Tuesday, April 10, 2012

FURAHA NGANDA ASHINDA PAMBANO LAKE DHIDI YA JAMHURI SAIDI TAREHE 8 APRILI, 2012

"Nimefurahi sana kwa ushindi huu, nilimwambia Jamhuri (Said) ajiandae vya kutosha, hakunielewa, alifikiri namtania, sasa nimemuonesha kuwa mimi si wa kawaida, si wale wale, hapa kazi tu". Hayo ni maneno ya Mwanamasumbwi Furaha Nganda mara baada ya kumaliza pambano lake na bondia machachari Jamhuri Saidi katika ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Furaha Nganda (mwenye bukta ya bluu akimsukumia konde zito Jamhuri Said (Picha zote kwa hisani ya Super D)


Mpambano kati ya mabondia hao ulikuwa ni wa utangulizi ambapo pambano lenyewe hasa liliwakutanisha mabondia Rashid Matumla (Snake Boy) dhidi ya Manano Oswald (Mtambo wa Gongo) ambapo Maneno Oswald alishinda pambano hilo na kunyakua ngao ya pasaka. kwa matokeo ya mpambano huo na mapambano mengineyo duniani tembelea tovuti ya Boxing Records.

Viongozi na wanachama wote wa Biafra Sports Club wanampongeza Mwanabiafra mwenzao Furaha Nganda kwa ushindi huo na kumsisitiza aongeze bidii kwenye mazoezi na kutunza afya yake! 

2 comments:

  1. hongera sana dada furaha naamini hilo ni jambo zuri kwako na hata katika club yako ya mazoezi ya biafra

    ReplyDelete
  2. Nami nampongeza sana Furaha Nganda. Wanabiafra tumpe mkono wa pongezi mwenzetu tafadhali!

    ReplyDelete