Monday, January 23, 2012

BIAFRA SPORTS CLUB YAPATA USAJILI RASMI

Kwa furaha, tabasamu na bashasha, klabu ya michezo ya Biafra inapenda kuwaarifu wanachama, wapenzi, mashabiki, wadau pamoja na jamii kwa ujumla kwamba klabu hiyo imepata usajili rasmi na kupewa Namba ya Usajili  9848 tangu tarehe 20 Januari, 2012. Wanachama wote walipata taarifa rasmi ya usajili huo kupitia kwa mwenyekiti wa klabu siku hiyo hiyo kwenye kikao ambacho pamoha na mambo mengine wanachama walijumuika na kufurahi pamoja kwa kufungua 'champagne'.  

Barua inayoonyesha kusajiliwa kwa 'Biafra Sports Club'

Mwanachama mpya wa Biafra Sports Club  dada Edita a.k.a. Mama Ritchie akiibariki 'champagne' iliyotolewa maalumu kwa ajili ya kubariki usajili. Pembeni ni Katibu wa Biafra akisoma ujumbe wa pongezi kwa wanachama


No comments:

Post a Comment