Monday, February 20, 2012

VILABU VYA 'JOGGING' VYATEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII BAGAMOYO TAREHE 19 FEBRUARI, 2012

Katika kuhamasisha utalii wa ndani na michezo, hasa mchezo wa mbio za pole pole, klabu za michezo za Kunduchi Kwanza, Biafra na Namanga, Sotojo na Kawe zatembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika mji wa Bagamoyo ambao ni mmoja kati ya miji mikongwe na wa kihistoria.  Ziara hiyo ya Kihistoria iliandaliwa na kuratibiwa na klabu ya Kunduchi Kwanza. Vilabu vyote vilikutana kuanzia saa 12:45 asubuhi katika mji wa Bagamoyo na kuanza mbio za pole pole moja kwa moja kuelekea katika magofu ya kale ya Kaole ambayo yapo takriban kilomita saba kutokea Bagamoyo mjini.
Wanabiafra Michael Silili na Ally Juma katika picha ya pamoja na mwanadada kutoka klabu ya Kawe punde tu baada ya kuwasili Bagamoyo

Baadhi ya wanakunduchi kwanza wakijiandaa kwa kuimba nyimbo za kuhamasishana kufanya mazoezi ... Zaina zaina! Zaina mtoto Zaina, mtoto wa Kunduchi zaina...!!!

Baadhi ya wanabiafra wakiongozwa na Ally Juma mwenye filimbi wakijumuika kwenye mbio punde tu baada ya kuwasili Bagamoyo

Mamaa Chimbinga aka Rose Mwakibugi akiiwakilisha vyema  klabu ya Biafra

Klabu ya kawe iliwakilishwa vyema kama unavyoona wanakawe wakiwa wamependeza na jezi zao za bluu
Mwenyekiti wa klabu ya Biafra Abdul Mollel akiwaongoza wana-jogging kukatiza maeneo ya Taasisi ya Sanaa bagamoyo (TaSuBa) kuelekea kuelekea Kaole
Watoto wadogo pia walikuwa ni sehemu ya washiriki wa mbio za polepole - pichani ni katibu wa klabu ya Biafra akikimbia na mtoto mdogo kuliko watoto wote waliohudhuria mbio hizo

Baadhi ya watoto kutoka vilabu mbalimbali

Watu wazima nao hawakukosa - pichani ni Henry Maseko (mwenye fulana nyeupe) akiwakilisha klabu ya Biafra
Sehemu ya watoto walioshiriki mazoezi kutoka vilabu mbalimbali wakiimba kwa hisia na hamasa kubwa ... chikichi chaaaa! x2
kina dada nao hawako nyuma katika kufanya mazoezi kama wanavyoonekana wakiongoza Jacqueline Barozi na Editha Tungaraza (wenye fuana nyeupe)

wengine mzuka ulipanda wakaanza kucheza na kwaito katikati ya mbio

Katika kuhakikisha usalama wa wakimbiaji wote mshika bendera wa Biafra Ramadhan Said alikuwa makini kuhakikisha hakuna gari, pikipiki au bajaj inayokuja kwa kasi kuonyesha bendera nyekundu kwa madereva

Back-Benchaz hata kwenye mbio wapo sio darasani tu

Aerobics iliendelea mara tu baada ya kuwasili kwenye Magofu ya Kaole kama anavyoonekana Ally Masharubu akitoa maelekezo

Watu hoi baada ya kukimbia mwanzo hadi mwisho bila kuchoka- pichani ni Robert Mwakibugi na Acholo Luvanda

kutoka kushoto ni Henry Maseko, Kaka Poli, Abdul Mollel, Charles Juma wakiwa wamesimama kwenye kibla ya msikiti wa kale kabisa

baadhi ya wana-jogging wakifuatilia kwa makini maelezo ya historia za magofu mbalimbali

Mwendo ule ule, baada ya kumaliza utalii kwenye magofu ya kale pale Kaole wana-jogging walirudi mjini kwa kukimbia kama wanvyoonekana Chande Kukuru, Michael Silili na Ismail Hamad wakiongoza mbio hizo
Wana-jogging wakijiburudisha mara tu baada ya kurejea toka magofu
Wengine waliamua kwenda kwenye fukwe za Badeco kupumzika na kupata upepo mwana wa bahari

unaogopa?!! Mbona mi nimemshika - Noah Machaka aakiwa amemshika nyoka

Tumepapenda sana - kutoka kushoto ni Mbusilo Joseph, Emmy Msechu na Mwajuma Usale wakifurahia mandhari nzuri na upepo mwanana wa fukwe za Bagamoyo

Ally Juma na Michael Silili

Michael C Juma - mtunza hazina wa klabu ya Namanga











2 comments:

  1. Dah, ilikuwa nzuri sana hiyo, michezo na utalii!

    ReplyDelete
  2. hii kitu kilikuwa cha kihistori yani kila mtu alifurahia mana wengine huenda ilikuwa ndio mara ya kwanza na hatukuwa na mawazo kama tutafika shukrani kwa uongozu kufanya kitu kama kile

    ReplyDelete