Thursday, July 05, 2012

BIAFRA DAY 2012 YAPANGWA KUFANYIKA MWEZI WA NANE

Kama ilivyo ada, kila mwaka tangu kuanzishwa kwake, klabu ya michezo ya Biafra hutenga siku maalum ambayo hujulikana kama BIAFRA DAY kwa ajili ya kujumuika pamoja na wadau wake wote kwa ajili ya michezo na shughuli nyingine mbalimbali. Mwaka huu 2012,  BIAFRA DAY imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam.
Wanabiafra katika picha ya pamoja ndani ya DarLive Mbagala

BIAFRA DAY 2012 itaanza rasmi saa kumi na mbili asubuhi na kumalizika saa moja usiku ambapo wanamichezo na wadau wengine wote watajumuika pamoja kwa mbio za pole pole jogging ambaazo zitaanzia katika viwanja vya Biafra na kuzunguka maeneo mbalimbali ya Kinondoni na hatimaye kumalizikia katika viwanja vya biafra. Akizungumzia matukio yatayofanyika siku hiyo, Katibu wa klabu ya Biafra alitanabaisha kwamba, mwaka huu Biafra Day inatarajiwa kuwa tofauti kwa kuongeza masuala mbalimbali kama vile huduma za upimaji wa virusi vya UKIMWI, kisukari, kansa, n.k. Michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, kukimbia na guni, kurusha mshale nayo pia itachezwa.
Wanabiafra wakishusha kilima cha Mbagala kuelekea Zakheem

Mwenyekiti wa klabu ya Biafra, Abdul Mollel akizungumzia maandalizi ya siku hiyo alitanabaisha kwamba, maandalizi yanaendelea, wanachama wamekuwa wakikutana mara mara katika kuhakikisha siku hiyo inafanyika kwa kadri ilivyopangwa.

Pia alitanabaisha kwamba, fursa ya kudhamini BIAFRA DAY 2012 ipo kwa  kampuni, mashirika au mtu binafsi hivyo aliwaomba wadau wote kujitokeza kwa wingi katika kuidhamini siku hiyo.
Baadhi ya washiriki wakielekea katika viwanja vya Biafra - BIAFRA DAY 2011

BIAFRA DAY 2011 - washiriki wakijiandaa kuanza mashindano ya mbio mita 100


KWA UDHAMINI:
WASILIANA NA:
0717 375375 (MWENYEKITI)
0719 947700 (MWEKA HAZINA)
0715 253 653 (KATIBU MKUU)

AU TUANDIKIE BARUA PEPE:



No comments:

Post a Comment