Thursday, December 15, 2011

HAFLA YA SHUKRANI KWA WANAMICHEZO WOTE WALIOJITOLEA KATIKA KUFANIKISHA ZOEZI LA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA TAREHE 9 DISEMBA KATIKA PICHA

Baada ya kumaliza kazi ya kufanya usafi hospitalini pamoja na kugawa misaada kama ilivyopangwa, wanamichezo wote walirejea makao makuu ya klabu ya Biafra ambapo kulikuwa na hafla maalumu ya kutoa vyeti kwa wahisani, pamoja na klabu zote zilizoshiriki katika kufanikisha maadhimisho hayo. Mgeni wa heshima kwenye hafla hiyo alikuwa ni Mzee Faustin Makima ambaye ni mwenyeketi wa serikali ya mtaa wa balozi msolomi yalipo makao makuu ya klabu ya Biafra.
Wanamichezo wakicheza kwaito kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa vyeti
 Kwa niaba ya kampuni ya Esoshi General Trading Ltd, ambayo ilitoa paketi mia tano za maziwa ya Tanga Fresh, cheti kilipokelewa na Henry Byarugaba anayeonekana pichani hapo chini.


Mzee Kodi Siara almaarufu Serikali akipokea cheti kwa niaba ya kampuni ya TKT Ltd ambao walijitolea chupa zaidi ya mia tatu za maji ya uhai ya lita moja pamoja na biskuti ambazo ziligawiwa kwa watoto waliolazwa kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya mwananyamala

Robert Mwakibugi akipokea cheti kwa niaba ya kampuni ya Promasidor (PTY) Tanzania. kampuni hiyo ilitoa boksi 20 zenye maziwa ya cowbell ya kopo

Bwana Tobias Owur akipokea cheti kwa niaba ya Royal Billy's Lodge ambao walijitolea mchango wa fedha taslimu pamoja fulana 60

Bwana Benson Simba akipokea cheti niaba ya kampuni ya Dabenco Enterprises ambao walijitolea fedha taslimu katika kufanikisha maadhimisho hayo

Bi. Asha M. Warisanga almaarufu mama Kenisha akipokea cheti kwa niaba ya Ninenty Degrees Pub ambayo ndio makao makuu ya klabu ya Biafra. Picha ya chini akikionesha cheti hicho kwa wanamichezo waliohudhuria hafla hiyo
 Bi. Asia Mohamed ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Kunduchi Kwanza akipokea cheti kwa niaba ya Klabu ya Kunduchi Kwanza ambayo ni miongoni mwa klabu zilizofanikisha kazi hiyo.
Bwana Olest Kalembo (Makamu mwenyekiti wa klabu ya namanga) akipokea cheti kwa niaba ya klabu ya Namanga ambayo ni moja klabu kongwe zinazohamasisha mbio za pole pole katika wilaya ya Kinondoni. Klabu hiyo pia ni miongoni mwa klabu zilizofanikisha zoezi hilo.
Bwana Betwely Kyando (katibu mkuu msaidizi wa klabu ya Biafra) akipokea cheti kwa niaba ya klabu ya Biafra
Mgeni wa Heshima mzee Faustin Makima (mwenye kofia) akiwa pamoja na viongozi wa klabu za Namanga na Kunduchi Kwanza pamoja na Biafra mara baada ya kumaliza zoezi la utoaji wa vyeti

Baada ya kumaliza zoezi la utoaji wa vyeti wadau waliendelea kujipatia vinywaji, chakula na burudani mbalimbali hasa muziki



5 comments: