Tuesday, February 28, 2012

BIAFRA SPORTS CLUB YATOA SHUKRANI KWA MASHABIKI WALIOTEMBELEA BLOGU YA KLABU

Blogu ya klabu ya michezo ya Biafra ilianzishwa mnamo mwezi Agosti, 2011 ikiwa kama ni kiunganishi mahususi cha kupashana habari miongoni mwa wanachama, mashabiki pamoja na wadau wengine ulimwenguni kote. Kuanzishwa kwake kulileta hamasa kubwa miongoni mwa klabu nyingine za michezo hasa zile zinazojihusisha zaidi na mchezo wa mbio za pole pole (jogging) ambapo kufikia januari mwaka 2012 moja ya klabu iliyohamasika na kufungua blogu yao pia. Hadi kufikia mwezi Februari 2012 blogu imeshatembelewa na watu zaidi ya 1440 kutoka mataifa mbalimbali duniani kama takwimu zinavyoonesha.


Kikosi cha Biafra Kids - The Juniors

Wanabiafra wakiwa kwenye mbio za pole pole za kila jumapili

Baadhi ya viongozi na wanachama wa Biafra Sports Club


Wanachama wa Biafra Sports Club wakiingia hospitali ya mwananyamala 'kimya kimya' kwa ajili ya kufanya usafi kuadhimisha miaka 50 ya uhuru 9/12/2011

Uongozi na wanachama unatoa shukrani kwa wale wote waliopata fursa ya kutembelea blogu na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu, na pia shukrani ziwaendee wanablogu pamoja na wanamtandao kwa kushirikiana kwa ukaribu kwa aidha kuweka habari mbalimbali zinazotolewa na klabu na/au kuweka kiunganishi 'link' ya blogu ya klabu kwenye menu za blogu zao kama vile Issa Michuzi, Maggid Mjengwa, Ahmad Michuzi, Shaffih Dauda, n.k.


Mwanabiafra Michael Silili akimjulia hali na kumfariji mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya Mwananyamala

Wanabiafra wakitoa maji na sabuni kwa wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala

We! We! Mazoezi ni Afya .... Acha Kujiachia!!!

Wanabiafra wakijipatia chakula pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu

Hati ya usajili wa klabu


Tuendelee kushirikiana katika kudumisha michezo, kupashana habari na kuimarisha afya zetu.

Monday, February 20, 2012

VILABU VYA 'JOGGING' VYATEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII BAGAMOYO TAREHE 19 FEBRUARI, 2012

Katika kuhamasisha utalii wa ndani na michezo, hasa mchezo wa mbio za pole pole, klabu za michezo za Kunduchi Kwanza, Biafra na Namanga, Sotojo na Kawe zatembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika mji wa Bagamoyo ambao ni mmoja kati ya miji mikongwe na wa kihistoria.  Ziara hiyo ya Kihistoria iliandaliwa na kuratibiwa na klabu ya Kunduchi Kwanza. Vilabu vyote vilikutana kuanzia saa 12:45 asubuhi katika mji wa Bagamoyo na kuanza mbio za pole pole moja kwa moja kuelekea katika magofu ya kale ya Kaole ambayo yapo takriban kilomita saba kutokea Bagamoyo mjini.
Wanabiafra Michael Silili na Ally Juma katika picha ya pamoja na mwanadada kutoka klabu ya Kawe punde tu baada ya kuwasili Bagamoyo

Baadhi ya wanakunduchi kwanza wakijiandaa kwa kuimba nyimbo za kuhamasishana kufanya mazoezi ... Zaina zaina! Zaina mtoto Zaina, mtoto wa Kunduchi zaina...!!!

Baadhi ya wanabiafra wakiongozwa na Ally Juma mwenye filimbi wakijumuika kwenye mbio punde tu baada ya kuwasili Bagamoyo

Mamaa Chimbinga aka Rose Mwakibugi akiiwakilisha vyema  klabu ya Biafra

Klabu ya kawe iliwakilishwa vyema kama unavyoona wanakawe wakiwa wamependeza na jezi zao za bluu
Mwenyekiti wa klabu ya Biafra Abdul Mollel akiwaongoza wana-jogging kukatiza maeneo ya Taasisi ya Sanaa bagamoyo (TaSuBa) kuelekea kuelekea Kaole
Watoto wadogo pia walikuwa ni sehemu ya washiriki wa mbio za polepole - pichani ni katibu wa klabu ya Biafra akikimbia na mtoto mdogo kuliko watoto wote waliohudhuria mbio hizo

