Tuesday, January 24, 2012

CHIMBINGA UNIQUE PUB YADHAMINI NA KUFANIKISHA BONANZA LA VILABU VYA JOGGING WILAYA YA KINONDONI

Siku ya jumapili tarehe 22 Januari, 2012 palifanyika bonanza lililoandaliwa na kuratibiwa na klabu ya michezo ya Biafra na kudhaminiwa na Chimbinga Unique Pub. Bonanza hilo lilishirikisha vilabu vya Namanga, Kunduchi Kwanza, Sotojo, Kawe, Kunduchi Veterani na wenyeji Biafra. Wanamichezo walikusanyika makao makuu ya klabu ya Biafra - 90 Degrees Pub Kinondoni kuanzia saa 12:30 asubuhi na mbio ziliishia katika Pub ya Chimbinga maeneo ya Kota Kinondoni. Fuatilia matukio kwa picha.

         

               Mwimbishaji wa Biafra Michael Silili akiwa na mwenyekiti wake Abdu Mollel

 Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza - Asia Mohamed (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Biafra pamoja na mwanachama Namanga John Gako (mwenye suruali nyeusi)


 Mtunza nidhamu wa Kawe Jogging (mwenye dredlocks) akiteta jambo na wanachama wake

 Baadhi ya wanachama wa Biafra wakibarizi muda mfupi kabla ya kuanza mbio

 Wanamichezo wakijipanga tayari kwa kuanza mazoezi ya mbio za pole pole (jogging)

 Ally Masharubu (mwenye bukta nyeusi) wa Biafra akiongoza mbio katika mitaa ya Stereo Kinondoni

 Ibrahim Kilasa (mwenye miwani) akiwaongoza watoto

 Wanamichezo wakiingia barabara ya Kawawa








Mgeni wa heshima Mzee Mkupete akitoa salam zake





 Katibu wa Biafra akiserebuka na dada Rose Mwakibugi almaarufu mamaa Chimbinga

 King A. Y. Mpore wa Biafra

Champagne ya kubariki siku hiyo ya bonanza ilifunguliwa kwa ustadi mkubwa na Robert Mwakibugi mwanabiafra na mkurugenzi wa Chimbinga Unique Pub 
 Neno la shukrani lilitolewa

No comments:

Post a Comment