Thursday, December 22, 2011

BIAFRA SPORTS CLUB YATOA POLE KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM BAADA YA KUKUMBWA NA MAFURIKO YALIYOTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Klabu ya michezo ya Biafra, inatoa pole kwa wakaazi wote wa Dar es Salaam ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika na mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku ya tatu mfululizo Dar es Salaam na mikoa ya jirani ambayo kwa kiasi kikubwa imepakana na bahari ya Hindi.
 Hapa ni maeneo ya Kinondoni B bondeni kama unaelekea Msisiri

 Bwawa likiwa limefurika na kuingiza maji katika nyumba zinazolizunguka maeneo ya Msisiri
 
Kwa mujibu wa Wakala/Idara ya Hali ya Hewa mvua bado zitaendelea kunyesha na kuleta madhara zaidi. Hivyo, ni wajibu wa wananchi wote kuchukua tahadhari mapema ili kujiepusha na madhara zaidi lakini pia hatuna budi kuwasaidia wenzetu wameathirika na mafuriko haya huku wengine wakikosa makazi, chakula, mavazi na huduma muhimu za kijamii. Mpaka sasa vituo vinavyopokea watu walioathirika na mafuriko haya Shule ya sekondari ya Azania, Shule ya msingi Gilman Rutihinda Kigogo na kwa misaada ya kibinadamu unaweza kupeleka maeneo hayo pia.

 
 
     Inavyoonekana , bado mvua zitaendelea kunyesha hadi jumapili tarehe 25 Disemba, 2011 ambayo itakuwa ni siku ya kusherehekea sikukuu ya x-mass. Unaweza kutembelea blogu ya Muhidini Sufiani, Muhiddini Michuzi, Issa Michuzi, Maggid Mjengwa, John Badi na nyinginezo ili ujionee athari za mafuriko hayo kwa upana zaidi.
           
                                MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA

No comments:

Post a Comment