Tuesday, July 30, 2013

MCHEZO WA MBIO ZA POLE POLE NA USALAMA BARABARANI

"Kuna umuhimu mkubwa sana kwa wana-jogging kutumia vizuri barabara zetu wakati tunapofanya mazoezi ili kupunguza ajali za barabarani". Rai hiyo ilitolewa na Katibu wa Chama cha Jogging Kinondoni ndugu Yahya Poli wakati akitoa salamu za pole kwa wanamichezo wakati wa Msiba wa Bi. Hellen Michael. aliyefariki kwa ajali ya gari wakati akiwa mazoezini.

Ili kuweza kuweza kukimbia barabarani, kuna mambo muhimu ya kuzingatiwa kwa ajili ya usalama wa wakimbiaji Kama yalivyobainishwa hapa chini: - 

1. Kukimbia katika mistari mitatu 
Inashauriwa, kabla ya kuanza mazoezi na kuingia barabara, wanamichezo wote wanapaswa kupanga mistari mitatu iliyonyooka ambapo watoto watapanga mbele ya mistari hiyo. Kupanga mistari mitatu kunawezesha kupunguza usumbufu kwa vyombo vya moto vinavyotumia barabara wakati tukiwa mazoezini. Mara baada ya kupanga na kuanza kuingia barabarani, ni vyema kutumia upande wa kushoto wa barabara. Ni muhimu kwa wakimbiaji wote kuheshimu misari kwa kutoivuruga.
Wakimbiaji wakikimbia katika mistari mitatu

Watoto wakiwa mstari wa mbele kabisa
Angalizo; Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea au kusababisha ajali iwapo wanamichezo watakimbia kiholelaholela kwa sababu wanaweza kuzidi hadi upande wa pili wa barabara hivyo kutoa nafasi finyu kwa watumiaji wa vyombo vya moto kupita. Pia, ni rahisi kuwadhibiti watoto wanapokuwa mstari wa mbele.

2. Kuwa na Waongoza na vifaa vya kuongozea
Waongozaji wa mazoezi ni watu muhimu sana kwa kuwa wao kazi yao kubwa ni kuongoza wanamichezo kufuata njia (route) watakayotumia katika maziezi hayo n pia kuongoza vyombo vya moto barabarani. Waongozaji wanapaswa kuwa wawili na kuendelea ambapo mmoja ataongoza mbele ya wanamichezo na mwingine ataongoza nyuma ya wanamichezo. Ili kuboresha usalama, waongozaji wanapaswa kuwa katika umbali kidogo kati yao na wanamichezo na wanapaswa kuwasiliana. Waongozaji pia wanapaswa kuwa na bendera zitakazozuia na kuruhusu vyombo vya moto wakati wa mazoezi.
Muongozaji wa mbele akiwa na kibendera

3. Huduma ya Kwanza
Wakati wote wa mazoezi panapswa kuwepo na huduma ya kwanza. Huduma ya kwanza humsaidia mtu anapopata matatizo kabla ya kumpeleka hospitali. Vikundi vinapaswa kuwa na watoa huduma ya kwanza na kisanduku cha huduma ya kwanza chenye vifaa na dawa mahususi kwa ajili ya utoaji wa huduma ya kwanza.
Mwanamichezo aliyepoteza fahamu mara tu baada ya kumaliza mazoezi
4. Kushirikiana na wadau wa usalama barabarani (trafiki)
Ni vyema kutoa taarifa kwa wadau mbalimbali wa usalama barabarani likiwemo jeshi la polisi idara ya usalama barabarani angalau juma moja kabla ya mazoezi ili wadau hao wapate fursa ya kujipanga na kutoa ushirikiano na msaada pale itakapohitajika kwa haraka na kwa wakati. 

