Thursday, July 19, 2012

BIAFRA SPORTS CLUB YAWATAKIA WAISLAM WOTE HERI YA MFUNGO WA RAMADHANI

Kwa niaba ya wanachama, wadau na mashabiki wa Biafra, mwenyekiti wa klabu hiyo ndugu Abdul Ahmad Mollel amewatakia waisalamu nchini na duniani kwa ujumla heri ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao unatarajiwa kuanza Ijumaa tarehe 20 Julai, 2012. Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa watu wote wanaoshiriki mfungo wa Ramadhan na wasioshiriki pia kutumia kipindi hiki katika kutenda yale yote mema ambayo yatupasa kutenda ikiwemo kufanya ibada, kutoa sadaka, kuwajali wasio na uwezo hasa yatima na wajane.
Baadhi ya watoto kutoka katika kituo cha Hananasif

Kwa wanabiafra, mwenyekiti aliwakumbusha kuwa wakati wa Ramadhan wanachama wataendelea na mazoezi kwa wale wenye kupenda kwa kuwa kufanya mazoezi ni jambo muhimu katika kujenga afya za watu. Hivyo basi, alitoa rai kwa wanachama wote ambao wangependa kufanya mazoezi wanakaribishwa.
Baadhi ya wachezaji wa Biafra Kids wakijipatia mlo wa Idd pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu 2011


No comments:

Post a Comment