mechi hiyo kwa kuwa timu waliyocheza nayo haikuwa imejiandaa vyema isipokuwa mpira uliotumika ndio ulisababisha wasipate ushindi mnono hiyo ni kwa sababu kadri muda ulivyozidi kwenda ndio mpira ulivyozidi kuharibika. Hivyo basi walitumia pia fursa hiyo kuwaomba wapenda michezo kwa ujumla kuwasaidia mipira na vifaa vya michezo kwa ujumla ili waweze kushiriki mashindano hayo vizuri na pia kulitwaa kombe hilo.
NA SISI VIONGOZI KWA NIABA YA VIJANA HAWA, TUNAWAOMBA WADAU WOTE KUWAWEZESHA VIJANA HAWA VIFAA VYA MICHEZO KWA KADRI YA UWEZO WENU ILI WATIMIZE NDOTO ZAO ZA KUCHEZA SOKA NA KULISAIDIA TAIFA!!!
Kwa msaada, wasiliana na;
Katibu Mkuu,
Biafra Sports Club (Namba ya Usajili NSC. 9848)
Simu: +255 715 253 653,
Barua pepe: biafra.jsclub@gmail.com
Ukurasa wa Facebook: facebook.com/BiafraKidsAkaTheJuniorz
TUNAKUSHUKURU SANA!!!
No comments:
Post a Comment