Tuesday, July 17, 2012

KATIBU WA KAMATI YA UFUNDI YA BIAFRA AFUNGA NDOA!!!

Siku jumamosi tarehe 14 Julai, 2012 ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa mwanabiafra Ally Juma ambaye ni katibu wa Kamati ya Ufundi ya klabu hiyo baada ya kufunga ndoa na Bi Zahra Iddi. Ndoa hiyo ilifungwa nyumbani kwa familia ya bi harusi Tegeta Msikitini na sherehe iliyofana kufanyika katika ukumbi wa 90 Degrees Pub ambako ni makao makuu ya klabu ya michezo ya Biafra.

Bwana na Bi harusi baada ya kuingia ukumbini wakiwa pamoja na wapambe wao

Baadhi ya wanabiafra wakiongozwa na makamu mwenyekiti Jackline Barozi (mwenye gauni jeusi)

Katibu wa Biafra Kaka Poli akiwakaribisha wageni ukumbini pembeni ni MC wa sherehe hiyo

Bwana harusi ambaye ni katibu wa kamati ya ufundi ya klabu akimtambulisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo ndugu Michael Silili 

Maharusi wakilishana keki 


Mwenyekiti wa Biafra Abdul A. Mollel akila keki kwa niaba ya klabu 

Wanabiafra wakijadiliana
Wanabiafra waliohudhuria sherehe hiyo wakiongozwa na Katibu Kaka Poli

Baadhi ya wageni waalikwa

Kwa niaba ya wanachama, viongozi, mashabiki na wadau wote, klabu inatoa pongezi za dhati kwa maharusi na kuwaoombea mwenyezimungu aibariki ndoa yao.



Thursday, July 12, 2012

BIAFRA DAY 2012 YASOGEZWA HADI SEPTEMBA KUPISHA ZOEZI LA SENSA YA WATU

Katibu Mkuu wa klabu ya michezo ya Biafra ndugu Yahya Poli ameutangazia umma kwamba BIAFRA DAY 2012 ambayo awali ilipangwa kufanyika tarehe 26 Agosti, 2012 sasa imesogezwa mbele hadi tarehe 2 Septemba, 2012. Kusogezwa huko mbele kwa juma moja kumetokana na siku ya awali tarehe 26 Agosti, 2012 itakuwa ni siku maalum ya Sensa ya watu na makazi nchini Tanzania.
Wanabiafra wakikatiza eneo la daraja la salender wakiwa kwenye mazoezi ya mbio za polepole


Akielezea zaidi, ndugu Poli alitanabaisha kwamba mipango ya kufanikisha BIAFRA DAY 2012 bado inaendelea na kuwakaribisha wadau wote ambao wangependa kushiriki siku hiyo kwa ufadhili na udhamini wasisite kuwasiliana na viongozi wa klabu kwa kuwa fursa bado ipo. Pia alitoa msisitizo kwa kamati zote za klabu kukutana kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya BIAFRA DAY, 2012. 
BIAFRA DAY 2011 - Wanabiafra wakishindana kuvuta kamba



  

Thursday, July 05, 2012

BIAFRA DAY 2012 YAPANGWA KUFANYIKA MWEZI WA NANE

Kama ilivyo ada, kila mwaka tangu kuanzishwa kwake, klabu ya michezo ya Biafra hutenga siku maalum ambayo hujulikana kama BIAFRA DAY kwa ajili ya kujumuika pamoja na wadau wake wote kwa ajili ya michezo na shughuli nyingine mbalimbali. Mwaka huu 2012,  BIAFRA DAY imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam.
Wanabiafra katika picha ya pamoja ndani ya DarLive Mbagala

BIAFRA DAY 2012 itaanza rasmi saa kumi na mbili asubuhi na kumalizika saa moja usiku ambapo wanamichezo na wadau wengine wote watajumuika pamoja kwa mbio za pole pole jogging ambaazo zitaanzia katika viwanja vya Biafra na kuzunguka maeneo mbalimbali ya Kinondoni na hatimaye kumalizikia katika viwanja vya biafra. Akizungumzia matukio yatayofanyika siku hiyo, Katibu wa klabu ya Biafra alitanabaisha kwamba, mwaka huu Biafra Day inatarajiwa kuwa tofauti kwa kuongeza masuala mbalimbali kama vile huduma za upimaji wa virusi vya UKIMWI, kisukari, kansa, n.k. Michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, kukimbia na guni, kurusha mshale nayo pia itachezwa.
Wanabiafra wakishusha kilima cha Mbagala kuelekea Zakheem

