Katika kusherehekea siku ya kina mama duniani (mother's day) leo, timu ya Biafra Kids almaarufu The Juniors wameichapa timu ngumu ya Vijana Muslim almaarufu 'dume' kwa mabao 2 -1 bila huruma katika michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17 kanda ya Kinondoni.
The Jrz wakipasha misuli moto kabla ya kuingia uwanjani.
Vijana Muslim nao wakipasha moto misuli kabla ya kuingia uwanjani
Dume ni moja kati ya timu zinazohofiwa sana kwenye michuano hiyo kwa kuwa ni timu yenye uzoefu wa kushiriki mashindano mbalimbali kwa muda mrefu huku The Juniorz wakiwa wageni kabisa kwenye mashindano hayo hali iliyopelekea mashabiki wengi kuipa nafasi kubwa timu ya Dume lakini katika hali ya kushangaza, The Juniorz waliwafundisha mpira Dume.
Kikosi kilichoanza - The Juniorz
Kikosi kilichoanza - Vijana Muslim
Baada ya kutandaza kandanda safi tangu sekunde ya kwanza ya mchezo, Biafra Kids walijiandikia bao la kwanza dakika ya 28 kupitia kwa winga wake machachari Babulu Nussura. Hadi mapumziko Biafra Kids walikuwa wakiongoza kwa bao 1.
Kiongozi wa Dume akiwa na majonzi ya kufungwa timu yake
Mchezo huo ambao pia ulishuhudiwa na wanasoka mbalimbali wa zamani (pichani chini) uliendelea tena kipindi cha pili ambapo timu ya Dume walijipatia bao la kusawazisha lilioleta utata ambapo wengi miongoni mwa watazamaji walilisisitiza kuwa mchezaji aliyefunga goli la Dume alikuwa ameotea na alionekana wazi kabisa kuwa ameotea. hata hivyo, The Juniorz hawakukata tamaa kabisa kwani pamoja na kuchezewa rafu nyingi hatimae waliandika bao la pili kwa njia ya penalti dakika ya 87 baada ya golikipa wa timu ya Dume kumchezea rafu mbaya kiungo machachari wa The Juniorz Hussein Tahiddin kwenye eneo la hatari. Penati hiyo iliwekwa kimiani na Rashid Sajji.
Golikipa wa zamani
Hadi mwisho wa mchezo Biafra Kids iliibuka kidedea na ushindi wa mabao 2 -1 wakiwa na pointi saba na magoli 8. Timu hiyo inarudi tena uwanjani jumatano tarehe 16 Mei, 2012 ambapo itacheza na timu ya Hanasif mchezo ambao utapigwa katika dimba la shule ya sekondari ya Muslim ambao ni uwanja wa nyumbani wa Dume.
No comments:
Post a Comment