Monday, January 23, 2012

BIAFRA KIDS YAANZA MWAKA 2012 VIZURI

Kwa heshima taadhima, viongozi, wanachama na mashabiki wa klabu ya Michezo ya Biafra wanawatakia wadau wote wa michezo heri ya mwaka 2012. Harakati bado zinaendelea na mwaka huu klabu yenu imedhamiria kufanya makubwa zaidi kwa manufaa ya wanachama, mashabiki na jamii kwa ujumla. Tarehe 14 Januari, 2011 pale katika viwanja vya Biafra kulikuwa na fainali ya ligi ya kugombea jezi ambapo kama kawaida timu yenu ya Biafra Kids ilimmenyana vikali na timu ya Mwenge shooting. Mchezo ulimalizika kwa timu ya Biafra Kids kuichabanga timu ya Mwenge Shooting kwa bao 1 bila lililowekwa kimiani na mshambuliaji mahiri wa timu hiyo anayejulikana kwa jina la Hussein Tajuddin a.k.a Chongo (pichani chini). Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa ni Mwenyekiti wa klabu ya Biafra Abdul Mollel ambaye aliongozana na mwanachama mwengine Henry Maseko.
 

No comments:

Post a Comment