Mwenyekiti wa klabu ya Biafra, Abdul Mollel akizungumzia maandalizi ya siku hiyo alitanabaisha kwamba, maandalizi yanaendelea, wanachama wamekuwa wakikutana mara mara katika kuhakikisha siku hiyo inafanyika kwa kadri ilivyopangwa.

Pia alitanabaisha kwamba, fursa ya kudhamini BIAFRA DAY 2012 ipo kwa  kampuni, mashirika au mtu binafsi hivyo aliwaomba wadau wote kujitokeza kwa wingi katika kuidhamini siku hiyo.
Baadhi ya washiriki wakielekea katika viwanja vya Biafra - BIAFRA DAY 2011

BIAFRA DAY 2011 - washiriki wakijiandaa kuanza mashindano ya mbio mita 100


KWA UDHAMINI:
WASILIANA NA:
0717 375375 (MWENYEKITI)
0719 947700 (MWEKA HAZINA)
0715 253 653 (KATIBU MKUU)

AU TUANDIKIE BARUA PEPE:



TANZIA: MWANABIAFRA ASHA YUSUF AFIWA NA BABA YAKE MZAZI LEO TAREHE 5 JULAI, 2012

Klabu ya michezo ya Biafra, kwa masikitiko makubwa inapenda kuwatangazia wanachama, wadau, mashabiki na wapenda michezo kwa ujumla kwamba mwanachama mwenzao ASHA YUSUPH (pichani chini) amefiwa na BABA YAKE MZAZI asubuhi ya leo tarehe 5 Julai, 2012 katika hospitali ya Mwananyamala.
ASHA YUSUPH (WA KWANZA KUSHOTO) AKIWA NA EDITHA TUNGARAZA NA NANCY RUPIA

Akizungumza na Katibu wa Biafra, Asha aliwaarifu wadau wote kwamba, msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu Kinondoni Shamba na mazishi yatafanyika kesho jioni huko shambani kwa marehemu Kongowe (mbagala) Dar es Salaam.
Asha Yusuf (wa tano toka kushoto waliosimama mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wanabiafra

Kwa niaba ya wanachama na wadau wote wa Biafra, mwenyekiti anatoa pole kwa mwanachama mwenzetu pamoja na ndugu, jamaa na rafiki zake kwa msiba huo na pia kuwaomba Wanabiafra wote kumfariji mwanachama mwenzao. Kwa mawasiliano, namba ya Asha Yusuph ni 0659327117.

Inna Lillahi - Wa Inna Ilaihi Raaji'un, Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa; Jina lake Lihimidiwe.

Tuesday, June 19, 2012

Monday, June 18, 2012

BIAFRA KIDS YAIZAMISHA TEMEKE KIDS KWA MABAO 3 - 0

Katika kujiweka fiti kwa ajili ya kushiriki michuano ya Winome mwezi Julai mwaka 2012, timu ya Biafra Kids ilichuana na Temeke Kids katika uwanja wa Zakheem Mbagala. Mechi hiyo iliyochezwa majira ya saa sita mchana ilishuhudiwa na watazamaji zaidi ya mia tano ambao ni wanamichezo kutoka katika vilabu mbalimbali vya michezo mkoani Dar es Salaam.

Kikosi kazi cha Biafra Kids




Mchezaji wa Soka Aziza (Biafra Ladies) mwenye suruali nyeusi akifuatilia mechi kwa makini


Biafra Kids wakitoka uwanjani kwa mapumziko

Pamoja na uwanja kuwa na michanga mingi, vijana walionyesha kandanda safi kiasi cha kushangiliwa muda wote na hadi mpira unakwisha Biafra Kids walikuwa washindi wa mechi hiyo kwa mabao 3 - 0.



