Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 juni, 201 wanamichezo toka katika klabu ya Biafra waliamua kutembelea kituo cha kulelea wasiojiweza cha "Missioneries of Charity (Mother Teresa) Children's Home" Mburahati Madoto maarufu "Kwa Mama Tereza". Lengo la kutembelea la safari hiyo lilikuwa ni kujumuika pamoja na watoto wanaolelewa kituoni hapo na kutoa misaada ya kibinadamu kama vile chakula, mavazi na vifaa vya shuleni na pia kushirikiana na watendaji wa kituo hicho katika kazi mbalimbali kama vile kufanya usafi, kufua na kuwakutanisha watoto wanaolelewa kituoni hapo na watoto wenzao ili kuwa na wakati mzuri na kufurahi pamoja kucheza.
Mratibu wa zoezi la ukusanyaji misaada Bi. Mariam Sabaje akiipanga mara baada ya kukabidhi |
Zoezi la kutupa taarifa mbalimbali za kituo hicho lilifanyika na hatimaye tulipata fursa ya kuwasabahi watoto wanaolelewa kituoni hapo pamoja na watu wengine wakiwemo wazee na wafanyakazi.
Katibu Mkuu wa Biafra Yahya Poli akimsikiliza kwa makini Sister Saviona |
Wanabiafra wakisikiliza historia ya Kituo cha Mama Tereza toka kwa Sister Saviona (hayupo pichani) |
Katibu wa Kamati ya Ufundi Ally Juma akiongoza msafara kutembelea maeneo mbalimbali kituoni hapo |
Baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni wakichangamana na Wanabiafra |
Hamza Kimathy akiwa na mtoto |
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Biafra - Ally Selemani pamoja na watoto |
Ally Juma |
Watoto wakifurahi picha |
Mhamasishaji na mwimbishaji wa Biafra Chriss Matembo (wa pili kushoto waliosimama) akiwa na Makamu Mwenyekiti na watoto |
Mara baada ya kutembezwa maeneo mbalimbali na kuwasalimia watoto kazi mbalimbali zilianza kufanyika ikiwemo kufua, kufagia na kupiga deki, kufuta vumbi madirisha na pia kupiga hadithi na watoto, fuatilia matukio yote kwenye picha.
Zoezi la kufanya usafi lilikamilika na wakati wa mapumziko wanabiafra waliutumia vyema kujadiliana mambo mbalimbali waliyojifunza kituoni hapo pamoja na kuzungumza na wazee wanaoishi kituoni.
Hatimaye siku maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa mwaka 2013 kwa wanabiafra yalikamilika majira ya saa 6:30 mchana kwa kuwashukuru wahusika wote katika Kituo cha Mama Tereza kutukubalia ombi letu la kuwatembelea na pia uongozi pamoja na wafanyakazi na watoto kituoni hapo walitoa shukrani kwa kuwa pamoja nao na kuomba tuwe na utaratibu wa kwenda mara kwa mara. Baada ya shukrani, safari ya kurudi klabuni ikaanza kwa mwendo mdogomdogo hadi njia panda ya Madoto na kisha kupanda gari.
Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Michezo ya Biafra, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wanachama wote kwa kujitolea vitu mbalimbali na kujitokeza kwa wingi. Vile shukrani za dhati ziwaendee wadau wetu Janice Mlunde na Faraja Emmanuel kwa kujitolea nguo kadhaa za watoto pamoja na sukari.
Kutoka kushoto; Mwajuma Mohamed, Zawadi Rajab, Emmy msechu na Mariam Sabaje |
Abdallah Omari (kulia) na Ibrahim Kilasa |
Chriss Matembo |
Vijana wakifua |
Magreth Warisanga (mwenye kofia) akifua pamoja na Jaqueline Barozi |
Nancy Raphael (kushoto) akisaidiana kufua |
Salma Mathias aifuta dirisha |
Zawadi Rajab (mwenye kitambaa) na Mariam Sabaje wakipiga deki |
Salma Mathias akisuuza nguo |
Henry Maseko |
Makamu M/Kiti Jqueline Barozi akianika nguo |
Rehema Shaban na Miriam Joseph wakinika nguo |
Watoto wakicheza pamoja |
Mossi Said akiwahidithia hadithi kwa watoto |
Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Michezo ya Biafra, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wanachama wote kwa kujitolea vitu mbalimbali na kujitokeza kwa wingi. Vile shukrani za dhati ziwaendee wadau wetu Janice Mlunde na Faraja Emmanuel kwa kujitolea nguo kadhaa za watoto pamoja na sukari.
No comments:
Post a Comment