Thursday, December 15, 2011

ZOEZI LA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA NA KUGAWA MISAADA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA TARE 9 DISEMBA, 2011 LAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA

Klabu za michezo za Biafra, Namanga na Kunduchi Kwanza, katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru (1961 - 2011) ziliazimia kufanya usafi wa mazingira pamoja na kugawa misaada kwa wagonjw katika Hospitali ya Mwananyamala ambayo ni hospitali ya Wilaya Kinondoni. 

Wanamichezo pamoja na wadau wengine wote kutoka Kunduchi, Namanga na maeneo tofauti tofauti ya jiji la Dar es Salaam walianza kuwasili katika viwanja vya Biafra - Kinondoni kuanzia saa 12:30 asubuhi kwa ajili ya kugawiwa fulana zenye ujumbe mahususi kwa ajilia ya siku hiyo pamoja na maandalizi ya kuanza mbio za pole pole (jogging) kuelekea sehemu ya tukio - hospitali ya Mwananyamala.
Kama inavyoonekana pichani, msafara wa wanamchezo uliwasili katika hospitali ya Mwananyamala mnamo majira ya saa 1:20 asubuhi

Ili kuondoa usumbufu wa kelele kwa wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala, wanamichezo waliingia hospitali kwa mbio za pole pole kimya kimya (Picha kwa hisani ya Blogu ya John Badi)

Mara tu baada ya kuwasili lilifuatia zoezi la kugawana vufaa vya kufanyia usafi na majukumu mengine. Pichani ni mwanahabari mkongwe John Badi  (mwenye kamera) pamoja na dada Asia Mo'hd (mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Sports Club na Bw. Tobias Owur (mkurugenzi wa Royal Billy's Lodge)

Zoezi la kufanya usafi wa mazingira likaanza moja kwa moja kama wanavyoshuhudiwa wanamichezo wakizoa taka


Mwanabiafra Robert Mwakibugi hakuwa nyuma katika kuhakikisha shughuli inafanyika kwa ufanisi zaidi, hapa anaonekana akiweka 'gloves'zake vizuri tayari kuingia kazini

Mwanabiafra Robert Mwakibugi kiwakilisha maziwa ya cowbell yaliyotolewa na kampuni ya Promasidor kwa watoto waliolazwa kwenye hospitali ya Mwananyamala 
Viongozi wa klabu za Biafra na Kunduchi wakikabidhi sehemu ya msaada kwa viongozi wa hospitali
Katibu wa hospitali ya Mwananyamala akipokea sehemu ya paketi 500 za maziwa ya tanga Fresh kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa hospitalini hapo
Baadhi ya wasanii wa bendi ya mapacha watatu wakiongozwa na Khalid Chokoraa wakikabidhi maziwa ya Tanga Fresh kwa Katibu wa Hospitali ya Mwananyamala

Khalid Chokoraa akigawa maziwa ya cowbell kwa wazazi katika wodi ya wazazi

Wadau wakiwajulia hali wagonjwa hospitalini

Mwanabiafra mzee Faustin Makima akimkabidhi mmoja wa wagonjwa mche wa sabuni
Mweka hazina wa klabu ya Namanga Michael J almaarufu Mopao akimkabidhi maziwa ya Cowbell moja wa wazazi aliyejifungua wakati wa mkesha wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru

Mwenyekiti wa klabu Kunduchi Kwanza Asia Moh'd akimpa biskuti mtoto aliyelazwa hospitalini hapo kutokana na majeraha ya kuungua moto

Pichani ni dada katibu msaidizi wa Klabu ya Namanga (mwenye suruali nyeusi) na Bi. Everlast wakiendelea na usafi


Akiwakilisha klabu ya Namanga mzee Ibrahim Lincoln almaarufu 'Mjomba'
Wadau wengine walikumbushi enzi kwa kukamata mpini wa jembe na kulima kama wanavyoonekana pichani

Mwanabiafra  Mustafa Muro akifyeka majani

Wanamichezo wakijadiliana

Pichani kutoka kushoto ni Angel, Happy Mdeka na Khamis S. almaarufu Masharubu


 

Wengine walifanya usafi huku wakicheza muziki na tabasamu la hali ya juu kama wanavyoonekana pichani wanamichezo hawa

Mwimbishaji maarufu wa klabu ya Namanga almaarufu Likopa akionesha kipaji cha mchezo wa sarakasi mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi hospitalini hapo

Wanamichezo wengine walichangia damu kwa wagonjwa hospitalini hapo kama anavyoonekana Mama Kenisha mara baada ya kutoa damu akiwa pamoja na wanamichezo wengine

Baada ya kumaliza kazi ya kufanya usafi hospitalini pamoja na kugawa misaada kama ilivyopangwa, wanamichezo wote walirejea makao makuu ya klabu ya Biafra ambapo kulikuwa na burudani kadha wa kadha na likafuatiwa na zoezi la utoaji wa vyeti kwa wahisani, pamoja na klabu zote zilizoshiriki.



No comments:

Post a Comment