Jumapili ya tarehe 23 Juni, 2013 ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwa wanamichezo hususani katika tasnia ya mbio za pole pole (jogging) kwa kumpoteza mwanachama wa klabu ya jogging ya Kopa - Mwananyamala Bi. Hellen Michael aliyefariki katika ajali ya gari ambayo ilitokea maeneo ya Viktoria, Barabara ya Mwai Kibaki, Kinondoni majira ya asubuhi. Ajali hiyo ambayo pia imeacha wanamichezo tisa wakiuguza majeraha huku wawili kati yao wakilazimika kufanyiwa upasuaji. Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani majira ya saa 10:30 jioni na maziko yalifanyika saa 11 kasorobo jioni. Fuatilia matukio mbalimbali kwa picha.
|
Katibu Mkuu wa M'nyamala Jogging ambaye pia alikuwa ni mmoja wa waratibu wa shughuli za msiba akitoa taarifa mbalimbali za maandalizi ya mazishi |
|
Katibu Mkuu wa Mzimuni Jogging Kabambura akitoa ufafanuzi wa jambo |
|
Baadhi waombolezaji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed (Mwenye kofia) na Katibu wake Alphonsina Jospeh (mwenye mkoba) |
|
Yahya Poli (katikati) Mratibu wa msiba akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed na Kocha Said wa Faita Jogging | | | | | | |
|
|
Jeneza lenye mwili wa marehemu Hellen Michael lilipowasili nyumbani kwa ajili ya mazishi |
|
Mwili wa marehemu ukiswali tayari kwa ajili ya kuzikwa |
|
Wana-jogging walipanga mstari kuanzia nyumbani mpaka makaburini |
|
Diwani wa kata ya Mwananyamala Songoro Mnynge (mwenye suti) alikuwa ni sehemu ya waombolezaji |
Kwa niaba ya uongozi wa Chama cha Jogging - Kinondoni, katibu Mkuu ndugu Yahya Poli anatoa pole tena kwa wafiwa na kuhimiza mshikamano miongoni mwa wana-jogging katika matukio kama haya. Tunamuombea pia marehemu Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.
No comments:
Post a Comment