Monday, July 29, 2013

WANA-JOGGING WAJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MSIBA WA MTOTO WA MAKAMU M/KITI WA MZIMUNI JOGGING

Tasnia ya mchezo wa mbio za pole pole (jogging) ilikumbwa na huzuni kwa mara nyingine tena baada ya kupata msiba ambapo Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Jogging ya Mzimuni bwana Abbas Said almaarufu China amefiwa na mtoto wake aliyekuwa akiitwa Aboubaka tarehe 27 Julai, 2013 na kuzikwa tarehe 28 Julai, 2013 katika makaburi ya Kimamba Magomeni Mwembechai Dar es Salaam. Wadau wambalimbali wa mchezo wa mbio za pole pole walikuwa ni miongoni mwa walioshiriki katika msiba huo na kumfariji mwanamichezo mwenzetu. Fuatilia matukio mbalimbali ya msiba huo katika picha. 
Wanamichezo wakiwasili msibani majira ya saa 4 asubuhi.


Jeneza lenye mwili wa marehemu


Mwili wa marehemu ukiwasili makaburini tayari kwa mazishi
Mwenyekiti wa Kopa Original Jogging bwana Mustafa (mwenye suruali nyeupe)
Shughuli za mazishi zikiendelea
Wanabiafra Aly Juma (kushoto) na Ally Masharubu wakiwa makaburini
Baada ya kutoka makaburini wadau wote tulirejea nyumbani kwa marehemu na kuendelea na itifaki nyingine ikiwemo kukusanya rambirambi pamoja na kupanga mipango mingine ya mazishi kama vile arobaini, n.k. 











































Katibu Mkuu wa Mzimuni Jogging bwana Aboubakar Kabambura akifanya majumuisho ya rambirambi zilizkusanywa toka katika  vilabu vya jogging vilivyohudhuria msibani
Mfiwa akitoa neno la shukrani kwa wanamichezo wote walioweza kuhudhuria msiba wa mwanae

Akipoke mkono wa pole



"Nimefarijika sana kuona umati wa wana-jogging, sikutarajia, tuudumishe na kuuenzi umoja huu" ni maneno aliyoyasema mfiwa kumwambia Katibu wa Biafra Sports Club na Chama cha Jogging Kinondoni (pichani) wakati akiagana na wana-jogging

Safari ya kurejea nyumbani baada ya mazishi

MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI! AMEN

UMOJA NDIO NGUVU TULIYONAYO WANA-JOGGING!!

No comments:

Post a Comment