Wanabiafra leo tarehe 28 Julai, 2013 walijitokeza kwa wingi na kushiriki mazoezi ya mbio za pole pole ambayo yalianzia klabuni, mtaa wa Isere, Kinondoni kisha kuingia barabara ya Kawawa hadi kwenye makutano ya barabara ya Kawawa na Kinondoni, kupitia shule ya sekondari ya Muslim, mwembejini, kona ya tazara mpaka kwenye mataa ya salenda kuelekea barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuelekea sea view na hadi katika fukwe za Agha Khan ambapo walifanya mazoezi ya viungo kwa jumla na hatimaye kurejea klabuni kwa mchakamchaka kupitia barabara zilezile walizotumia. Fuatilia matukio yote katika picha.
|
Tukiingia barabara ya Kawawa kutokea klabuni |
|
Watoto wakiimba kwa shangwe na hamasa |
Tulipofika maeneo ya Manyanya, tulikutana na klabu ya Kopa Original upande wa pili wa barabara kuelekea Moroko ambapo Katibu Mkuu alijumuika nao kuwaunga mkono na kuwasalimia.
|
Katibu Mkuu wa Biafra akivuka barabara kuwasalimia Kopa Original Jogging |
|
|
M/Kiti wa Biafra - Abdul Mollel Akiimbisha |
|
Maeneo ya makaburini tukielekea shule ya sekondari Muslim |
|
Wale wa mwisho mwisho |
|
Waongozaji wetu Ally Juma ambaye pia ni katibu wa kamati ya ufundi ya Biafra (mwenye tracksuit nyekundu) na Khamis Magodoro (mwenye kizibao) wakituongoza kuingi barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwenye mataa ya Salendar Bridge |
|
Tukiingia Barabara ya Ali Hassan mwinyi |
|
Tukikatiza maeneo ya Seaview |
Mara
|
Tukiingia katika fukwe za Agha Khan/Gymkhana |
|
Mduara wa mazoezi ya viungo |
|
Katibu katika vita dhidi ya kitambi |
Mara baada ya mazeozi ya viungo ya pamoja na binafsi, tulipata fursa ya kupiga picha ya pamoja ya wanabiafra wote walioshiriki mazeozi kisha safari ya kirudi klabuni ikaanza.
|
Picha ya pamoja |
|
Safari ya kurudi klabuni |
|
Mollel akiimbisha kwa mzuka |
|
Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Mipango Robert Mwakibugi (mwenye bukta ya bluu akionesha ukakamavu |
|
Tukiwa klabuni baada ya kumaliza mbio |
Tunatoa shukrani za dhati kwa jeshi la polisi, idara ya usalama barabarani kwa kuwa wamekuwa wakituonesha ushirikiano wa hali ya juu kila tunapofanya mazoezi ya mbio za pole pole siku za jumapili, mara zote wamekuwa wakituongoza vizuri na kuonesha utayari wa kutusaidia tunapoomba msaada wao.
MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!
No comments:
Post a Comment