Monday, January 30, 2012

AROBAINI YA MAREHEMU HASSAN kUKURU YAPANGWA KUFANYIKA TAREHE 5 FEBRUARI, 2012

Kwa wanachama, mashabiki, wapenzi na wadau wote wa klabu ya michezo ya Biafra, kwa niaba ya mwanabiafra mwenzetu Chande Kukuru, napenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha kuwa arobaini ya marehemu Hassan Kukuru aliyefariki tarehe 25 Disemba, 2011 kwa ajali ya gari na hatimaye kuzikwa nyumbani kwao Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam tarehe 26 Disemba, 2011 itafanyika Jumamosi tarehe 5 Februari, 2012 Kinondoni.


Mwanabiafra Chande Kukuru (mwenye shati jeusi lenye mistari meupe) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa Biafra Sports Club mara baada ya mazishi huko Bunju.


Wanabiafra wote kwa ujumla wetu tunakumbushwa kumalizia michango yetu ya rambirambi na pia kushiriki kikamilifu katika kukamilisha arobaini ya marehemu Hassan Kukuru.

 Baadhi ya wanabiafra waliohudhuria ibada ya mazishi ya marehemu Hassan Kukuru iliyofanyikakatika msikiti wa Taqwa kabla ya kusafirishwa kwenda Bunju kwa mazishi wakiongozwa na mwenyekiti wa Biafra Sport Club (wa pili kutoka kushoto waliokaa)


"Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raaji'un"
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Hassan Kukuru kwa Amani - Amen


No comments:

Post a Comment