Sunday, July 14, 2013

MBIO MAALUM ZA KUMUENZI MWANABIAFRA MAREHEMU ABOUBAKAR IDDI MAGANGA ZAFANYIKA TAR 14 JULAI, 2013

Katika harakati za kumuenzi mwanachama wa klabu ya michezo ya Biafra, marehemu Abubakar Iddi Maganga aliyefariki tar 7 Julai, 2013 na kuzikwa tarehe 8 Julai, 2013 wanabiafra waliamua kufanya mazoezi ambayo yatakuwa rasmi kwa ajili ya kumuenzi, mazoezi hayo yalipangwa kufanyika tarehe 14 julai, 2013 yalianzia Makao Makuu ya klabu ya Michezo ya Biafra na kuishia nyumbani kwao marehemu ambapo wazazi wake ndugu Iddi Maganga ambaye ni mwanachama pia mjumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na mkewe almaarufu mama Aboubakar pamoja na familia nzima walitupokea. Fuatilia picha za tukio hilo hapa chini.
Wanabiafra wakipita barabara ya Mwananyamala hospitali




Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (mwenye kiremba) akiimbisha

Mwananyamala Jogging pamoja na Ungaunga Jogging tulipishana nao maeneo ya Mwananyamala



Khamis almaarufu magodoro (mwenye miwani) akiimbisha kwa mbwembwe


Wanabiafra wakikatiza barabara ya Kwa kopa - Mwanayamala




ko





Baada ya kuwasili nyumbani kwa bwana Iddi Maganga waliendelea na zoezi la 'aerobics'





Tulikaribishwa rasmi baada ya mazoezi ya aerobics.
Baba wa marehemu Aboubakar Idd Mganga bwana Idd Maganga (mwenye kanzu) akiwakaribisha Wanabiafra





Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (kushoto) akijadiliana jambo na mhamasishaji wa Biafra Chriss matembo (kulia)




Baba wa maerehemu Aboubakari bwana Idd Maganga akiwa na mkewe

Baadhi ya marafiki wa marehemu ambao wote kwa paoja na wanachama wa Biafra


Mwenyekiti wa Biafra Abdull Mollel akikabidhi rambi rambi ya wanabiafra kwa bwana iddi Maganga na mkewe






Katibu wa Biafra ndugu Yahya Poli akiaga kwa niaba ya Wanabiafra

Baada ya kumaliza kutoa rambirambi kwa familia ya marehemu Aboubakar Iddi Maganga, safari ya kurudi klabu ni ilianza.






Tukiwa klabuni, kwa pamoja wanabiafra tulipitisha maazimio mawili (1) Kuundwa kwa Kamati ndogo kwa ajili ya maandalizi ya safari ya Mikumi ambayo itajumuisha baadhi ya wajumbe wa Kamati zote za Klabu, na (2) Kila mwanachama kuchangia kiasi cha Shilingi elfu tano ikiwa ni ada ya kila mwezi ya uanachama kuanzia mwezi Julai, 2013.


No comments:

Post a Comment