VILABU KADHA VYA 'JOGGING' MKOA WA DAR ES SALAAM VYAKUTANA NA KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NA TEMEKE JOGGING

Jumapili ya tarehe 17 Juni, 2012 ilikuwa ni siku njema kwa wanamichezo katika mkoa wa Dar es Salaam. Vilabu zaidi ya 15 vya michezo, hasa vinavyohamasisha mchezo wa mbio za pole pole "jogging" vilifanya mazoezi ya pamoja kwa mwaliko wa klabu kongwe ya Temeke. Wanamichezo zaidi ya mia sita walikusanyika katika uwanja wa Taifa na saa 12:30 asubuhi walianza safari ya kuelekea Mbagala katika ukumbi wa Dar-Live kisha katika viwanja vya Zakheem kwa mchezo wa mpira wa miguu.
Biafra Jogger wakiongoza msafara wa wana-jogger


Biafra Kids wakiongoza Biafra Jogger








Baadhi ya wanakunduchi Kwanza





Makamu Mwenyekiti wa Biafra Ms. Jacqueline Barozi akiingia Darlive



Mwenyekiti wa Biafra (mwenye bukta ya bluu) akishiriki aerobics



Wanabiafra walioshiriki mazoezi katika picha ya pamoja ndani ya Darlive Mbagala


Monday, June 11, 2012

Songs makes jogging fun!!

Joggers

BIAFRA JOGGING NDANI YA JEZI MPYA YAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NA NAMANGA NA KUNDUCHI KWANZA

Klabu ya michezo ya Biafra imezindua awamu ya kwanza ya uzinduzi wa jezi za mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) kwa kufanya mazoezi ya pamoja na klabu za Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Jogging.
Wadada wa Biafra Jogging waking'aa ndani ya 'uzi' mpya



Jezi mpya ya Biafra Jogging inavyoonekana kwa nyuma

Wanamichezo wakikatiza maeneo ya polisi Oysterbay

Mazoezi hayo yaliyofanyika jana jumapili tarehe 10 Juni, 2011 yalianzia na kuishia katika klabu ya Namanga na wanamichezo walikimbia zaidi ya kilomita 8 kwa kupitia barabara za old Bagamoyo na Ali Hassan Mwinyi (Namanga, Oysterbay Polisi, Drive -Inn, Moroko, Viktoria, Sayansi, Rose Garden, Kwa Nyerere, Chama, Drive-Inn, Oysterbay Polisi na Namanga).







Wadada wa Kunduchi Kwanza waking'aa pia na uzi wao


Viongozi wa klabu zote 3 walikutana




MATUKIO KATIKA MECHI YA BIFRA KIDS DHIDI YA KOMBAINI YA KINONDONI

Katika kujiimarisha zaidi na kuongeza uzoefu wa mechi ngumu, timu ya Biafra Kids ilipokea na kukubali mwaliko wa kucheza na timu ya kombaini ya mkoa wa Kinondoni ambao wameteuliwa kutoka katika timu mbalimbali zilizoshiriki michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17 kanda ya Kinondoni. Mechi hiyo iliyochezwa katika viwanja vya Tanganyiksa Packers Kawe, siku ya J'mosi tare 9 Juni, 2012 illisha kwa Biafra Kids kupoteza mchezo huo baada ya kufungwa mabao 2 - 1.
KIKOSI CHA BIAFRA KIDS

KOMBAINI YA KINONDONI






Kocha wa Biafra Kids William Masika (kushoto) akiwa na viongozi wa Kombaini


Tuesday, June 05, 2012

BIAFRA KIDS PLAYER OF THE WEEK 4 - 10 JUNE, 2012

From this week on, we'll be presenting you the club's player of the week. The said players is chosen by the players themselves, trainers and team captains. in order for the player to be selected a player of the week, he must demonstrate highest state of discipline on and off the field, follow and keep the instructions given by the trainers, demonstrate the ability and agility of playing footbal, e.t.c.
Players and leaders of Biafra Kids 

And, the player for this week (4th - 10th June, 2012) is Ahmed Suleiman (pictured below). He joined the club in 2011. Ahmed is 16 years old studying at Hanasif Secondary School Form II. He is mong the players club enrolled in Copa Coca Cola under 17 tournament for Kinondoni Zone. His teammates calls him Mafisango because his kind of play resembles the late player who played for Simba 2011/12 season.