Monday, July 29, 2013

WANA-JOGGING WAJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MSIBA WA MTOTO WA MAKAMU M/KITI WA MZIMUNI JOGGING

Tasnia ya mchezo wa mbio za pole pole (jogging) ilikumbwa na huzuni kwa mara nyingine tena baada ya kupata msiba ambapo Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Jogging ya Mzimuni bwana Abbas Said almaarufu China amefiwa na mtoto wake aliyekuwa akiitwa Aboubaka tarehe 27 Julai, 2013 na kuzikwa tarehe 28 Julai, 2013 katika makaburi ya Kimamba Magomeni Mwembechai Dar es Salaam. Wadau wambalimbali wa mchezo wa mbio za pole pole walikuwa ni miongoni mwa walioshiriki katika msiba huo na kumfariji mwanamichezo mwenzetu. Fuatilia matukio mbalimbali ya msiba huo katika picha. 
Wanamichezo wakiwasili msibani majira ya saa 4 asubuhi.


Jeneza lenye mwili wa marehemu


Mwili wa marehemu ukiwasili makaburini tayari kwa mazishi
Mwenyekiti wa Kopa Original Jogging bwana Mustafa (mwenye suruali nyeupe)
Shughuli za mazishi zikiendelea
Wanabiafra Aly Juma (kushoto) na Ally Masharubu wakiwa makaburini
Baada ya kutoka makaburini wadau wote tulirejea nyumbani kwa marehemu na kuendelea na itifaki nyingine ikiwemo kukusanya rambirambi pamoja na kupanga mipango mingine ya mazishi kama vile arobaini, n.k. 











































Katibu Mkuu wa Mzimuni Jogging bwana Aboubakar Kabambura akifanya majumuisho ya rambirambi zilizkusanywa toka katika  vilabu vya jogging vilivyohudhuria msibani
Mfiwa akitoa neno la shukrani kwa wanamichezo wote walioweza kuhudhuria msiba wa mwanae

Akipoke mkono wa pole



"Nimefarijika sana kuona umati wa wana-jogging, sikutarajia, tuudumishe na kuuenzi umoja huu" ni maneno aliyoyasema mfiwa kumwambia Katibu wa Biafra Sports Club na Chama cha Jogging Kinondoni (pichani) wakati akiagana na wana-jogging

Safari ya kurejea nyumbani baada ya mazishi

MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI! AMEN

UMOJA NDIO NGUVU TULIYONAYO WANA-JOGGING!!

Sunday, July 28, 2013

MAZOEZI YA MCHAKAMCHAKA (JOGGING) YA JUMAPILI TARE 28 JULAI YAWANOGESHA WANABIAFRA

Wanabiafra leo tarehe 28 Julai, 2013 walijitokeza kwa wingi na kushiriki mazoezi ya mbio za pole pole ambayo yalianzia klabuni, mtaa wa Isere, Kinondoni kisha kuingia barabara ya Kawawa hadi kwenye makutano ya barabara ya Kawawa na Kinondoni, kupitia shule ya sekondari ya Muslim, mwembejini, kona ya tazara mpaka kwenye mataa ya salenda kuelekea barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuelekea sea view na hadi katika fukwe za Agha Khan ambapo walifanya mazoezi ya viungo kwa jumla na hatimaye kurejea klabuni kwa mchakamchaka kupitia barabara zilezile walizotumia. Fuatilia matukio yote katika picha.
Tukiingia barabara ya Kawawa kutokea klabuni



Watoto wakiimba kwa shangwe na hamasa
Tulipofika maeneo ya Manyanya, tulikutana na klabu ya Kopa Original upande wa pili wa barabara kuelekea Moroko ambapo Katibu Mkuu alijumuika nao kuwaunga mkono na kuwasalimia.