Baadhi ya watoto kutoka vilabu mbalimbali

Watu wazima nao hawakukosa - pichani ni Henry Maseko (mwenye fulana nyeupe) akiwakilisha klabu ya Biafra
Sehemu ya watoto walioshiriki mazoezi kutoka vilabu mbalimbali wakiimba kwa hisia na hamasa kubwa ... chikichi chaaaa! x2
kina dada nao hawako nyuma katika kufanya mazoezi kama wanavyoonekana wakiongoza Jacqueline Barozi na Editha Tungaraza (wenye fuana nyeupe)

wengine mzuka ulipanda wakaanza kucheza na kwaito katikati ya mbio

Katika kuhakikisha usalama wa wakimbiaji wote mshika bendera wa Biafra Ramadhan Said alikuwa makini kuhakikisha hakuna gari, pikipiki au bajaj inayokuja kwa kasi kuonyesha bendera nyekundu kwa madereva

Back-Benchaz hata kwenye mbio wapo sio darasani tu

Aerobics iliendelea mara tu baada ya kuwasili kwenye Magofu ya Kaole kama anavyoonekana Ally Masharubu akitoa maelekezo

Watu hoi baada ya kukimbia mwanzo hadi mwisho bila kuchoka- pichani ni Robert Mwakibugi na Acholo Luvanda

kutoka kushoto ni Henry Maseko, Kaka Poli, Abdul Mollel, Charles Juma wakiwa wamesimama kwenye kibla ya msikiti wa kale kabisa

baadhi ya wana-jogging wakifuatilia kwa makini maelezo ya historia za magofu mbalimbali

Mwendo ule ule, baada ya kumaliza utalii kwenye magofu ya kale pale Kaole wana-jogging walirudi mjini kwa kukimbia kama wanvyoonekana Chande Kukuru, Michael Silili na Ismail Hamad wakiongoza mbio hizo
Wana-jogging wakijiburudisha mara tu baada ya kurejea toka magofu
Wengine waliamua kwenda kwenye fukwe za Badeco kupumzika na kupata upepo mwana wa bahari

unaogopa?!! Mbona mi nimemshika - Noah Machaka aakiwa amemshika nyoka

Tumepapenda sana - kutoka kushoto ni Mbusilo Joseph, Emmy Msechu na Mwajuma Usale wakifurahia mandhari nzuri na upepo mwanana wa fukwe za Bagamoyo

Ally Juma na Michael Silili

Michael C Juma - mtunza hazina wa klabu ya Namanga











Monday, February 13, 2012

TAREHE YA MWISHO YA KUCHUKUA FOMU ZA UANACHAMA WA KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA YATANGAZWA

Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Biafra Bw. Abdul Mollel ametangaza kwamba tarehe 15 februari, 2012 kuwa ndio tarehe ya mwisho ya kuchukua fomu za uanachama wa klabu. Tangazo hilo alilitoa mara baada ya kumaliza mazoezi ya mbio za pole pole zilizoandaliwa na kuratibiwa na klabu ya Biafra na namanga. Aliwakumbusha wanachama na wadau wengine wote kuwa tarehe hiyo imepangwa kwa kuzingatia pia kwamba klabu kwa sasa inajiandaa na uchaguzi mkuu wa kwanza wa viongozi ambao umepangwa kufanyika tarehe 11 machi, 2012.
Mwenyekiti wa Biafra Abdul A. Mollel akiongoza mazoezi ya mbio za pole pole (jogging)

ZAMBIA YATWAA UBINGWA WA 'CAN 2012'


'Tumekuja kwenye fainali hizi tukiamini kwamba tunaweza kushinda na baada ya ushindi wa mechi yetu ya kwanza tulijua kabisa kwamba hii ndio njia yetu ya kuwa mabingwa wa Afrika'. Hii ni kauli ya Kennedy Mweene,  golikipa mahiri wa timu ya taifa ya Zambia almaarufu Chipolopolo ambayo aliitoa jana wakati akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya timu yake kuibwaga timu ya taifa ya Ivory Coast kwa mikwaju ya penati katika fainali hiyo.

