Kama ilivyo ada, jumapili hii wanabiafra walikutana tena katika mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambazo zilikutanisha pamoja na marafiki zao wa Namanga Jogging katika fukwe za Coco, Dar es Salaam. Fuatilia matukio ya siku hiyo katika picha.
|
Wanabiafra waliowahi mapema klabuni wakijiandaa kuondoka |
|
Msafara ukingia barabara ya kuelekea ada estate |
|
Tukiingia barabara ya Best-Bite |
|
Tukiingia barabara ya Ally Hassan Mwinyi kuelekea Namanga |
|
Tlikutana na Vegas Jogging kwenye kona ya kuelekea Namanga wao wakielekea barabara ya A.H.Mwinyi |
|
Tukiingia fukwe za coco |
|
Namanga Jogging wakifanya mazoezi ndani ya Coco Beach wakiongozwa na Michael Juma (Mopao) |
|
Biafra waliungana na Namanga na kuendelea na mazoezi ya ufukweni |
|
Baadhi ya wanabiafra katika picha ya pamoja |
|
Watoto wa Biafra pichani |
|
Katibu akiwa pamoja na watoto |
|
Mwanabiafra Ayoub Layson |
Mara baada ya mazoezi ya nguvu ya ufukweni kwa pamoja na wana namanga Jogging tulianza safari ya kurejea kwenye ngome zetu kwa mbio za pole pole.
|
Tukijipanga tayari kuanza safari ya kurudi baada ya mazoezi ya ufukweni |
|
Wakati sisi tunarudi wengine ndio walikuwa wanaenda |
|
Tukielekea barabara ya CCBRT |
|
Tukishusha kilima cha CCBRT |
|
Tukipandisha kilima cha CCBRT kuelekea barabara ya Namanga |
|
Barabara ya Namanga |
|
Hapa ni karibu kabisa na Leecaz ambako ni makao makuu ya Namanga Jogging na waliishia hapo sisi tukaendelea na safari ya kurudi klabuni |
|
Barabara ya Best-Bite |
|
|
Tukielekea klabuni |
|
Utamu wa mazoezi ya viungo |
|
Tukiwa kwenye kikao |
Mara baada ya mazoezi, katika kikao chetu cha kawaida, tuliamua kwa pamoja kuwa jumapili ya tarehe 28 Julai, tutafanya mazoezi ya mbio za pole pole kuanzia klabuni hadi fukwe za Agha Khan kupitia barabara ya Kinondoni, Salendar na Seaview. Tunawakaribisha wote!
MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!!!!
No comments:
Post a Comment