Kama ilivyo ada, kila siku ya jumapili, wanachama wa Biafra pamoja na wadau wote wanaopenda kufanya mazoezi ya mbio za pole pole hukutana na kufanya mazoezi hayo kwa pamoja. Kwa kawaida mazoezi huanzia na kuishia makao makuu ya klabu pale 90 Degrees Pub Kinondoni. Akizungumza na wanachama pamoja na wadau, Katibu Mkuu wa Biafra ndugu Yahya Poli kwa niaba ya Kamati ya Ufundi, alitangaza njia zitakazotumika kwa ajili ya mazoezi ya mbio za pole pole zitakazofanyika jumapili tarehe 13 Mei, 2012 kuanzia saa 12:30 asubuhi.
Wanabiafra wakikatiza barabara ya Ali Hassan Mwinyi
Katibu Mkuu huyo alibainisha kwamba, wanachama pamoja na wadau wote wanatakiwa kuwa klabuni kabla ya saa 12:25 asubuhi na itakapotimu saa 12:30 mazoezi yataanza moja kwa moja kwa kupitia barabara ya Kawawa kuelekea Moroko, kisha wakimbiaji wataingia barabara ya Ali Hassan Mwinyi mpaka njia panda ya kuelekea Leaders Club, wataifuata barabara hiyo hadi makutano ya barabara ya Kinondoni kuelekea shule ya sekondari Muslim, kisha watakatiza barabara ya kuelekea stereo kupitia kanisa la Pinda hadi studio. Baada ya kufika studio, wanabiafra wataifuata barabara ya Kawawa kuelekea mkwajuni hadi chuo cha Baraka na kukatiza maeneo ya Mango Garden hadi kwa Manyanya na kumalizia mbio klabuni.
Wanabiafra wakiingia barabara ya Kawawa
Akiongezea, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ndugu Michael Silili (pichani chini) alitanabaisha kwamba ruti hiyo inaweza kuwachukua wakimbiaji takriban dakika tisini kuimaliza hivyo amewasisitizia wanamzoezi wote kuwahi mapema.
Wenyeviti - Michael Silili Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Klabu Abdul Mollel
Mwenyekiti wa klabu ndugu Abdul Mollel kwa kumalizia aliwakaribisha watu wote wenye kupenda kufanya mazoezi ya mbio za pole pole kujumuika pamoja na wanachama kila jumapili na pia watumie fursa hiyo kuielewa klabu na hatimaye wajiunge na kuwa wanachama. Aliendelea kubainisha kuwa, kwa yeyote atakayependa kufanya hivyo basi awasiliane moja kwa moja na Katibu kwa simu (0715 253 653)
WE! WE! MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!!!!!!!!!!
No comments:
Post a Comment