Thursday, July 11, 2013

UKOSEFU WA VIWANJA VYA MICHEZO NI KIKWAZO KATIKA MAENDELEO YA MICHEZO

Ukosefu wa viwanja vya michezo ni kikwazo katika kufikia maendeleo tarajiwa ya soka. Katika eneo la Kinondoni, uwanja maarufu sana wa Biafra unaelekea kupotea baada ya kuingiliwa na shughuli mbalimbali ambazo hazihusiani kabisa na michezo ikiwemo kuosha na kupaki magari, n.k. Hali hiyo imeufanya uwanja kuwa hifadhi ya vifusi vinavyotokana na ujenzi wa barabara katika maeneo ya Kinondoni.


Ufinyu wa nafasi katika uwanja huo unasababisha timu mbalimbali kushindwa kufanya mazoezi hali inayosababisha wachezaji wenye umri tofauti kufanya mazoezi kwa pamoja.


Baada ya kuliona hilo, uongozi wa klabu ya michezo ya Biafra uliamua kuomba kuutumia uwanja wa shule ya sekondari ya Oysterbay kwa ajili ya mazoezi ya timu yake ya vijana #BYFT. 
Wachezaji wa #BYFT


No comments:

Post a Comment