Katibu Mkuu wa Biafra akivuka barabara kuwasalimia Kopa Original Jogging

M/Kiti wa Biafra - Abdul Mollel Akiimbisha

Maeneo ya makaburini tukielekea shule ya sekondari Muslim

Wale wa mwisho mwisho


Waongozaji wetu Ally Juma ambaye pia ni katibu wa kamati ya ufundi ya Biafra (mwenye tracksuit nyekundu) na Khamis Magodoro (mwenye kizibao) wakituongoza kuingi barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwenye mataa ya Salendar Bridge

Tukiingia Barabara ya Ali Hassan mwinyi


Tukikatiza maeneo ya Seaview
 Mara
Tukiingia katika fukwe za Agha Khan/Gymkhana
Mduara wa mazoezi ya viungo





Katibu katika vita dhidi ya kitambi
Mara baada ya mazeozi ya viungo ya pamoja na binafsi, tulipata fursa ya kupiga picha ya pamoja ya wanabiafra wote walioshiriki mazeozi kisha safari ya kirudi klabuni ikaanza.


Picha ya pamoja
Safari ya kurudi klabuni

Mollel akiimbisha kwa mzuka

Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Mipango Robert Mwakibugi (mwenye bukta ya bluu akionesha ukakamavu

Tukiwa klabuni baada ya kumaliza mbio
Tunatoa shukrani za dhati kwa jeshi la polisi, idara ya usalama barabarani kwa kuwa wamekuwa wakituonesha ushirikiano wa hali ya juu kila tunapofanya mazoezi ya mbio za pole pole siku za jumapili, mara zote wamekuwa wakituongoza vizuri na kuonesha utayari wa kutusaidia tunapoomba msaada wao.

MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!

Wednesday, July 24, 2013

BIAFRA SPORTS CLUB NA NAMANGA JOGGING WAFANYA MAZOEZI PAMOJA

Kama ilivyo ada, jumapili hii wanabiafra walikutana tena katika mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambazo zilikutanisha pamoja na marafiki zao wa Namanga Jogging katika fukwe za Coco, Dar es Salaam. Fuatilia matukio ya siku hiyo katika picha.
Wanabiafra waliowahi mapema klabuni wakijiandaa kuondoka



Msafara ukingia barabara ya kuelekea ada estate


Tukiingia barabara ya Best-Bite


Tukiingia barabara ya Ally Hassan Mwinyi kuelekea Namanga


Tlikutana na Vegas Jogging kwenye kona ya kuelekea Namanga wao wakielekea barabara ya A.H.Mwinyi









Tukiingia fukwe za coco

Namanga Jogging wakifanya mazoezi ndani ya Coco Beach wakiongozwa na Michael Juma (Mopao)

Biafra waliungana na Namanga na kuendelea na mazoezi ya ufukweni

Baadhi ya wanabiafra katika picha ya pamoja

Watoto wa Biafra pichani

Katibu akiwa pamoja na watoto

Mwanabiafra Ayoub Layson
Mara baada ya mazoezi ya nguvu ya ufukweni kwa pamoja na wana namanga Jogging tulianza safari ya kurejea kwenye ngome zetu kwa mbio za pole pole.
Tukijipanga tayari kuanza safari ya kurudi baada ya mazoezi ya ufukweni

Wakati sisi tunarudi wengine ndio walikuwa wanaenda

Tukielekea barabara ya CCBRT

Tukishusha kilima cha CCBRT

Tukipandisha kilima cha CCBRT kuelekea barabara ya Namanga

Barabara ya Namanga
Hapa ni karibu kabisa na Leecaz ambako ni makao makuu ya Namanga Jogging na waliishia hapo sisi tukaendelea na safari ya kurudi klabuni

Barabara ya Best-Bite
Tukielekea klabuni

Utamu wa mazoezi ya viungo

Tukiwa kwenye kikao


Mara baada ya mazoezi, katika kikao chetu cha kawaida, tuliamua kwa pamoja kuwa jumapili ya tarehe 28 Julai, tutafanya mazoezi ya mbio za pole pole kuanzia klabuni hadi fukwe za Agha Khan kupitia barabara ya Kinondoni, Salendar na Seaview. Tunawakaribisha wote! 

MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!!!!