Golikipa wa Zambia Kennedy Mweene akidaka mpira kichwani mwa Gervinho





Wednesday, February 08, 2012

NEMBO RASMI YA KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA YAANZA KUTUMIKA

Katika kuirasimisha klabu yao, viongozi na wanachama wa klabu ya michezo ya Biafra wameanza rasmi kuitumia nembo mahususi ya klabu kama inavyoonekana hapo juu. Kwa kuwa klabu ina lengo la kuhamasisha michezo hususan mchezo wa mbio za pole pole ambazo hujulikana kama 'jogging' katika nembo ya klabu wanaonekana wa watu wawili wakikimbia kwa mtindo wa mbio za pole pole. Lakini bila kusahau michezo mingine, kuna picha ya mpira pamoja na ya mwanamasumbwi. Hiyo ni kwa uchache tu.

Tuesday, February 07, 2012

MICHUANO YA 'CAN 2012' YAELEKEA UKINGONI


Kwa wale mashabiki wa soka, hasa soka ya barani Afrika, tunafahamu kabisa kwamba michuano ya 'CAN 2012' inayoendelea huko 'Equatorial Guinea na Gabon inakaribia kabisa kufikia ukingoni ambapo fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kufanyika mnamo Februari 12, 2012 nchini Gabon. Chini hapa nimekuwekea ratiba ya michuano hiyo kuanzia hatua ya robo fainali. 

Wapi unatupa karata yako? Tabiri upate zawadi! Michezo ni Afya, michezo ni ushirikiano na upendo.

Robo Fainali
25.
04/02/2012
17H:00
Bata
26.
04/02/2012
20H:00
Malabo
27.
05/02/2012
17H:00
Libreville
28.
GHANA 2-1 TUNISIA
05/02/2012
20H:00
Franceville

Nusu Fainali
29.
ZAMBIA vs. GHANA
08/02/2012
17H:00
Bata
30.
MALI vs. COTE D'IVOIRE
08/02/2012
20H:00
Libreville

Mechi za kutafuta mshindi wa tatu
31.
Timu iliyopoteza Mechi Na. 29 vs. Timu iliyopoteza Mechi Na.30
11/02/2012
20H:00
Malabo

Fainali
32.
Timu iliyoshinda Mechi Na. 29 v Timu iliyoshida Mechi Na. 30
12/02/2012
20H:00
Libreville

Wednesday, February 01, 2012

KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA YAJIANDAA KUFANYA UCHAGUZI MKUU WA KWANZA WA VIONGOZI WA KLABU


RATIBA YA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA KWANZA WA VIONGOZI WA KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA UTAKAOFANYIKA TAREHE 11 MACHI, 2012.
Mara baada ya kupata usajili rasmi toka serikalini klabu ya michezo ya Biafra imejipanga kufanya uchaguzi mkuu wa kwanza wa viongozi ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 11 Machi, 2011. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Abdul Mollel, ratiba hiyo ya uchaguzi inafuatiwa na uchukuaji wa fomu za uanachama kwa mujibu wa ratiba inayoonekana hapa chini: -
Ratiba ya uchukuaji na urudishaji fomu mbalimbali
1.      Fomu za maombi ya uanachama zimeanza kuuzwa tarehe 28 Januari, 2012
2.      Tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu za uanachama ni 15 Februari, 2012
3.      Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa tarehe 19 - 22 Februari, 2012
4.      Mwisho wa kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi ni tarehe 25 Februari, 2012
5.      Uchaguzi mkuu wa viongozi utafanyika tarehe 11 Machi, 2012
Nafasi za uongozi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni kama ifuatavyo: -
1.      Mwenyekiti
2.      Makamu mwenyekiti
3.      Katibu Mkuu
4.      Katibu Mkuu Msaidizi
5.      Mweka Hazina
6.      Wajumbe watano (5) watakaoingia kwenye kamati ya utendaji
7.      Wajumbe nane (8) wa kamati ya uchumi na mipango
8.      Wajumbe saba (7) wa kamati ya ufundi
9.      Wajumbe saba (7) wa kamati ya nidhamu na rufaa
Kwa maelezo, maoni na maswali wasiliana na katibu wa klabu kwa anuani ifuatayo: -
BIAFRA SPORTS CLUB,
SIMU: +255 715 253 653
HQ: MTAA WA ISELE, 90 DEGREES PUB,  KINONDONI
DAR ES SALAAM.