Tuesday, June 05, 2012

KLABU YA BIAFRA YAITISHA MKUTANO MKUBWA WA WANACHAMA, MASHABIKI NA WADAU WAKE

Katika harakati za kuiimarisha klabu, Mwenyekiti wa klabu ya Michezo ya Biafra Bw. Abdul Mollel, kupitia Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ameitisha mkutano mkubwa ambao utawakutanisha wanachama wote, mashabiki na wadau wa klabu hiyo pamoja na wanamichezo kwa ujumla mnamo tarehe 8 Juni, 2012 siku ya ijumaa. Mkuktano huo unatarajiwa kuanza saa 12:30 jioni na kumalizika saa 2:30 usiku na utafanyika makao makuu ya klabu 90 Degrees Pub Kinondoni.
Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (kushoto) akiwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu Ally Selemani almaarufu Masharubu

Wanabiafra wakiwa klabuni

Wanabiafra: kutoka kushoto; Robert Mwakibugi, Dastan Barozi, na mgeni wao klabuni


Akitoa taarifa za mkutano huo, Katibu Mkuu wa klabu ya Biafra alieleza kuwa pamoja na masuala mengine, ajenda za mkutano huo ni: -
  1. Kupata taarifa na kujadili maendeleo ya klabu
  2.  
  3.  Ushiriki wa wanabiafra katika shughuli mbalimbali za klabu vikiwemo vikao na mazoezi,
  4.  
  5.  Kupokea mpango kazi wa mwaka wa klabu (Juni - Disemba, 2012)
  6.  
  7. Kugawa sare (uniform) kwa wanachama waliolipia.

Akitoa msisitizo, Katibu Msaidizi wa klabu Betwely Kyando (pichani chini) alieleza kuwa kikao hicho ni muhimu sana hivyo kila mwanachama, mshabiki na mdau wa Biafra anapaswa kuhudhuria bila kukosa kwa kuwa masuala yatakayojadiliwa yatasaidia harakati za kuimarisha klabu na mchakato wa kuleta maendeleo kwa wanachama kwa ujumla.
Betwely Kyando - Katibu Msaidizi, Biafra Sports Club

Kwa maelezo, maoni, ushauri, au ungependa kushiriki kwenye mkutano huo, wasiliana na Katibu Mkuu kwa barua pepe (biafra.jsclub@gmail.com) au kwa simu +255 715 253 653.



NYOTE MNAKARIBISHWA
     

2 comments:

  1. dah hii safi sana

    ReplyDelete
  2. Naomba muweke taarifa za kikao hicho pamoja na fomu za kuomba uanachama mtandaoni.

    ReplyDelete